Vituko Vya Wikiendi
Kifahamu Kidada kimbea kilichofukuzwa kazi
Unafahamu?
Kile kidada kimbea kinachosemaga salio lako halitoshi kimefukuzwa kazi saivi kupiga simu ni bure mjulishe na mwenzako
📲 📲
Angalia kilichonikuta nilipoenda kwa mganga
Usije ukaenda kwa mganga, mwenzako yamenikuta, yani masharti niliyopewa, acha tu,
yalikua hivi:-
1.Jasho la nyoka.
2.Manyoya ya mende.
3.Sisimizi Shoga.
4.Mbwa mjane.
5.Kuku aliye single.
6.Samaki mwenye miaka miwili bila kuoga
7.Mti wenye ujauzito.
8.Mbavu za Nzi.
9.Nywele za Kiroboto.
10.Mwanya wa Mbu.
Duuh..!! mwanangu kwa hali hii mbona itakula kwako.
Wengine wanasemaga
IGA UFE! Rizik anagawa Mungu tu shetan simuelew!
Tofauti kati ya Binti wa Kizungu na Binti wa Kibongo mwanamme anapotoka kuoga
Tofauti ya Binti wa Kizungu na Binti wa Kibongo pale ambapo Mwanaume wake atokapo kuoga.
Binti wa Kizungu: Baby you look nice and fresh.
Binti wa Kibongo: Naona safari imeiva, Mwanaume hupumziki kama nesi wa zamu
😆😆😆😆
Huyu mchaga kazidi sasa, angalia anavyomfanya huyu mbuzi
Mchaga alinunua mbuzi akamwambia mpishi Nyama nusu ipike pilau na ingine itie kwenye friza. Kichwa fanya supu, miguu fanya mchuzi chukuchuku. Ngozi usitupe tutafanya mswala, utumbo pikia ndizi na mifupa tutawauzia wenye mbwa. Kinyesi kihifadhi kwa mbolea ya bustani.
Mpishi akamuuliza Hutaki na sauti ya mbuzi tufanye ring tone kwenye simu yako? Mchaga akajibu Yesuu! hivi inawezekana? bac fanya hivyo tuwauzie na wengine hiyo ringtone. Chezeya mchaga!
Jee wajua! Maajabu ya whatsapp..
JE WAJUA?
Je wajua kwamba kuku wa kwenye Whatsapp anamzidi tembo ukubwa? 🐓👉🏽🐘.
😂😂😂Maajabu!
Hyuyu daktari ni noma, cheki anachokisema
Kuna Daktari wa Moyo alifariki wakamchongeaa jeneza lenye umbo la Moyo. Ghafla Daktari mwingine akaanza kucheka, watu wakamuuliza “kwanini unacheka unafurahia mwenzako kufariki?” Daktari yule akajibu “hapana mimi ni Daktari wa kutahiri nafikilia nikifa mtanichongea jeneza lenye umbo la ….”
Google, Facebook, WhatsApp, Internet na Umeme nani zaidi?
Google alisema : mimi nina kila kitu
Facebook ikasema : mimi najua watu wote
Whatsapp akasema : mimi napendwa zaidi kuliko nyinyi
Internet akasema : hahahaha nyinyi nyote bila mimi si kitu !
umeme ukatamka : mutabadilisha topic au niwaonyeshe😂😂😂😂😂
Alichofanya mke baada ya mme wake kupenda kumchunga sana
Alifanya hivi;
Siku ya kwanza
MUME: Halooo vipi mke wangu salama weye?.
MKE: Salama tu
MUME: Uko wapi?
MKE: Jamani si niko nyumbani
MUME: Mhh kama kweli uko nyumbani washa blender nisikie…..mke akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Okay haya mi natoka kazini naja
Siku ya pili
MUME: Vipi mko salama huko?
MKE: Tupo kama ulivyotuacha
MUME: kwani uko wapi?
MKE: Niko nyumbani napika
MUME: Washa brender kama kweli uko nyumbani
Mke akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Poa ntarudi baada ya masaa mawili
Siku sita baadae mume akaamua kurudi bila kumtaarifu mkewe alipofika home kamkuta mdada wa kazi yuko peke yake.
MUME: We mama yako yuko wapi?
MDADA: Sijui ameondoka na blender toka asubuhi
Watoto wa siku hizi ni shida! Angalia huyu mtoto anachomwambia baba yake
Ka ni wewe?
DOGO: baba mi siendi tena shule inaonekana walimu hawana uhakika na majibu yao.
BABA: Kwanini unasema hivyo?
DOGO: juzi walisema 3+4= 7, jana wakasema 1+6=7, halafu leo wanasema 5+2=7 sasa huoni kama wanatuchanganya.
ungekua wewe ungemjibu nini
Cheka na methali
1.Simba mwendapole =Huyo ni Sharobaro
2.Asiyefunzwa na Mamae= Ujue Mama hajapitia Ualimu
3.Zimwi likujualo= Lilikuona Sehemu.
4.Chelewa Chelewa= Ukizikusanya utapata Ufagio.
5.Hakuna Masika= Wakati wa Kiangazi.
6.Mpanda Ngazi= Asiwe Mwoga kuanguka
7.Dua la kuku=
Bismilah rahman rahim
11.Penye wengi= Pana Ajali au Tukio
12.Ukiona vyaelea= Ujue ni vyepesi.
13.Mwenye nguvu= amekula ugal wa dona(…..)
Faida 3 za uvutaji wa sigara
Ni hizi
1. Mvuta sigara hazeeki
2. Mvuta sigara haumwi na mbwa
3. Mvuta sigara nyumbani kwake haingii mwizi
UFAFANUZI
1. Hazeeki kwa sababu hufa mapema kwa kifua kikuu
2. Haumwi na mbwa kwa vile kifua na mapafu yanapooza na hulazimika kutembea na bakora
3. Nyumbani kwake haingii mwizi kwa kuwa inafika wakati ambapo halali:
atakohoa usiku kucha hivyo mwizi anajua yupo macho
kumbe kikohozi tu!
Wadada acheni hizo
Mfalme Sulemani alikuwa na wake 700 na alichepuka(cheated)na vimada 300 . Mpenzi wako/Mume wako unamfumania na kimada mmoja tu ugomvi na amani imapotea ndani ya nyumba,unasimulia kuanzia padri,mchungaji,ukoo wako mzima,mashoga, stress,vidonda vya tumbo,inapelekea mpaka unaokoka,eti kisa kamuonjesha mmoja☝ sasa akionjesha 700 si utakutwa Mirembe�
Wadada acheni HIZO
😂😂😂😂😂😂.
Duh, Ukisikia ngoma droo ndio hii
Ni noma!
Baada ya Talaka mke kamtumia mume meseji:- “Nasikitika kukujulisha kuwa binti uliyemlea kwa miaka 20 sio mtoto wako” Mume akamjibu:- “Duh! Nashukuru Mungu kwani nilikuwa nikiumia rohoni kila siku kwamba nazini na binti yangu” 😂😂😂😂😂😂😂😂😂 🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃
Ulishawahi kupenda kwa namna hii??!!
Ushawai kumpenda dem na kumfia mazima kiasi kwmb anakwambia ye ana msela lkn we huelewi..unamkazia!!
Inabidi dem asisitize,”I HAVE ONLY ONE HEART,PLZ, I CANT LOVE TWO MEN”
Nawewe unaona haiwezekan,unamwambia ‘NIPENDE ATA NA KIDNEY’😃😃😙😃😃😃😗😃
Maisha ya Pwani ni Shidaaaaah
😆😆 😂😂😂😂😂😂 Jamaa kagombana na mkewe, akasusa kula🍽🍨 kurudi kazini kamkuta mkewe amevaa kanga imeandikwa ukisusa wenzio wala ilipofika asubuhi mke akavaa kanga imeandikwa ukitoka 🚶🚶mwenzio anaingia💃💃
jamaa akagoma kwenda kazini 😬😬 mke akabadili kanga na kuvaa iloandikwa nimemdhibiti ndo mana hatoki🚷 jamaa akaenda kuomba ushauri kwa rafiki yake akaambiwa twende nyumbsni kwako, walipofika walimkuta mke kavaa kanga imeandikwa ulidhani rafiki yako kumbe adui yako🤔🤔 jamaa akaamua kusafiri siku tano ili kupunguza hasira. Aliporudi akamkuta mke amevaa kanga imeandikwa ni bora nimpe jirani kuliko kiozee ndani
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
hata kama hupendagi ujinga kwa maneno ya kwenye kanga utasanda tu
Cheki huyu dingi alivyo mnoko
Unamtumia baba ako meseji ukiwa shule “Baba naomba unitumie 100,000 ya pckt mny” anakuuliza “pckt mny” ndo nini? Unamjibu ni kifupi cha “pocket money” af ankutumia 10,000, unamuuliza hiyo hela ni ya nini? Anakwambia ni kifupi cha 100,000.
Hapo ndo unatamani kuchoma shule ufe.
Cheki hiki kibabu kulivyowaacha watu hoi wakati mchungaji anafungisha ndoa
Mchungaji Kauliza: Yeyote mwenye pingamizi la haki kwa ndoa hii asimame na aje mbele.
Mara kasimama kibabu na kwenda mbele, bibi harusi alipomuona tu yule babu akazimia.
Mchungaji akauliza: tueleze pingamizi lako
Kibabu kikajibu: Nimeamua kuja mbele kwasababu kule nyuma sisikii!!!.
kanisa zima hoi,
Angalia huyu jamaa alivyowafanyia watu uhuni bar
Jamaa kaingia Bar;
Jamaa: Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji, maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji. Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,
Jamaa: Muhudumu nipe supu na kila mtu humu ndani mpe supu maana ninapokunywa supu kila mtu lazima anywe supu. Watu wakapewa supu tena safari hii wakapiga makofi.
Jamaa: Muhudumu nipe bili, na kila mtu humu ndani mpe bili maana wakati nalipa bili yangu kila mtu lazima alipe yake. Zogo lilianzia hapo…….
MAMBO KUMI YA KUFURAHISHA NA HUWEZI KUYAFANYA
1. Huwezi kuosha Macho kwa Sabuni;
2. Huwezi kuhesabu Nywele zako;
3. Huwezi kupumua kwa Pua na huku umetoa Ulimi;
4. Unajaribu kufanya namba 3
6. Umeona inawezekana, sanasana unakuwa Kama Jibwa;
7. Unatabasamu kwa kuwa umejiona Mjinga!
8. Umeruka namba 5;
9. Unahakikisha Kama kweli 5 haipo.
10. Unacheka kwa kuwa nimekubamba!
Recent Comments