Vituko Vya Kukupa Mudi Mpya
Madhara ya kubeba nauli kamili tuu. Cheki kilichonipata
Kubeba nauli kamili nayo ni shida
Yani nimepanda daladala
Kondakta mmoja akaingia kwenye Gari amevaa suti za blue za daladala na miwani Kisha akakusanya pesa Gari Zima alafu akakaa siti ya nyuma baade Kondakta mwingine akaanza kukusanya pesa watu wakalalamika na kusema tayari tumelipa na kumuonyesha tuliemlipa Kondakta akacheka na kusema huyo tuliemlipa ni kipofu na alikuwa anaomba msaada..!!
Angalia huyu jamaa alivyowafanyia watu uhuni bar
Jamaa kaingia Bar;
Jamaa: Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji, maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji. Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,
Jamaa: Muhudumu nipe supu na kila mtu humu ndani mpe supu maana ninapokunywa supu kila mtu lazima anywe supu. Watu wakapewa supu tena safari hii wakapiga makofi.
Jamaa: Muhudumu nipe bili, na kila mtu humu ndani mpe bili maana wakati nalipa bili yangu kila mtu lazima alipe yake. Zogo lilianzia hapo…….
Huyu dogo nimsaidieje? Cheki alivyojichanganya
Nimekutana na dogo mmoja hivi hapa analia,namuliza analia nin??ananambia ”ALIPEWA MIA TANO ZIPO MBILI,MIA TANO MOJA YA NYANYA na MIA TANO NYINGINE YA VITUNGUU sasa KAKOSEA KAZICHANGANYA HAJUI TENA IPI NI YA NYANYA na IPI NI YA VITUNGUU!!!
.
.
NA PESA ZOTE ANAZO KAZISHIKA MKONONI,
Mume mgonjwa kazua mpya baada ya kuruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospitali alipokuwa kalazwa
John aliruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospital ya
Vichaa, akapakiwa ktk ambulance hadi karibu na
nyumbani kwake, akaulizwa kwako unapakumbuka?
akajibu ndio nyumba yangu ilee, mara wakatoka
watoto wawili wamevaa uniform akasema watoto
wangu walee wanakwenda shule..
Akatoka mwanamke akasema na mke wangu yulee,
Ghafla akatoka mwanaume john akasema mimi
yuleeeeeeee…. naenda kazini!! JE, NI KWELI
AMEPONA??
Huyu bibi kweli kiboko, cheki alichofanya akiwa na babu
Bibi na Babu walisafiri wakielekea kwa mtoto wao ambae hawajamuona zamani.
Walipofika njiani wakawa wamechoka Sanaa. Wakaamua kutafuta hotel ili walale.
Wakakubaliana walale kwa masaa 4. Wakalala, Walipoamka, mfanyakazi wa Hotel akawatoza Tsh. 500,000/=
Wale wazee wakashangaa hata kama ni hotel ya kisasa lakini sio laki tano kwa masaa 4.
Babu akagoma kulipa akasema aitiwe meneja.
Meneja akaja kuwasikiliza
Babu: ” Kwanini bili ni kubwa hata kama ni hotel ya kisasa?”
Manager;“kuna maswiming puli, ya kisasa “
Babu; “Lakini hatukuyatumia”
Manager; “Ah ah ah. Lakini mungeweza kama mngetaka”
Babu: “Hata hivo bado haithamini kuwa laki 5”
meneja: “Pia Kuna waimbaji kutoka sauzi, Uganda , Congo”
Babu: “Lakini sisi hatukuwasikiliza”
Meneja: “Ndiooo. Lakini mngeweza kama mngetaka”
Babu; aka give up na kumwambia mkewe andika cheki uwape,,
Bibi akaandika akampa meneja.
Meneja anaangalia anaona sh. 50,000
Akashangaa na kusema. “VP mbona hamsini'”
Bibi akajibu “450,000 ya kulala na mimi”
Meneja akajibu; “Lakini sijalala”
Bibi :“ungeweza kama ungetaka”
Cheki huyu dingi alivyo mnoko
Unamtumia baba ako meseji ukiwa shule “Baba naomba unitumie 100,000 ya pckt mny” anakuuliza “pckt mny” ndo nini? Unamjibu ni kifupi cha “pocket money” af ankutumia 10,000, unamuuliza hiyo hela ni ya nini? Anakwambia ni kifupi cha 100,000.
Hapo ndo unatamani kuchoma shule ufe.
Angalia huyu demu alivyo mbulula
Jamaa aliamua kumtoa demu wake out kwaajili ya chakula cha usiku kufika hotelini wakakaa mezani mhudumu akaja,
Mhudumu: kaka nikuhudumie nini,
Jamaa: afathal NILETEE MENU LISTI
Mhudumu: dada na wewe?
Demu akajibu kwa pozi tena kwakujishaua, “NA MIMI NILETEE MENU LIST ILA USIWEKE CHUMVI NYINGI”
Chezea mbulula wewe…!!!
Cheki hawa washikaji wanachokifanya baada ya kuvuta bangi, Bangi si mchezo
Kuna washikaji walikuwa wakivuta bangi… kiberiti kikawaishia… wakamtuma mwenzao akatafute kingine… bangi lilikuwa limemkolea… akazungukazunguka hatimaye akarudi palepale kijiweni…
MSHIKAJI: oyaaa wanangu eeeh… niazimeni kiberiti mwanangu mwenyewe …..
WENZAKE: baharia ee subiria kimtindo kuna mwana tumemtuma akatafute kiberiti.
Huyu jamaa ni shida, Chezea wimbo wa Taifa!
Mke mmoja alimpa mme wake redio aende nayo chooni ili asiboreke kwa vile huwa anakaa muda mrefu.
Basi alvyotoka akamuuliza,”ehe mme wangu ulienjoy?” Mme,”ah wajinga hawa!
Wameniwekea wimbo wa taifa,nimejisaidia huku nimesimama
Eti wanadamu walikuja vipi duniani
Mtoto wa miaka sita alimuuliza babake:
MTOTO: Baa, eti sisi wanadamu tulikuja vipi
duniani?
BABA: Mungu alimuumba Nabii Adam na Hawa.
Kisha wao wakaanza kuzaa watoto na watoto
wakazaa mpaka tukazaliwa sisi. (Mtoto hakuridhika
akamfuta mamake)
MTOTO: Mma, eti sisi wanadamu tulikuja vipi
duniani?
MAMA: Wanasayansi wamesema sisi tulitokana na
manyani baadae tukawa binadamu. (Mtoto akarudi
kwa baba)
MTOTO: Baa mbona mama ansema sisi tulikuwa
manyani mwanzo?Au wanidanganya?
BABA: Mwanangu, mimi nimekuelezea kuhusu ukoo
wetu. Mamako amekuelezea kuhusu ukoo wao😂😂🚶🏼🚶🏼🚶🏼




































































I’m so happy you’re here! 🥳









Recent Comments