Mambo ya msingi kwa mwanamke kuyajua unapojiremba
Updated at: 2024-05-23 14:34:15 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kope nazo humpendezesha mwanamke kuna aina ya rangi za kupaka kwenye kope, lakini zinatofautiana. Ni vyema ukawasiliana na wataalamu wa mambo ya urembo kwa ushauri na siyo kukurupuka. Siyo umemuona fulani kapendeza na aina fulani ya rangi ya kwenye kope halafu na wewe ukakimbilia kupaka, utachekesha. Rangi ya mdomo nayo ni eneo lingine linalompendezesha mwanamke. Ukweli ni kwamba tunatofautiana sana midomo wazungu wanaita âLipsâ Kila mwanamke ana tofautiana midomo na mwingine kwa hiyo hata rangi ya midomo nayo inakwenda sambambana aina ya lips na rangi ya ngozi ya mwili aliyo nayo mwanamke, siyo unajisiriba rangi ya mdomo halafu unaonekana kituko. Wasiliana na wataalamu wa urembo kwa ushauri zaidi. Kucha kwa wanawake ni eneo lingine linolatakiwa kuwekwa katika unadhifu. Kuna baadhi ya wanawake unaweza kukutana nao kucha zao zimelika aidha kwa kung'atwa au kwa kuliwa na fangasi. Ni vyema wanawake wenye tatizo hilo kumuona mtaalamu wa ngozi kwa msaada wa tiba. Unaweza kukutana na mwanamke kucha zake zimelika na zina sharp edges kiasi kwamba akikugusa utadhani umeguswa na msasa. Au akishika Glasi ya Kinywaji ukiangalia kucha utadhani mkono ni wa mwanaume maana kwa jinsi kucha zake zilivyo hata hafanani nazo. Kuna kucha za bandia kama mwanamke ana matatizo ya kucha basi akazinunue kusitiri aibu. Marashi, manukato au unyunyu kama wanavyoita vijana wa mjini ni muhimu kwa wanawake lakini ni vyema nikaweka angalizo. Haipendezi kwa mwanamke anayepulizia manukato yanayonukia sana mpaka yakawakera wengine ni vyema wanawake wakajipulizia marashi yenye staha na yasiyokera. Ngozi ya mwanamke ni bora âsensitiveâ sana na inaakiwa ipakwe aina ya mafuta au lotion yenye virutubisho kulingana na aina ya Ngozi. Kuna wanawake wenye Ngozi ya mafuta âOil Skinâ kuna wenye Ngozi mchanganyiko na kuna wale wenye ngozi kavu (Dry Skin). Ni vyema mwanamke kujua aina ya ngozi yake ili ajie aina ya product ya ngozi anayopaswa kutumia na siyo kwa sababu umemuona mwenzio anapaka aina fulani ya losheni na wewe unakimbilia kununua. Omba ushauri kwa wataalamu wa ngozi watakusaidia. Kuna baadhi ya maduka yanyouza vipodozi wanatoa msaada huo bure kabisa.
Updated at: 2024-05-23 14:34:09 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Watu wengi hupendelea kutumia maji ya moto kuoga pale hali ya hewa inapobadilika na kuwa ya baridi au wakati mwingine mtu anaumwa hivyo anatumia maji ya moto.
Sehemu kama Dar es Salaam ni mara cheche utakuta wakazi wake wanaogea maji ya moto kutokana na hali ya joto katika jiji hilo.
Lakini kwa ajili ya urembo na afya ya ngozi, maji ya moto yanatajwa kuwa ni kitu muhimu sana kama vilivyo vipodozi vingine vinavyoisaida ngozi yako kuwa nyororo.
Hizi hapa ni baadhi ya faida zitokanazo na matumizi ya maji ya moto angalau mara tatu kwa wiki
Maji ya moto husaidia kulainisha ngozi yako tofauti na ukitumia maji ya baridi. Maji ya moto hasa yaliyo katika jakuzi ambapo utatumia muda mrefu kidogo ngozi yako ikiwa kwenye maji, husaidia kuilainisha ngozi yako na kuiweka katika hali nzuri.
Kama huwa unapata matatizo kupata usingizi usiku, amka oga kwa kutumia maji ya moto kwani husaidia kulainisha misuli ya mwili wako na itakaa sawa na utaweza kupata usinngizi.
Kuna wakati mwingine mtu hujisikia uchovu wa mwili na kutotaka kufanya chochote (Off mood). Ukioga kwa maji ya moto yatakusaida kukuondolea uchovu na utajisikia mwenye nguvu na upo tayari kukabiliana na changamoto za siku.
