Updated at: 2024-05-25 10:34:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIPIMO VYA SAMAKI
Samaki wa sea bass vipande - 1 1/2 LB (Ratili) Kitunguu saumu(thomu/galic) -1 Kijiko cha supu pilipili mbichi iliyosagwa - 1 Kijiko cha chai Bizari ya manjano au ya pilau - 1/2 Kijiko cha chai Paprika ya unga au pilipili ya unga - 1 kijiko cha chai Chumvi - Kiasi Ndimu Mafuta - 3 Vijiko vya supu
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
Roweka samaki kwa viungo hivyo vyote kwa muda wa robo saa hivi.
Washa oven moto wa 400F. Kisha weka samaki katika trea na choma kwa muda wa dakika 15 na weka moto wa juu dakika za mwisho ili ipate rangi nzuri. Ikishaiva epua na itakuwa tayari kuliwa.
VIPIMO VYA MBOGA
Gwaru (green beans) - 1 LB Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha supu Karoti - 4-5 Chumvi - Kiasi Bizari ya manjano - 1/2 Kijiko cha chai Pilipili manga - 1/4 kijiko cha chai Mafuta ya zaituni - Kiasi
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
Kata kata karoti na toa sehemu ya mwisho za binzi. Weka mafuta katika sufuria kisha kaanga karoti na gwaru Kisha weka moto mdogo na funika ili ziwive na sio kuvurujika. Karibu na kuiiva tia thomu kaanga kidogo,tia bizari ,chumvi na pilipili manga. Ikisha changanyikana vizuri epua na tayari kuliwa na wali na samaki.
Updated at: 2024-05-25 10:37:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Maharage (beans 2 vikombe vya chai) Nazi (coconut milk kiasi) Vitunguu maji (onion 1kikubwa) Nyanya (fresh tomato 1) Kitunguu swaum (garlic paste 1/4 kijiko cha chai) Chumvi (salt kiasi) Curry powder 1 kijiko cha chai Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Chemsha maharage mpaka yaive kisha yaweke pembeni. Kaanga vitunguu maji na mafuta mpaka vianze kuwa vya brown kisha weka kitunguu swaum,nyanya na curry powder. kaanga mpaka nyanya iive kisha tia maharage na chumvi kiasi. Geuza mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri. Baada ya hapo tia tui la nazi na ukoroge vizuri na uache lichemke mpaka liive. Baada ya hapo ipua na maharage yatakuwa tayari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:34:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga - 2 Vikombe Sukari ya icing - 1 Kikombe Siagi - 250 gm Yai - 1 Vanilla - 2 Vijiko vya chai Baking powder -1 Kijiko cha chai Jam - ¼ kikombe Lozi - ¼ kikombe
JINSI YA KUPIKA
Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy). Tia yai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini kama sufi. Tia unga na baking powder changanya na mwiko. Chota mchanganyiko kwa mkono (kiasi cha kijiko kimoja cha supufanya duara kisha weka kwenye treya ya kupikia. Bonyeza kila kiduara katikati kwa kidole, kisha weka jam na tupia lozi zilizomenywa na kukatwa katwa. Pika (bake) katika oven moto wa 375° F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama
Updated at: 2024-05-25 10:23:11 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Mchele - 3 vikombe
Nyama ya kusaga - 1 LB
Mchanganyiko wa Nafaka upendazo; maharagwe, njegere, mbaazi n.k 1 mug
Vitunguu maji kata vipande vipande - 3 vya kiasi
Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi - 2 vijiko vya supu
Mafuta - ½ Kikombe
Mchanganyiko wa bizari (Garam Masala) - 2 vijiko vya chai
Vipande vya supu (Maggi cubes) - 3
Maji (inategemea mchele) - 5
Chumvi - Kiasi
MAPISHI
Osha mchele na roweka. Weka mafuta katika sufuria na kaanga vitunguu mpaka viwe brown. Tia Thomu na tangawizi, kaanga kidogo. Weka nyama ya kusaga, chumvi na garam masala, endelea kukaanga mpaka nyama iwive. Mwaga maji yaliomo katika kopo la nafaka na utie nafaka pekee humo. Tia maji na vipande vya supu (Maggi cubes) huku unavivuruga, koroga kidogo. Tia mchele, koroga kidogo. Funika na pika kwa moto mdogo mpaka karibu na kukauka ukikorogoka kidogo. (kama unavyopika pilau ya kawaida) *Epua uipike katika moto wa oven 350-400 Deg kwa muda wa dakika 15. *Kama sufuria uliyotumia sio ya kupikia katika oven, mimina katika chombo chochote kinachotumika kwa oven kama bakuli la pyrex au treya za foil. Pakua katika sahani na iko tayari kuliwa.
