Vituko Vya Kukupa Mood Mpya

Cheka kidogo, angalia anachosema huyu mchaga

Mchaga baada ya kufa akaulizwa na malaika anayetoa roho: Mangi hapa ni njiapanda kulia ni Mbinguni na kushoto ni Jehanamu, Je unachagua kwenda wapi?

MANGI: Bwashee, mi nabaki hapa hapa njiapanda aisee.
MALAIKA: Kwa nini?
MANGI: Aisee, nikifungua duka hapa si nitapata wateja wa Mbinguni na Jehanam. Yani patakuwa senta ya hatari, supu na nyama choma muda wote. Hata we utafaidi, unavyoenda kuchukua roho unaniletea stock nakupa hela yako cash mkononi. Na kila ukipita hapa unapiga mchemsho wako wa ulimi na bia mbili chap kabla ya kuingia mbinguni.
Kwanza nashangaa Shirima alipitaje hapa bila kushika ploti, au alikufa amelewa sana?

Faida 3 za uvutaji wa sigara

Ni hizi

1. Mvuta sigara hazeeki
2. Mvuta sigara haumwi na mbwa
3. Mvuta sigara nyumbani kwake haingii mwizi

UFAFANUZI

1. Hazeeki kwa sababu hufa mapema kwa kifua kikuu

2. Haumwi na mbwa kwa vile kifua na mapafu yanapooza na hulazimika kutembea na bakora

3. Nyumbani kwake haingii mwizi kwa kuwa inafika wakati ambapo halali:
atakohoa usiku kucha hivyo mwizi anajua yupo macho
kumbe kikohozi tu!

Huyu jamaa bonge la bwege, ungekua wewe ndiyo rafiki ake ungemwambiaje?

RAFIKI: Vipi mbona leo huna uchangamfu
JAMAA: Wanawake bwana, mwanamke hata umpendeje atakugeuka tu
RAFIKI: Nini tena ndugu yangu? Mbona shemeji mtu fresh sana
JAMAA: Hata mimi nilikuwa najua hivyo, leo nimegundua kumbe ana siri kubwa sana
ananificha, mi naita huu ni usaliti wa ndoa.
RAFIKI: Nini tena?

JAMAA:Nimegundua mke wangu kumbe anafanya biashara ya kitimoto na hajawahi hata kuniambia
RAFIKI: Kitimoto? We umejuaje?
JAMAA: Leo asubuhi nilichelewa kuamka niliamua nijipumzishe kidogo kabla ya kwenda kazini, simu ya mke wangu ikalia, nikaamua kuipokea, kabla hata sijafungua mdomo, nikasikia sauti ya mwanaume mmoja akauliza, “Huyo nguruwe umeshamuondoa?’ Hebu we fikiria nilivyoshtuka, yaani mpaka sasa nashindwa kuamini kuwa mke wangu ananizunguka anafanya biashara ya nguruwe hajaniambia hata siku moja

Kilichotokea kati ya mkaka na mdada walipokutana hotelini

Mkaka aliingia kwenye hoteli moja akaketi meza moja na mdada mrembo maarufu sana;
MKAKA: Samahani dada sijui saa ngapi?
MDADA: Nani kakwambia saa yangu ndio ya kuangalia kila mtu?

MKAKA: Samahani sana….jamaa akachukua Galaxy yake akapiga simu….aise saa ngapi saa hizi? mi ndio nimeingia toka USA nataka kurekibisha saa yangu ifwate muda wa huku. Na wewe uwahi kuchukua iPad nimekuja nazo tatu tu za zawadi. Halafu ntafutie mtoto mzuri nimumwagie midola niliyokuja nayo, ok ciao tuonane badae.
MDADA: Kaka samahani saa hizi ni saa…..
MKAKA: Achana na mimi wewe

Ha ha ha ha haaaaa!!

Angalia wanachokifanya Zuzu na msichana chumbani kwenye giza

Zuzu: Mambo Anna!
Anna: Poa!
Zuzu: Kuna kitu nataka nikuonyeshe…
Anna: Kitu gan?
Zuzu: Twende chumbani kwako (wakaenda)
Anna: Haya nionyeshe…

Zuzu: Funga mlango na madirisha kwanza (akafunga)
Anna: Haya nionyeshe sasa!..
Zuzu: Zima taa kwanza (akazima)
Anna: Mhm…nionyeshe sasa!
Zuzu: Haya njoo hapa kitandani…
Anna: Ok, nionyeshe!
Zuzu: Ona nimenunua saa ambayo inawaka yenyewe gizani… Acha mawazo mabaya ww???

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About