Unapooga kwa kutumia maji ya moto husaidia kuchangamsha ubongo na kuufanya uweze kufanyakazi kwa ufanisi na kwa haraka zaidi.
Ukiachanna na masuala ya urembo, kuoga maji ya moto kunatajwa kuwa ni njia ya haraka ya kusaidia kushusha shinikizo la damu. Tafiti zinaonyesha kuwa mtu mwenye shinikizo la damu la kupanda, akioga kwa maji ya moto husaidia kushusha.
Ukioga kwa kutumia maji ya moto husaidia kusisimu na kuitanua mishipa ya damu hivyo kuwezesha damu kuwa na mzunguko mzuri mwilini.
Licha ya kuwa maji ya moto ni mazuri kiafya, unashauriwa kuto oga kwa maji ya moto sana kwani huathiri ngozi.
Updated at: 2024-05-23 14:34:08 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujit-okeza kama viuvimbe/vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso,kifuani na hata mgongoni.Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani Bacteria.
Kwa lugha ya kidaktari chunusi huitwa Acne Vulgaris.Chunusi ndio ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa kwa mfano nchini Marekani pekee huathiri watu zaidi ya milioni kumi na sa-ba..Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wa-kati wa balehe (adolescents) .
Karibu asilimia 85 ya vijana kati ya umri wa miaka 12 hadi 25 hupata chunusi na zaidi ya asilimia 20 ya wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka ishirini hupata chunusi wakati mwingine hata watoto wadogo pia huweza kupata chunusi hii ni tofauti na watu wengi wanavyofikiria kuwa chunusi ni dalili ya balehe.
Chunusi ni ugonjwa unaoathiri vifuko au glandi za ngozi.Katika ngozi ya binadamu kuna glandi ziitwazo Sebaceous ambazo zipo chini ya ngozi na kazi yake kubwa ni kutoa mafutamafuta yaitwayo Sebum ambayo hu-saidia kuiweka ngozi kuwa nyevu na yenye mvuto.
Wakati wa balehe mwili wa binadamu hutoa Sebum kwa wingi na kwa sababu wakati huu vikemikali vya mwili yaani sex hormones hutolewa kwa wingi hasa hormone ya kiume iitwayo androgen husababisha utoaji wa sebum kuwa mwingi zaidi kuliko kawaida. Sebum inapotolewa kwa wingi huungana na seli za ngozi zilizo-kufa na kutengeneza mchanganyiko mzito kama nta uitwao comedo ambao huziba vishimo vya kutolea joto.
Maambukizi zaidi hutokea pale ambapo vijidudu yaani baktaria vinaposhambulia vishimo vilivyoziba hapo kivimbe ambacho watu wengine huita Pimple hujitokeza pale ambapo Sebum, bacteria, seli za ngozi na seli nyeupe za damu zinapo-changanyika na kujikusanya katika vishimo vya jasho vilivyoziba na eneo husika hupata vivimbe au vipele ambavyo tunaviita chunusi.
Ukubwa wa kipele hutegemea ngozi ya mtu au kiasi cha mchanganyiko nilioeleza hapo juu katika eneo husika.Vipele vinaweza kuwa vidogo au vikubwa. Chunusi wakati mwingine husababisha mabaka katika ngozi hali hii hutokea pale ambapo seli za ngozi zilizoharibika huondolewa na seli mpya kutengenezwa.
Ngozi mpya hutengenezwa kirahisi tu mahali palipokuwa na chunusi hali hii husababisha mlingano usiosahihi wa ngozi na hutoa kidonda ambacho baadaye hubaki kama baka. Chunusi hutokea zaidi katika uso,kifua ,mabega na mgongoni kwa sababu maeneo hayo yana vifuko au glandi za Sebaceous nyingi.
Chanzo halisi cha chunusi hakijulikani.hata hivyo baadhi ya vitu vinavyoongeza uwezekanifu wa kupata chunusi ni;
UMRI â Kama nilivyosema hor-mone/vikemikali hutolewa kwa wingi sana mtu anapofikia umri wa kubale-he.Kemikali hizi huongeza utengenezaji wa nta (sebum) katika ngozi ambayo huchochea kutokea kwa chunusi
VIPODOZI âBaadhi ya vipodozi kama Make-up za kina dada na Sprays za ny-wele zina mafuta ambayo yanaweza kusababisha chunusi kuwa nyingi zaidi.
CHAKULA- Chunusi hazisababishwi na chakula bali baadhi ya vyakula hufan-ya chunusi kuwa nyingi zaidi.
