Kama umeajiriwa au pia umejiajiri ni mojawapo ya njia zinazokuingizia kipato maana wengi wanaanzia hapo mpaka kuja kufikia kule wanakohitaji.
Ila kuna maswali machache ya kukupa changamoto ambayo nataka ujiulize:-
Kwako muajiriwa
ππΏUmeshawahi kujiuliza huo mshahara unaolipwa unakutosha kukutimizia Yale yote unayohitaji maishani mwako??
ππΏUmeshawahi kujiuliza ukifukuzwa au ukipunguzwa kazini utafanya nini?
ππΏUmeshawahi kujiuliza ofisi au kampuni unayofanyia ikifilisika wewe utafanya nini?
ππΏUmeshawahi kujiuliza kwa nini unataka kuhama au kuacha kazi hapo unapofanyia uende ofisi nyingine??
ππΏUmeshawahi kujiuliza kwanini hupapendi hapo unapoishi lakini bado unaendelea kuishi hapo?
ππΏUmeshawahi kujiuliza kwa nini huo usafiri unaoutumia huupendi lakini kila siku unautumia huo huo??
ππΏUmeshawahi kujiuliza ni kwa nini wanao au watoto wako hawapendi shule wanayosoma lakini wewe uwezo wako ndipo ulipoishia??
ππΏUmeshawahi kujiuliza kwa nini hupendi mikopo lakini bado unaendelea tu kukopa??
ππΏUmeshawahi kujiuliza unaipenda kwa dhati tena kutoka moyoni kazi unayoifanya??
ππΏUmeshawahi kujiuliza kwa nini unaomba kila Mara kuongezewa mshahara kama sio kuandamana??
ππΏUmeshawahi kujiuliza kwa nini unatamani ukasome uongeze elimu??
ππΏUmeshawahi kujiuliza kwa nini mkubwa wako kazini hataki uache kazi au ukasome au uhamie ofisi nyingine??
ππΏUmeshawahi kujiuliza kwa nini kila siku uko “busy” kazini au ofisini mpaka unakosa muda wa kufurahia na ndugu,jamaa,na marafiki na familia na mifuko yako au akaunti yako benki haiko “busy”??
ππΏUmeshawahi kujiuliza kwa nini unataka kufungua kibiashara chako au unataka ufanye kilimo Fulani kwa sababu umesikia kinawatoa watu???
ππΏUmeshawahi kujiuliza usipokwenda kazini kwa muda Wa wiki au mwezi au mwaka je kipato hicho hicho unachokipata utaendelea kukipata??
Hebu jiulize hayo maswali na mengine mengi yanayofanania na haya ujaribu kuona kama majibu yake unayo na kama majibu yapo ni njia gani unatumia au unategemea kutumia ili kuondokana na hayo??
Kwako wewe uliyejiajiri
ππΏUmeshawahi kujiuliza kwa nini biashara yako haikui kwa muda wote huo uko pale pale??
ππΏUmeshawahi kujiuliza kwa nini unataka uachane na hiyo biashara ufanye nyingine??
ππΏUmeshawahi kujiuliza kwa nini kila kitu unafanya wewe mwenyewe haumruhusu msaidizi kuwepo??
ππΏKwa nini huthubutu kumuachia mtu biashara yako kwa muda tu ukiondoka unafunga??
ππΏKwa nini unawaumiza wengine au wengine wanaumia ndipo wewe utengeneze faida yako??
ππΏKwa nini huwezi kuwasaidia wengine waweze kutengeneza kipato kama chako??
ππΏKwa nini akija mwenzako pembeni yako kufungua biashara kama yako unachukia???
ππΏKwa nini unachukia kulipa kodi ya pango lakini inakubidi tu ufanye hivyo??
ππΏNi watu wangapi wanaichukia au kuipenda biashara yako??
ππΏWangapi wanakuongea vizuri au vibaya kutokana na Huduma yako unayotoa??
ππΏKwa nini unatamani usiwe unalipa kodi??
ππΏKwa nini hupendi kuwaonyesha wengine njia unazotumia katika kuijenga biashara yako??ikiwa ni pamoja na upatikanaji Wa mizigo,unavyouza na unavyopata Wateja??kwa nini?
ππΏKwa nini hupendi kuona aliyeanza nyuma yako akifanikiwa kabla yako??
Hayo ni baadhi ya maswali ya kujiuliza wewe kama mjasiriamali au uliyejiajiri ingawa yapo na mengine unaweza kujiuliza tu uone kama utapata majibu yake na yawe ya kueleweka
References:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE