Nilichokifanya baada ya kualikwa na mchumba wangu kwao
Mchumba wangu amenialika kwao nikawaone wazazi wake lakini akaniambia nisiende mikono mitupuβ¦
Nikaamua kuvaa glovesβ¦
Sipendagi aibu ndogo ndogo ukweni.πππ
Mchumba wangu amenialika kwao nikawaone wazazi wake lakini akaniambia nisiende mikono mitupuβ¦
Nikaamua kuvaa glovesβ¦
Sipendagi aibu ndogo ndogo ukweni.πππ
ππππππ
Mwenzenu nilikatiwa umeme jana basi leo si nikaamua kwenda kununua luku ya 10,000. Kufika njiani nikatamani fursana nikaingia kijisupermarket mara sindo nakutana na ex wangu! Mshenzi yule kaniona mimi sijui alikua na mpango wa kununua vocha ya jero eti kabadili kanunua vocha ya buku tano ilimradi nione maisha yake safi tangu tuachane. Mambo ya kijinga spendi kudadeky nimetoa buku kumi nikanunua mipampers nami nijifanye nimeowa nina mtoto halafu huyoo nikashika njia yangu.
Sasa washkaji zangu tafadhalini mwenye mtoto au shida ya pampers naomba anunue kwangu maana leo nalala tena kiza πββ
MASSAWE alienda na marafiki zake bar kunywa, baada ya kumaliza kutumia akaletewa bili kama ifuatavyo:
Manka 35,000
Marieta 20,000
Kekuu 30,000
Kitime 15,000
Kinabo 10,000
TOTAL 110,000/=
MASSAWE akaicheki akasema “Wote nitawalipia lakini huyo “TOTAL” Yesuu simlipii.
Kwansa anamiliki sheli kibao sa mafuta hapa bongo. Shensi taip ! Na amekunywa nyingi kuliko wote alipe mwenyeweβ¦
Nimekuja kwa Rafiki angu kumtembelea kaacha maji jikon yeye kaenda kununua unga. Huku mm nikaongeza maji pale jikon. Kumbe yy aliweka maji saiz ya unga wake peke ykeβ¦ Sasa hiv TUNAKUNYWA UJI hata hatuongeleshani. Kimbelembele changu kimeniponza.. ππππ
Hakuna m2 mwenye ndugu wengi kama konda wa daladala.
Utasikia,
“HAYA, DADA HAPO MBELE, MJOMBA KULE MWISHO.
MA-MDOGO UNAENDA?,
NGOJA ASHUKE BIBI.
HAYA SHEMEJI UMEIKUTA YA KUWAH.
Babu njoo ukae!
Baba angu hapo tusogee kidogo,
Shangazi maliza ngazi,
Swaiba geukia mbele,
Kaka hapo shika upande wa pili,
Mdogo wangu mpishe Ma Mkwe akae.
Subiri Shemeji yako apandeβ¦
Duhβ¦ makonda nomaβ¦!!
CHEKA KIDOGO
Majambaz waliliteka gar moja lililokua limeshehen abiria
Baada ya abiria kusachiwa na majambaz hao na kukutwa hawana pesa, majambaz wakasema kila m2 atapigwa viboko (bakora) kutokana na namba ya shati alilovaa
Aliyekua hana namba atasalimika
Kaz ikaanza, jamaa alievaa jez ya ROONEY wa Man U akapigwa fimbo 10, mwengine alievaa nguo ya 50cent akapigwa 50, n.k, sasa kwa pemben kulikua na jamaa analia sn yaani kila akijiangalia, kumbe alikua amevaa fulana limeandikwa LOWASA 2015 duuuh! Unajua kilichotokea ngoja niweke cm chaji kwanza.
ππ ππππππ Jamaa kagombana na mkewe, akasusa kulaπ½π¨ kurudi kazini kamkuta mkewe amevaa kanga imeandikwaΒ ukisusa wenzio walaΒ ilipofika asubuhi mke akavaa kanga imeandikwaΒ ukitoka πΆπΆmwenzio anaingiaππ
jamaa akagoma kwenda kazini π¬π¬ mke akabadili kanga na kuvaa iloandikwaΒ nimemdhibiti ndo mana hatokiπ· jamaa akaenda kuomba ushauri kwa rafiki yake akaambiwa twende nyumbsni kwako, walipofika walimkuta mke kavaa kanga imeandikwaΒ ulidhani rafiki yako kumbe adui yakoπ€π€ jamaa akaamua kusafiri siku tano ili kupunguza hasira. Aliporudi akamkuta mke amevaa kanga imeandikwaΒ ni bora nimpe jirani kuliko kiozee ndani
ππππππππππ
hata kama hupendagi ujinga kwa maneno ya kwenye kanga utasanda tu
Jamaa kaingia mgahawani kwa fujo
JAMAA :Β Nipe soda moja na kila mtu mpe yake maana ninapokunywa soda napenda kila mtu anywe
WATU :Β Ha! Ha! Ha! Haaaa!
JAMAA :Β Nipe mchemsho na kila mtu mpe wa kwake maana ninapokula mchemsho napenda kila mtu ale wake
WATU:Β Watu weweeee! Tena safari hii Na makofi juu..
JAMAA :Β Mhudumu, nipe bili na kila mtu mpe yake maana ninapolipa bili napenda kuona kila mtu analipa yake
πππππππ
WIVU HUU NI NOMA
Mke: Hivi mume wangu una wanawake wangapi huko nje?
Mume: Kama nywele za kichwa changu.