DAWA-Chunusi zinaweza kujitokeza kutokana na kutumia dawa kadhaa kama vile antibiotics,Vidonge vya uzazi wa mpango,steroids na tranquilizers.Steroid ni dawa zenye homoni zilizotengenezwa kitaalamu ambazo wakati mwingine wanariadha huzitumia tofauti na ma-kusudio ili kuongeza unene wa misuli yao.
MAGONJWA- Magonjwa yatokanayo na matatizo katika vikemikali (hormonal disorders) huongeza matatizo ya chunusi hasa kwa wasichana.
MAZINGIRA- Chunusi huweza kuwa nyingi zaidi hasa unapoishi mazingira yenye mafuta,grisi au hewa chafu .Kutoa jasho sana hasa katika mazingira ya joto huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi.
JINSIA-Wavulana hupata sana chunusi kuliko wasichana.
FAMILIA- Wakati mwingine chunusi hujitokeza sana kwa wanafamilia wa familia kadhaa kuliko nyingine.
HOMONI- Mabadiliko ya homoni za mwili hasa wakati mwanamke akiwa katika siku zake,ujauzito au mwanamke anapokuwa na umri mkuwa hupelekea kupata chunusi.
USAFI WA MWILI- Kutumia sabuni zenye kemikali,kujisugua sana na kuzitoboatoboa chunusi au vipele hu-sababisha chunusi kuongezeka zaidi.Kukaa muda mrefu na jasho mwi-lini au kutooga huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi
MAWAZO AU STRESS-Mtu anapokuwa na mawazo mengi vimkemikali kadha hutolewa mwilini ambavyo huwe-za kuchangia au kusababisha chunusi
Vipele au vivimbe vidogo vidogo ambavyo pengine husababisha mwasho au vinavyouma ni dalili ya chunusi.Wakati mwingine huweza kujitokeza kama baka dogo na wakati mwingine mtu anaweza utambuzi wa chunusi unaweza kuwa mgumu kutokana na watu walivyomakini au wanavyojenga wasiwasi kubwa katika mwonekano wao hasa usoni.Ikumbukwe kuwa kutokana mwonekano wa chunusi ni rahisi sana.
Daktari kuzigundua, japokuwa katika familia zetu ni mara chache sana mtu akaenda kumwona daktari au mtaalamu wa magonjwa ya ngozi kwa sababu ya chunusi.Pale inavyotokea hivyo basi hali inakuwa ni mbaya zaidi.Hata hivyo si vibaya kumwona daktari ambaye atakuuliza kuhusu chakula, ngozi, dawa unazotumia na vitu vingine vinavyowe-za.kuchangia mtu kupata chunusi
Matibabu ya chunusi yanajumuisha kupunguza utoaji wa anta (sebamu ), kuondoa seli za ngozi zilizokufa na kuua wadudu yaani bacteria.
Matibabu huweza kutofautiana kutokana na wingia au ukubwa wa tatizo. Suala la kuzingatia ni kuepuka mambo yanayoweza kusababisha chunusi kama nilivyoeleza hapo juu.
Kuna dawa za kupaka ambazo hupaka katika eneo la ngozi lililoathirika kwa chunusi. Dawa hizi hupatikana kama cream,lotion,gel au pad.
Dawa hizi hutumika kutibu chunusi ambazo haziko katika hali mbaya hasa kama kuna vijipele vidogo vidogo tu. Mojawapo ya dawa hizi ni antibi-otic kama zenye mchanganyiko wa gentamyicin na betamethasone au dexame-thasone kama vile Gentrisone au Gentriderm cream, Erythromycin,B-Tex na kadhalika.Pia Persol forte Gel husaidia hasa ukianza na asilimia ndogo (2.5%) na kuen-delea kadri ngozi yako inavyohimili dawa. Gentamycin huua wadudu wanaosababisha chunusi wakati dawa nyingine huondoa mwasho.
Dawa nyingine ni zile zinzolainisha nta au Comedolytics na kufanya vishimo vya jasho kufunguka na dawa nyingine huongeza kasi ya utengenezwaji wa seli mpya za ngozi.
Dawa hizi za kupaka hushauriwa kupakwa angalau mara mbili au tatu kila siku hasa baada ya kusafisha kwa maji safi na sabuni ya kawaida na kukausha kwa taulo eneo lenye chunusi na matibabu yanaweza kuchukua wiki kadhaa.
Wakati mwingine daktari anaweza kumshauri mgonjwa kutumia dawa za kumeza kulingana na wingi au ukubwa wa tatizo.
Dawa kama antibiotics huua wadudu na huzuia chunusi ,dawa hizo ni kama vile Erythromycin topical, Accutane (isotret-inoin), Benzamycin Cleocin T (clindamycin phosphate), Desquam-E (benzoyl peroxide) Minocin (minocycline hydrochloride) na âSi vema kujinunulia mwenyewe tu na kuanza kutumia bila ushauri wa daktari au mtaal-amu wa magonjwa ya ngozi.â
Wanawake wenye chunusi zisizotibika wanaweza kupewa Anti-androgens kama vile baadhi ya vidonge wa uzazi wa mpango.Chunusi sugu hutibiwa kwa ciorticosteroids na anti-iflammatory drugs ambazo hutibu chunusi sugu ambazo huitwa Acne fulminans na hupatikana zaidi kwa vijana.
Kwa nchi zilizoendelea matibabu yanaweza kuwa hata upasuaji mdogo (skin grafting) au plastic surgery kama chunusi imesaba-bisha baka kubwa na kuna njia kama vile Chemical peel ambapo kemikali hupakwa kwenye ngozi na inapokauka kipande au gamba la juu la ngozi huondolewa na kuondoa baka.
Haya hujumuisha lishe bora na usafi wa mwili.Ni vema kuoga mara kwa mara na kujifuta maji kwa taulo safi na kuiweka ngozi katika hali ya ukavu nakuepuka upakaji wa mafuta mengi ya mgando hasa wakati wa joto.
Watu wenye chunusi wanashauriwa kulAa mlo kamili wenye vyakula vyenye madini ya zinki,nyuzinyuzi, matunda, mboga za ma-jani,vitamin B complex na Chromium. Ni vema kuepuka au kupunguza matumizi ya pombe,vyakula vya maziwa, tumbaku, sukari, vyakula vilivyoandaliwa viwandani na vyakula vyenye Iodine nyingi kama vile chumvi
Chunusi haziwezi kutibika kabisa japokuwa iwapo matibabu Yatakuwa sahihi watu 60 kati ya 100 hupona na unapokuwa unatumia dawa usitarajie kupona haraka kwani inaweza kuchukua hata miezi miwili kupata nafuu na zinaweza kujitokeza unapoacha kutumia dawa.Chunusi pia huweza kupona kwa kuacha mabaka ambayo kwa hapa nchini hakuna utaalamu sahihi wa kuyaondoa bali huweza kuondoka kadri muda unavyoenda au kwa kemikali kali ambazo zinaweza kuwa na madhara katika ngozi.
Updated at: 2024-05-23 14:34:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Suala la kutunza nywele za asili wengi hutamani japokuwa ukweli kwamba kuna changamoto kadhaa, lakini kwa mtu aliye makini anao uwezo wa kupata kilicho bora katika nyewle zake. Leo tunaangazia vitu vya kufanya ili kukuza na kutunza nywele za asili.
Kwanza kabisa unapaswa kuzikubali nywele zako na kuzipenda , jambo hilo litapelekea mahusiano mazuri, kuelewa tatizo la nywele zako na kuanza kuchukua hatua taratibu ya kuzipatia uvumbuzi tatizo hilo.
Pili, unapaswa kufanya usafi wa kina wa ngozi na nywele zenyewe kwasababu endapo nywele zitaachwa chafu, basi ule uchafu unaziba matundu ya nywele na kuzuia njia kama vile ambavyo matundu ya uso yakiziba unapata chunusi.
Tatu, ni kulinda unyevu wa nywele . pale zinapooshwa, yale mafuta asilia ya kuzilinda huondoka na uchafu. Nywele inabaki ikiwa na udhaifu fulani maana haiwezi hata kushikilia hayo maji yaliyoo vizuri na zikikauka zinakuwa kavu sana. Ni vizuri kabla hazijakauka vizuri, zikafanyiwa âconditionâ , kwa zile nywele ambazo ni nyepesi na chache pia kuna bidhaa zinasaidia kutunza vizuri unyevu na hivyo kuwa na afya nzuri.
Hatua nyingine ni ya kupaka mafuta kichwani, kwani mafuta yana umuhimu mno katika ukuaji wa nywele na mafuta mazuri ni ya nazi ambayo yamewafaa baadhi ya watumiaji wengi .
Njia nyingine ni ya kuzichambua vizuri nyele kabla ya kuzichana, hapa mtu anatakiwa kuwa na subira na nywele zake , asifanye pupa kuzichana na ikiwezekana aziloweshe maji kidogo halafu ndipo azichane kwa chanuo kubwa lenye upana wa kutosha (wide toothed comb) ili kuzipa afya na kuepuka kujiumiza wakati wa kuzichana.