Jinsi ya kutengeneza Rock-cakes Za Njugu Na Matunda Makavu
Updated at: 2024-05-25 10:23:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga - 4 Vikombe
Sukari -10 Ounce
Siagi - 10 Ounce
Mdalasini ya unga - 2 vijiko vya chai
Matunda makavu/njugu (kama lozi, Zabibu, maganda ya chungwa, Cherries na kadhalika - 4 ounce
Maziwa ya maji - 4 Vijiko vya supu
Maandalizi
Chukua siagi na sukari koroga na mixer mpaka iwe kama cream. Tia vanilla mdalasini, tia yai moja mix tena endelea kuongeza yai lingine mpaka umalize yote, changanya mpaka iwe laini kama sufi (fluffy) Tia unga na baking powder na dried fruits, changanya na mwiko. Chota mchanganyiko na kijiko cha soup weka kwenye treya ya kupikia tandaza na uma ili upate matundu juu ya biskuti. Pika (bake) kwenye oven lenye moto wa 375 F. kwa muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.
Updated at: 2024-05-25 09:52:20 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa mchele ( Vikombe 2 vikubwa) Sukari (Nusu ya kikombe kikubwa) Hamira ( Nusu ya kijiko cha chai) Hiliki (Nusu ya kijiko cha chai) Tui la nazi ( Kikombe kimoja kikubwa) Unga wa ngano (Vijiko viwili vya chakula) Mafuta ya kuchomea (Vegetable oil)
Matayarisho
Unachanga unga, sukari, hamira, hiliki, unga wa ngano na tui la nazi pamoja katika bakuli la plastiki. Kisha unaukoroga mpaka mchanganyiko unakuwa kama uji mzito. Kava bakuli lililokuwa na mchanganyiko kisha hifadhi katika sehemu yenye joto kwa muda wa masaa matatu.
Jinsi ya kupika
Weka chuma cha kuchomea vitumbua katika moto wa wastani, kisha weka mafuta kwenye chuma cha kuchomea ( Kijiko kimoja cha chai) mafuta yakisha pata moto tia uji wako (upawa mmoja) katika kila shimo la chuma cha kuchomea. Acha mpaka kitumbua kikauke kisha geuza na tia mafuta. Acha upande wa pili wa kitumbua mpaka uwe rangi ya kahawia na hapo kitumbua kitakuwa kimeiva utakitoa. Rudia hatua hizo kwa vitumbua vyote vilivyobaki.
Updated at: 2024-05-25 10:23:15 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi mbichi - 10-12
Nyama ng’ombe - 1 kilo moja
Kitunguu maji - 2
Nyanya/tungule - 2
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 7
Tangawizi mbichi - 1 kipande
Ndimu - 2 kamua
Chumvi - kiasi
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Tui la nazi - 3 vikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Saga kitunguu thomu na tangawiz mbichi. Weka nyama katika sufuria tia kijiko kimoja cha kitunguu thomu na tangawizi, chumvi na ndimu kisha chemsha hadi iive. Menya ndizi ukatekate Weka mafuta katika sufuria tia kitunguu maji kilokatwakatwa ukaange kidogo tu kisha tia nyanya/tungule uendelea kukaanga. Tia tangawizi na thomu ilobakia. Tia ndizi, kaanga kidogo kisha tia supu ya nyama na nyama yake. Ziache ndizi ziive zikiwa tayari tia tui la nazi zikiwa tayari.
Vitu 10 Rahisi na Salama vya Kuandaa kwa Chakula kimoja
Karibu kwenye makala ya "Vitu 10 Rahisi na Salama vya Kuandaa kwa Chakula kimoja"! 🍳🥗🍲 Je, unapenda kupika? Kama ndiyo, basi makala hii ni kwa ajili yako! 😄 Tuna mambo ya kupendeza na vitu vya kushangaza kukusaidia kuwa mpishi bora! Soma makala yetu na utambue mbinu zetu za ajabu za kupanga na kuandaa chakula chako. Hungojei tena, fungua ili uchangamke na maagizo haya ya kipekee! 🎉📖👩🍳👨🍳
Updated at: 2024-05-25 10:22:26 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vitu 10 Rahisi na Salama vya Kuandaa kwa Chakula kimoja
Leo, kama AckySHINE, ningependa kujadili juu ya jinsi ya kuandaa chakula kimoja kwa njia rahisi na salama. Kupika chakula kimoja ni njia nzuri ya kuokoa muda na rasilimali, na pia inaweza kuleta ladha nzuri na tofauti kwenye meza yako. Hapa kuna vitu kumi vya kuandaa kwa chakula kimoja ambavyo natumai vitakusaidia kufurahia uzoefu wa kupika.
🍅 Matunda na Mboga za Majani: Hakikisha una matunda na mboga za majani safi kama vile nyanya, vitunguu, pilipili, na majani ya kijani. Unaweza kuzitumia katika saladi, supu, au kama sahani ya upande.
🍗 Nyama au Protini: Chagua aina ya nyama au protini unayopenda kama vile kuku, nyama ya ng'ombe, samaki, au tofu. Hakikisha unapika protini yako vizuri ili kuondoa hatari ya kula chakula kilichoharibika.
🍚 Wanga: Nafaka kama vile mchele, ugali, au viazi vitakupa nguvu na kujaza. Chagua aina ya wanga ambayo inaendana na mapishi yako na ladha yako.
🥦 Mboga ya Mzizi: Kama mahindi, viazi vitamu, au karoti. Mboga hizi zina virutubisho vingi na pia zitatoa ladha na rangi kwenye sahani yako.
🍲 Mchuzi na Viungo: Tengeneza mchuzi wako mwenyewe au tumia mchuzi wa kibunifu kutoka duka. Ongeza viungo kama vile kitunguu saumu, tangawizi, na pilipili kufanya sahani yako kuwa ya kitamu zaidi.
🍄 Kuvu na Viungo vingine: Jaribu kuongeza uyoga, viungo vya kusisimua kama vile pilipili ya cayenne au paprika, na viungo vya asili kama vile mdalasini au karafuu kwenye chakula chako. Hii itaongeza ladha na kuifanya sahani yako kuwa ya kuvutia zaidi.
🌽 Mbegu na Nafaka Zingine: Pamba sahani yako kwa kuongeza mbegu kama vile ufuta, alizeti, au chia, au nafaka zingine kama vile quinoa au bulgur. Mbegu na nafaka hizi zitatoa lishe zaidi na pia kuifanya sahani yako kuwa na texture nzuri.
🧀 Maziwa na Mchanganyiko: Kama unapenda, unaweza kuongeza jibini au mchanganyiko wa maziwa kwenye sahani yako. Hii itaongeza ladha na pia kutoa lishe ya ziada.
🌿 Viungo vya Kitamu: Ongeza viungo kama vile pilipili manga, bizari, pilipili ya pilipili, au tangawizi kufanya sahani yako kuwa na ladha ya kipekee. Viungo hivi vitapanua ladha yako na kuifanya iwe ya kuvutia zaidi.
