Vituko Vya Watu Wote
Misemo 10 bora ya kuchekesha itakayokuacha mdomo wazi
1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.
2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.
3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?
4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.
5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.
6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.
7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.
8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.
9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.
10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi
kufunika sufuria.
Angalia nilivyookoa maisha ya mtu leo
Nmeokoa maisha ya mtu asubuhi ya leo huwezi amini.Nmekutana na ombaomba nikamuuliza atajisikiaje nikimpa sh.30,000/-
Akasema ATAKUFA kwa furaha.Nikaondoka bila kumpa ili ASIFE.๐๐๐๐
Sasa Hawa wadada Wapo in Relationship Na Nan!!??
Asilimia 76% Ya Wasichana Kila Ukiwatongoza Wanakwambia Wapo In relationship SAWA ATUKATAIโฆ
Asilimia 98% Ya Mamen Wapo SINGLEโฆ HAPA NDIPO HESABU ZANGU ZINAFELI..
Sasa Hawa wadada Wapo in Relationship Na Nan!?.
Angalia kilichonikuta nilipoenda kwa mganga
Usije ukaenda kwa mganga, mwenzako yamenikuta, yani masharti niliyopewa, acha tu,
yalikua hivi:-
1.Jasho la nyoka.
2.Manyoya ya mende.
3.Sisimizi Shoga.
4.Mbwa mjane.
5.Kuku aliye single.
6.Samaki mwenye miaka miwili bila kuoga
7.Mti wenye ujauzito.
8.Mbavu za Nzi.
9.Nywele za Kiroboto.
10.Mwanya wa Mbu.
Duuh..!! mwanangu kwa hali hii mbona itakula kwako.
Wengine wanasemaga
IGA UFE! Rizik anagawa Mungu tu shetan simuelew!
Angalia huyu mwanamke mwenye wivu kwa mumewe alivyoumbuka, Mme wake kamuweza kweli
WIVU HUU NI NOMA
Mke: Hivi mume wangu una wanawake wangapi huko nje?
Mume: Kama nywele za kichwa changu.
Mke akachukua nguo zake akaondoka, Kufika njiani akakumbuka mumewe alikuwa na kipara Akaanza kurudi kwa mumewe.
Hii bahati mbaya hii haifai kusema Samahani
(KIFO NI NIN)
KIFO ni pale unapokosea text na kumtumia
BABA yako kipindi mnakula
“hello Mrembo”๐๐
Kama utazubutu kusema Samahani ๐
Acha usumbufuโฆ
UNAMNG’ANG’ANIZA MPENZI WAKO AKUWEKE KWNY PROFILE PICHA MLOPIGA PAMOJA
HIVI ULIDHANI MWL.NYERERE ALISHINDWA KUKAA NA MKEWE MARIA KWNY NOTI YA BUKU
๐๐๐๐๐๐๐
Acha Usumbufuโฆ..
Dongo kwako kama una degree moja Halafu unachagua kazi
Mtu una degree 1 unachagua kazi! Wakati thermometer ina degree 100, inafanya kazi kwenye kwapa.
๐๐๐๐๐
Ni Utani tuuuuu!
Kwa nini watu hawapendi hesabu!! Sababu hii hapa!
Sababu ni hii
AL-SHABAB
AL-QAEDA
Kwenye MATHEMATICS pia kuna kundi linaitwa
“AL-GEBRA”
๐๐๐๐
๐ถ๐ป๐ถ๐ป๐ถ๐ป๐ถ๐ป๐ถ๐ป๐ถ๐ป
Kumbe ndo maana wengine hawapendi hesabu coz kuna element za ugaidi
Tofauti ya mchaga na mhaya wakipata kazi
Mchaga hata apate kazi bank bado atasema yupoย kibaruani.
Acha sasa mhaya apate kazi katka mashine ya kusaga na kukoboa; utaskiaย i work as a crucial engineer in a monocotyledon finalizing company
๐๐๐
ย
Recent Comments