Pia mtu anayetunza nywele za asili anatakiwa kupunguza matumizi ya vitu vyenye moto katika nywele zake kama vile pasi ya nywele na vingine kama hivyo. Nywele zinatakiwa zichanwe kawaida na ziachwe zikauke zenyewe kwa hewa bila kuzilazimisha.
Vipodozi visivyo salama ni vipodozi ambavyo vina kemikali zinadhuru au zinazoweza kuudhuru mwili na kuusababishia matatizo. Maana hii inaweza kuongezewa na kujumuisha vipodozi vyote ambavyo usalama wake unatia mashaka na vinaweza kuleta madhara kwa mtumiaji.
Updated at: 2024-05-23 14:34:19 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipodozi visivyo salama ni vipodozi ambavyo vina kemikali zinadhuru au zinazoweza kuudhuru mwili na kuusababishia matatizo. Maana hii inaweza kuongezewa na kujumuisha vipodozi vyote ambavyo usalama wake unatia mashaka na vinaweza kuleta madhara kwa mtumiaji.
-Vipodozi ambavyo havijasajiliwa na mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA)
-Vipodozi vyenye viambata (kemikali) vya sumu na vilivyopigwa marufuku na mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA)
-Vipodozi ambavyo muda wake wa matumizi umeisha
-Vipodozi ambavyo havioneshi tarehe ya kuharibika (mwisho wa matumizi)
-Vipodozi ambavyo maelezo yake hayajaandikwa kwa Kiswahili au kiingereza
Vinaweza vikawa ni mafuta, losheni, krimu, pafyumu, poda na kadhalika.
Vingi vikiwa katika lugha ya kiingereza, hizi ndizo kemikali ambazo huongezewa katika vipodozi ili kufanikisha au kusaidia dhumuni lililolengwa kwa kipodozi husika. Viambato vyenye sumu vilivyopigwa marufuku ni:
Angalia kwenye lebo ya kipodozi chako sehemu waliyoandika Ingredients au Contents au neno jingine lolote lenye maana ya Vitu vilivyomo ndani. Hapo angalia kama kuna kiamabato au kemikali yoyote ambayo nimeiandika hapo juu kuanzia namba 1 mpaka 12.
Kama kuna kiambato au kemikali ambayo imepigwa marufuku basi jua kipodozi chako sio salama. Acha kukitumia mara moja na toa taarifa kwa mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA).
Kama hakuna kiambato cha sumu basi kipodozi chako kinaweza kuwa salama. Tatizo linakuja pale watengenezaji wanapofanya uhuni kwa kudanganya au kuficha na kuacha kuandika baadhi ya viambato vilivyomo ndani. Ambalo pia ni kosa kisheria.
Vipodozi visivyo salama vina madhara mengi sana kwa afya ya mtumiaji. Na kama mtumiaji ni mjamzito basi madhara hayo yanaweza kumpata na mtoto aliyepo tumboni.
Pia vipodozi hivi vina athari nyingi sana kiuchumi kwani vitapelekea mtu kutumia pesa tena kugharamia matibabu ya matatizo atakayopata. Madhara hayo ni pamoja na:
-Ugonjwa wa saratani (kansa) ya ngozi, maini, ubongo, mapafu, mfumo wa damu, utumbo mpana na kibofu cha mkojo
-Uharibifu wa ngozi, macho, ini, mapafu na figo
-Magonjwa ya moyo na kutopumua vizuri
-Kutokwa na chunusi kubwa kubwa
-Ngozi kuungua, maumivu makali, ngozi kuwa nyekundu na kutokwa na vipele
-Ngozi kuwa nyembamba sana na laini na endapo ngozi itapata jeraha au kufanyiwa upasuaji, kidonda kitachelewa kupona au hakitapona
-Mzio (Allergy) na muwasho wa ngozi
-Kichefuchefu, kutapika, kusikia usingizi na kizunguzungu
-Magonjwa ya akili, mishipa ya fahamu (hasa kichwani)
-Uharibifu wa ubongo na mtindio wa ubongo kwa watoto wachanga na waliopo tumboni
-Ngozi kuwa laini na kusababisha kupata magonjwa kama fangasi kwenye ngozi au maambukizi ya vimelea vya maradhi
-Kuchubuka kwa ngozi
-Ngozi kuwa na mabaka meusi na meupe au rangi mbalimbali
-Upofu, uziwi na upotevu wa fahamu wa mara kwa mara
-Kuumwa kichwa, kusikia kizunguzungu na kupoteza fahamu
Kama tulivyoona hapo juu mengi ya madhara ya vipodozi visivyo salama ni makubwa na huhatarisha kabisa afya za watumiaji na watoto. Hivyo ni vyema kuvijua na kuviepuka kabisa ili usiweze kupata madhara.
