Updated at: 2024-05-25 10:34:54 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Unga 2 Magi (kikombe kibuwa cha chai)
Sukari 1/3 Kikombe cha chai Mayai 5
Siagi 4 Vijiko vya chakula
Hamira 1 Kijiko cha chakula
Baking Powder 1 Kijiko cha chai
Vanilla 1 Kijiko cha chai
Hiliki zilizosagwa 1 Kijiko cha chai
Sukari ya laini ya unga
(icing sugar) 1 Magi
Jinsi ya kuandaa na kupika
Unavunja mayai, unatia sukari, hamira, baking powder, vanilla na hiliki ikisha unapiga kwa kutumia mchapo wa kupigia keki. Unapiga mchanganyiko kwa muda wa dakika tano.
Unatia siagi kwenye sufuria na unaiyayusha na kuipasha moto mpaka iwe moto ikisha unaimimina kwenye mchanganyiko na unapiga tena kwa dakika mbili tu.
Unatia unga kwenye sinia au bakuli kubwa ikisha unamimina ule mchanganyiko kwenye unga na unaukanda kutumia mkono, mpaka ulainike.
Ukiona unga mwingi basi ongeza maziwa kidogo mpaka uwe sawa, na ukiona unga mwepesi sana basi unaweza kuongeza unga kidogo pia mpaka ukae sawa mfano wa unga wa maandazi.
Sukuma na ukate madonge kama unavyoyaona hapo juu. Tumia kifuniko cha chupa kwa kukatia kiduara kidogo katikakti ya madonge. Ukimaliza kukata madonge yote, yaweke kidogo yavimbe halafu teleka mafuta na uyachome. Ukitoa kwenye mafuta yachuje moto na kabla ya kupoa yawe moto moto yarovye kwenye icing sugar na uhakikishe yote yameenea sukari juu. Ukimaliza tia kwenye sahani acha zipowe na zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:12 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Mchele wa pishori (basmati) - 4
Nyama ya kuku bila mafupa - 1 Lb
Kamba saizi kubwa - 1Lb
Mchanganyiko wa mboga - njegere, karoti,
mahindi, maharage ya kijani (spring beans) - 2 vikombe
Figili mwitu (Cellery) - 2 mche
Vitunguu vya majani (spring onions) - 4-5 miche
Kebeji - 2 vikombe
Pilipili ya unga nyekundu - 1 kijiko cha chai
Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai
Sosi ya soya - 3 vijiko vya supu
Mafuta - 1/4 kikombe
Chumvi - kiasi
MAPISHI
Osha na roweka mchele. Tia kamba chumvi na pilipili nyekundu ya unga. Tia mafuta vijiko viwili katika kikaango (frying pan), kaanga kamba kidogo tu, weka kando. Katakata kuku vipande vidogo vidogo, tia chumvi na pilipili manga. Kaanga kaTika kikaango (ongeza mafuta kidogo) Weka kando. Katika karai, tia mafuta kidogo kama vijiko vitatu vya supu, tia kamba na kuku, tia mboga za mchanganyiko, sosi ya soya na chumvi, kaanga kidogo. (Kama mboga sio za barafu) itabidi uchemshe kidogo. Katakata kebeji, figili mwitu (cellery) na vitunguu vya majani (spring onions) utie katika mchaganyiko. acha kwa muda wa chini ya dakika moja katika moto. Chemsha mchele, tia mafuta kidogo au siagi, chumvi upikie uive nusu kiini, mwaga maji uchuje. Changanya vyote na wali rudisha katika sufuria au bakuli la oveni, funika na upike kwa moto wa kiasi kwa muda wa dakika 15-20 takriban. Epua na upakue katika sahani ukiwa tayari kuliwa.
Jinsi ya kutengeneza Biskuti Ya Keki Kavu (Shortcake)
Updated at: 2024-05-25 10:34:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga - 2 Magi (vikombe vya chai)
Sukari iliyosagwa - 2/3 Magi (kikombe cha chai)
Siagi - 220 g
Unga wa mchele - ½ Magi
Yai -1
Vanilla - 1 kijiko cha chai
MAANDALIZI
Changanya vitu vyote hivyo kwenye bakuli mpaka unga ushikamane. Paka mafuta treya ya kuchomea kisha utandaze kwenye treya ya 20cm kwa 30 cm au (8 in kwa 12 in) Choma kwenye moto 325˚C kwa muda wa saa nzima au mpaka ibadilike kuwa rangi ya dhahabu. Epua acha ipoe kisha kata vipande kama mstatili, weak kwenye sahani tayari kunywewa na chai.
NYONGEZA
Kwa unga huo huo unaweza kutengeneza vibiskuti vya duara duara.
1) Weka karai kwenye moto kiasi
2) Tia siagi
3) Tia tambi uzikaange usiachie mkoni mpaka ziwe rangu ya dhahabu.
4) Weka lozi na zabibu huku unakoroga
5) Tia maziwa na huku unakoroga usiachie mkono.
6) Tia arki
7) Epua karai, tumia kijiko cha chai kwa kuchotea na utie kwenye kikombe cha kahawa nusu usikijaze.
8) Kipindue kwenye sahani utoe kileja.
9) Fanya hivyo mpaka umalize vyote.