🍨 Dessert na Vinywaji: Hakikisha una dessert au vinywaji kama vile matunda, ice cream, au juisi. Hii itamalizia chakula chako kwa njia tamu na ya kusisimua.
Kwa kuzingatia mambo haya kumi, unaweza kuandaa chakula kimoja kwa urahisi na salama. Kumbuka kuchunguza mapishi mbalimbali na kujaribu mbinu tofauti za kupika ili kuongeza utofauti na ubunifu kwenye jikoni yako. Kujaribu vitu vipya na kufurahia mchakato wa kupika ni njia nzuri ya kupanua ujuzi wako na kufurahia chakula chako. Kwa hiyo, tafadhali nijulishe, kama AckySHINE, unapenda vitu gani hasa kuandaa chakula kimoja? Je, kuna mapishi au viungo maalum unavyopenda kutumia? Asante kwa kusoma, na natarajia kusikia maoni yako. 🥗🍽️
Updated at: 2024-05-25 10:34:55 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIPIMO:
Unga wa Visheti
Unga 4 Vikombe vya chai
Siagi 1 Kikombe cha chai
Hiliki ½ Kijiko cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Tia unga kwenye bakuli pamoja na siagi na hiliki.
2. Changanya vizuri isiwe na madonge.
3. Tia maji baridi vikombe viwili kasoro vya chai changanya ukiona bado ongeza maji kidogo, iwe kama chapati usikande uchanganye tu.
4. Halafu utakata sampuli unayopenda mwenyewe.
5. Unaweka karai ya mafuta yakisha kupata moto unaanza kuchoma moto usiwe mkali sana, kiasi, baadae unaweza kuongeza moto na vikaange hadi viwe rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. .
6. Ukipenda gawa visheti sehemu mbili, na shira pia igawe sehemu mbili
7. Changanya nusu ya visheti kwa shira nyeupe.
8. Nusu ya shira nyingine ibandike tena motoni na tia cocoa vijiko viwili vidogo vya chai. Inapochanganyika cocoa vizuri changanya nusu ya visheti ulivyogawa kupata visheti vya shira ya cocoa.
Shira:
Sukari 2 Vikombe vya chai
Maji 1 Kikombe cha chai
Vanilla ½ Kijiko cha chai
(cocoa ukipenda kugawa visheti aina mbili) 2 Vijiko vya chai.
Updated at: 2024-05-25 10:23:12 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viambaupishi
Mchele wa basmati - 3 vikombe
Kuku - ½
Bilingani - 2 ya kiasi
Viazi - 4
Vitunguu - 2
Kitunguu (thomu/galic) iliyosagwa - 2 vijiko vya supu
Pilipili mbichi iliyosagwa - 2
Chumvi - kiasi
Garama masala (mchanganyiko wa bizari) - 1 kijiko cha chai
Hiliki ya unga - ¼ kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia wali - ¼ kikombe
Mafuta ya kukaangia viazi na bilingani - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
Osha mchele na roweka kwa muda kutegemea na aina ya mchele. Kata kuku vipande upendavyo safisha Kisha mchemshe kwa chumvi, pilipili iliyosagwa, thomu, na bizari mchanganyiko (garama masala). Akiwiva kuku, mtoe weka kando, bakisha supu katika sufuria. Menya na kata viazi kaanga weka kando. Kata kata bilingani slesi nene kaanga, chuja mafuta weka kando. Katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangu ya hudhurungi. Tia vipande vya kuku, ukaange kidogo. Tia supu ya kuku, mchele, tia hiliki, ufunike hadi karibu na kuwiva kabisa. Tia viazi na bilingani uchanganye kidogo, kisha tia katika oven imalizike kupikika pilau humo au unaweza kuendelea kufunika juu ya jiko hadi pilau iwive. Pakua katika sahani ikiwa tayari kuliwa kwa saladi ya mtindi.