Pili msaidie kumuelimisha ndugu, jamaa na rafiki nay eye ajue na asitumie kabisa vipodozi visivyo salama
Pia ukiona mtu au duka ambalo linauza vipodozi visivyo salama acha kununua vipodozi kutoka kwake na toa taarifa kwa mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa
Epuka kabisa vipodozi visivyo salama. Hata kama vinakuletea matokeo mazuri kiasi gani.
Vifuatavyo ni vipodozi visivyo salama na vimepigwa marufuku kutumika. Epuka kabisa kutumia vipodozi hivi hata kama vinakuletea matokeo mazuri kiasi gani.
Dexamethasone nk)
3.9 Vipodozi vya kupunguza unene vilivyopigwa marufuku
3.10 Vipodozi vya nywele vilivyopigwa marufuku
3.11 Vipodozi vinginevyo vilivyopigwa marufuku
3.12 Vipodozi Vinavyosababisha muwasho vikitumika karibu na macho
TAHADHARI : VIPODOZI VISIVYO SALAMA VIPO VINGI ZAIDI YA HIVYO AMBAVYO VIMEORODHESHWA HAPO JUU NA VINGINE VINGI ZAIDI VINAWEZA VIKAFIKA SOKONI.
Mara zote kuwa makini na vipodozi na pata taarifa, elimu na ushauri kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) na wataalam wa afya, urembo na vipodozi.
Updated at: 2024-05-23 14:33:56 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kama kote duniani, wanawake wengi Tanzania wanatumia vipodozi kama nyongeza ya urembo wao ya kiasili. Ila, kuna makosa maalum zinazofanyiwa kwenye kutumia vipodozi Tanzania. Kuwasaidia dada zetu, Yafuatayo ni makosa 10 ya kuweka vipodozi na jinsi ya kuzirekebisha.
Kuna tabia ya wanawake kunyoa nyusi zao sana, na wengine kuzitoa kabisa. Alafu, wanaishia kuzichora na rangi nyeusi.
Hii inamfanya mwanamke kuonekana kama kikatuni.
Sasa:
Ingawa kupata faundesheni inayofanana na ngozi yako ni ngumu, hasa kwa wanawake weusi zaidi, wanawake wengi wanapata shida na kukubali rangi ya kiasili na wanajaribu kutumia vipodozi kubadilisa rangi yao.
Suluhisho:
Wanawake wengi wanfikiri kwamba kutumia poda nying ndio kupendeza zaidi. Matokeo yake, wanaishia kufanana na jinni.
Suluhisho:
Kutumia kwa usahihi ni tatizo duniani.
Suluhisho:
Badala ya kutumia vidole vyako, utahitaji burashi zifuatayo:
Wanawake wengi wanatumia kope bandia zisizo na ubora. Matokeo yake wanafanana na dolli ya mtoto.
Suluhisho:
Jicho la paka ni njia moja ya kuongeza umaridadi kwa sura yako na kuvutia zaidi. Ila, wanawake wengi wanakosea kuiweka.
Suluhisho:
Wanawake wengi wanatumia konsila kwa nje ya nyusi zao. Tatizo linakuja pale ambapo konsila iliyotumiwa haiendani na ngozi yao. Hii inafanya konsila hiyo kuonekana sana, kwenye picha haswa!
Suluhisho:
Wanawake wanatumia eyeshadow zinazo ngâaa au za rangi kali. Zaidi ya hapo, hawazichanganyi vizuri.
Suluhisho:
Kabla ya kuweka lipstick, hakikisha mdomo yako inaunyevu. Hii ni muhimu sana kwa lipstick yako kuseti vizuri.
Usiweke vipodozi kwa fujo
Kwenye swala la vipodozi, kutumia kidogo ni bora kuliko kutumia nyingi. Unataka urembo wako wa kiasili kuboreshwa, sio kubadalika kabisa.
Kwa kifupi, ukitumia vipodozi lakini unaonekana kama vile hujatumia vipodozi, basi hapo ndio utakuwa umepatia.
Updated at: 2024-05-23 14:33:57 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Unaweza kujiuliza, hivi inawezekanaje kuwa na umbo dogo la aina hii? Ukweli ni kwamba inawezekana, lakini inahitaji kazi ya ziada kufikia kwenye lengo hilo.
Kwa wale wanaojali maumbo ya kupendeza saizi zero linatafsiriwa ni kuwa na kiuno kisichozidi inchi 23, nyonga 32 na kifua 31. Kikubwa unachotakiwa kuzingatia ni mazoezi na ulaji wako, kwa kuwa mwangalifu katika kiasi cha kalori unachoingiza mwilini kila siku.
Unatakiwa kuwa mwadilifu katika uchaguaji wako wa chakula, haimaanishi ukae na njaa. Inawezekana ikawa ni vigumu kuelewa makala haya.
Kinachosisitizwa katika mpango huu, ni kuwa waangalifu katika upangiliaji wa vyakula. Aina hii ya mpangilio wa ulaji inafahamika zaidi kitaalamu kama âcrash dietâ Kula kiasi cha kalori 400- 500 kwa siku. Lakini unatakiwa kufanya mazoezi angalau kwa saa mbili kwa siku, ili kupunguza mara mbili ya kiasi cha mafuta uliyokula katika siku hiyo.
Kwa kunywa kiasi kikubwa cha maji itakusaidia kurahisisha umengâenyaji wa chakula mwilini. Ni vyema mwili wako ukawa na maji ya kutosha ikiwa umeingia kwenye mpango huu wa ulaji Kula mboga za kijani: Zina Vitamini, protini na virutubisho vingine kwa wingi ambavyo ni muhimu kwa afya. Kama ilivyoainisha awali, utaratibu huu hauhamasishi kukaa na njaa, bali kula vyakula vilivyo bora kiafya.
Mara nyingi vyakula vya aina hii, huwa na virutubisho muhimu na vinavyohitajika katika ustawi wa mwili.
Badala yake unaweza kula protini na kuingiza vyakula kama mayai na samaki kwenye mlo wako.
Vyakula kama chips, mihogo ya kukaanga na jamii yake vinachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza uzito wa mwili na pia hulifanya zoezi la umengâenywaji wa chakula tumboni kuwa gumu.
Supu kama ya kabichi licha ya kujaza tumbo, husaidia katika kurahisisha mfumo wa umengâenyaji chakula tumboni.
Hii itasaidia kukuweka sawa kiafya.
Jizuie kula vyakula vyenye sukari nyingi na hata vile vya mtaani unavyohisi vinaweza kukwamisha mpango wako wa kupungua.
Lakini pamoja na yote jipe mazoezi ya kutosha kama kukimbia, kuruka kamba au mazoezi ya kupunguza tumbo na maziwa
Updated at: 2024-05-23 14:33:59 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Katika miongo kadhaa iliyopita, uvaaji wa wigi umekuwa fasheni katika sekta ya urembo na hutumika hususani na wanawake. Ingawa uvaaji wa wigi huwafanya wanawake hao kuonekana mithili ya mtu aliyevaa kofia ngumu (helmet), lakini yaonekana ni mapendeleo ya wengi.
Wanaume wengi hujiuliza , "Ni kwanini kina mama hupendelea kuvaa wigi na kusuka nywele za bandia?, wakati hupendeza na kuwa warembo zaidi wakiwa na nywele zao za asili"?
Wigi huvaliwa zaidi na kinamama wenye asili ya Afrika au Wamarekani wa asili ya Afrika. Lakini tukiangalia moja ya chimbuko hasa la uvaaji wigi ni ubaguzi uliokuwepo wakati wa utumwa ambapo wale wenye ngozi nyeupe na nywele shombeshombe walipewa kazi za ndani na wale wasio na ngozi nyeupe na nywele zisizo shombeshombe walifanyishwa kazi ngumu za mashambani.
Watumwa waliopelekwa barani Amerika hawakuweza kuzihudumia nywele zao kutokana na hali ngumu, na mabwenyenye waliwashusha hadhi na kuwavunja moyo kwa kuwaambia hawakuwa na nywele bali ni "manyoya".
Lakini sababu nyingine inayodhaniwa kuwaathiri wanawake wa asili ya Afrika ni fikra kuwa mwanamke mwenye nywele ndefu pengine hadi mgongoni ni mrembo zaidi. Pia siku hizi warembo na wanaoshiriki katika mashindano ya urembo hujaribu kurefusha nywele zao ili kuwa na viwango na aina za mitindo ya ughaibuni.
Pamoja na kuwa wanawake wanajaribu kuwa warembo kwa uvaaji wa wigi, zifuatazo ni baadhi ya hasara au madhara kiafya ya uvaaji wigi na usukaji wa nywele za bandia.
Uvaaji wa wigi au nywele za bandia waweza kukusababishia mzio (allergy), endapo malighafi au kemikali zilizotumika kutengeneza wigi hiyo zitasisimua mfumo wa kinga ya mwili wa mvaaji.
Kupata m-ba ni tatizo jingine kutokana na uvaaji wigi, hii hutokana na kukosekana kwa hewa ya kutosha ya Oksijeni katika ngozi ya kichwa (scalp hypoxia) na katika tishu za shina la nywele. Kwa hiyo kama utaamua kuvaa wigi uhakikishe imetengenezwa kwa viwango vya ubora unaotakiwa na inapitisha hewa ya kutosha ya Oksijeni.
Pia waweza kunyonyoka nywele hata kama una nywele nzuri zenye afya, na kama utachagua kuvaa wigi na unataka kuepuka madhara hakikisha kuwa nywele zako ni safi, usilazimishe kuvaa wigi iliyo ndogo na yenye kubana sana, hakikisha unapata muda wa kupata hewa na nywele zako zinapakwa mafuta kuepuka ukavu wa ngozi ya kichwa na nywele kukatika .
Maumivu ya kichwa ni tatizo ambalo laweza kusababishwa na uvaaji wigi au usukaji wa nywele bandia. Wigi iliyo ndogo husababisha mkandamizo kichwani na kusababisha maumivu ya kichwa ya mara kwa mara.
Upotevu wa muda na fedha ni dhahiri kwa kuwa ufumaji wa nywele za bandia waweza kuchukua muda mrefu, itamlazimu mvaaji wigi kubadili kwa kununua mpya kila baada ya muda fulani au kuwa na wigi nyingi kwa ajili kubadili kulingana na fasheni.
Harufu mbaya huweza kujitokeza endapo mba na jasho vitachanganyikana na hupelekea uwepo wa bakteria au fangasi na kusababisha muwasho mkali, hii yaweza kumkosesha raha mvaaji wigi na mwenye kufuma nywele za bandia hasa pale anapokuwa katika majumuiko ya kijamii.Kama utachagua kuvaa wigi hakikisha nywele zako zinasafishwa na shampoo au sabuni, zinakaushwa vizuri na kupakwa mafuta.
Endapo mwanamama atachagua kuvaa wigi,asisahau kuwa nywele zake za asili zinahitaji matunzo,na azingatie wakati wa kununua wigi au nywele za bandia, ahakikishe ananunua yenye ubora unaotakiwa ili kuepuka madhara ya kiafya anayoweza pata kutokana na uvaaji wigi au anapofuma nywele za bandia.
Benson Chonya
Makovu sio kidonda naomba hili uelewe, ila makovu ni alama ya majeraha ambayo yamebaki kwenye ngozi baada ya kupona majeraha.
Kuna baadhi ya watu husumbuliwa na shida ya kuwa na makovu sehemu mbalimbali ya mwili.
Hivyo kama wewe ni miongoni mwao maandishi haya yanakuhusu sana.
Updated at: 2024-05-23 14:34:18 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Makovu sio kidonda naomba hili uelewe, ila makovu ni alama ya majeraha ambayo yamebaki kwenye ngozi baada ya kupona majeraha.
Kuna baadhi ya watu husumbuliwa na shida ya kuwa na makovu sehemu mbalimbali ya mwili.
Hivyo kama wewe ni miongoni mwao maandishi haya yanakuhusu sana.
Unachotakiwa kufanya ni; Pondaponda tango na kisha kutumia mchanganyiko wake kwa kupaka juu ya kovu. Hii husaidia sana kulainisha makovu na ikiwa utatumia kwa muda mrefu huondoa makovu pia.
Unachotakiwa kufanya ni; kata majani hayo na utumie utomvu wake kupaka katika makovu kisha mara baada ya muda Fulani utaona mabadiliko na itapunguza na kuondoa makovu.
Unachotakiwa kufanya; Paka asali juu ya kovu na kuiacha usiku kucha. Rudia mara kwa mara kupaka asali hadi pale kovu litakapotoweka.
Updated at: 2024-05-23 14:34:17 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
leo tutajaribu kuongalia sababu kwanini tunatakiwa tuvae saa za mkoni yaani nini haswa kinatulazimisha kuvaa saa za mkononi , hebu kwa tujue saa za mkononi zilianza kuvaliwa mwaka gani. Kabla ya vita ya kwanza ya dunia kulikuwa kuna saa za mfuko yaani pocket watch saa hizi zilipendwa sana enzi hizo. ila katika kipindi cha mapigano wanajeshi walihitaji saa ambayo itakuwa rahisi kuangalia sio mpaka watoe mfuko hivyo walianza kuvaaa saa mkononi na ikawa rahisi sana kuangalia wakati wa mapigano ..na vita ilivyoisha saa ikaonekana ni style sasa ikabidi watu waanze kuvaa kama fashion mitaani huko ulaya. sasa tuje sababu zinapelekea wewe au mimi kuvaaa saa japo simu zipo