Mke akachukua nguo zake akaondoka, Kufika njiani akakumbuka mumewe alikuwa na kipara Akaanza kurudi kwa mumewe.
Pale unapozamia kwenye Dinner Party ya Jumuiya Fulani, sasa Lengo la Jumuiya hiyo ni kupata Fedha za kutunisha Mfuko wa Jumuiyaβ¦sasa unakakaa mbele kabisa ili Muda wa Msosi usichelewe na kukuta kwenye Buffee yamebaki maharage!
MC : “Papai zuri kabisa kutoka Newala, Papai Mwendokasi, hili ni Shilingi laki 1..jamani Papai,nipeni ofa!”
MOSHA : “Laki 3 hapaaa!”
“Jamani laki 3 pale kwa Mosha, Papai linaondoka jamani, papai hili ni self contained kabisaβ¦.papai jamani”
KIBOLIBO: “Milioni 1 hapaaa”
“Jamani Mambo yanazidi kunoga hapa!β¦Benedict Kibolibo anataka papai kwa milioni 1 jamani, linaondoka papai!”
RWEYEMAMU : “nitanunua Papai hilo kwa Milioni 5”
Haya sasa jamani Rweyemamu ametoa ofa ya Milioni 5 Jamani, nani mweingineee?”
Kimyaaaβ¦
Haya jamani Papai kama hakuna Ofa basi Papai linakwenda kwa Rweyemamu!β¦β¦..haya sasa Kuna Kuku hapa Jogoo kabisa, bei yake ni laki 6 jamani Jogoo twitter huyu!”
WEWE “Milioni Mojaaa!”( hapa umejiwahi wa kwanza na wewe uonekane upo huku ukijua kabisa Wakina Mosha na Rweyemamu lazima watampandia Dau Jogoo, tena dau kubwa”
MC: ee sasa Kumekucha Jamani, Kabasele anamtaka Jogoo kwa Milioni 1 jamani!β¦.ofa nyingineeee!”
Kimyaaaβ¦
Jamani Jogoo anakwenda kwa Kabasele jamani!β¦ofa nyinginee!
Kimyaaaβ¦.
Kimyaaaβ¦.
πππβ¦hapa sasa ndio mfukoni kuna Buku jero,..huko kwengineko NMB nill balanceβ¦sasa unageuza mimacho kumtazama Mosha kama atapanda dau kwa jogooπ(mama wee Mosha anachezea Simu!)β¦..unamtazama Rweyemamu (teh anatafuna Kuku)β¦..mama weeeπ
MC: Haya jamani kama hakuna Mwingine basi zoezi letu liishie hapa na limekwenda kwa Mafanikio, Mpatieni Kabasele Jogoo wake!
Hapa sasa unapokea jogoo wako wa MILIONI kwa Tabasamu la Maitiβ¦.kule nyumbani Jogoo wako Mkubwa unauza elfu 20 lakini sasa haka kajogoo kapya Mkononi kanakuwa kazito utadhani umembeba John Cenaπβ¦Mama weee hapa sasa vidari ulivyotafuna unaviona kama vimerudi kwenye Ulimiβ¦.Chicken wings zinataka kutokea Masikioniβ¦..Uuuuwiiiii,πππ
Na hapa sasa kabla Dinner haijaisha ndipo unapojikuta Umebuni Cocktail ya Sparetta na Tomatoπππππ.
chiel wie okee
Leo kuna mdogo wangu nimemtumia meseji nimemuomba aniazime chaja yake ya simu. AkanijibuΒ 21002Β Nikawa mkali nikamuambia kuchajia mara moja tu ndio HELA yote hio si bora nikanunue Chaja yangu mpya. Akaniambia nimesema TUMIA TU ππmtatuua na lugha zenuπ
Mfugaji mmoja alikwenda kwa mfugaji mwenzake (ambae pia ni bwana mifugo wa eneo lao) asubuhi moja. Alipobisha hodi mtoto wa kiume wa umri upatao miaka 12 akamfungulia mlango. Mazungumzo yafuatayo yakafuatia:
Mkulima: Baba yako yupo?
Mtoto: Hapana Mzee, amekwenda mjini.
Mkulima: Mama yako?
Mtoto: Nae kaenda mjini na baba.
Mkulima: Kaka yako Howard yupo?
Mtoto: Nae hayupo, wote yeye, baba na mama wamekwenda mjini. Kwani una shida gani? Kama kuna kitu unahitaji niambie maana nimeachiwa funguo na najua vifaa vinapowekwa.
Mzee akawaza kidogo halafu akasema: Kwa kweli nilitaka kuongea na baba, mama au kaka yako kwa kuwa kaka yako amempa mimba binti yangu.
Mtoto akafikiria kidogo halafu akasema: Kusema ukweli itabidi umsubirie baba, ila kwa kukusaidia ni kuwa baba hulipisha shilingi laki moja kwa kupandisha dume la ng’ombe na elfu hamsini kwa beberu. Ila sijui baba hutoza shilingi ngapi kwa Howard akifanikiwa kutia mimba.
Alipelekwa Hospitali na baba yake, baada ya vipimo Doctor akawa anamuandikia dawa, baba yake akatoka nje kuongea na cm.
Mtoto akamwinamia Doctor na kusema kwa sauti ya chini:- “Doctor Kwenye dozi ya dawa niandikie na FANTA BARIDII, CHIPS na MISHIKAKI kutwa mara 2 kwa siku 30.
01.π Wale wanafunzi walioongoza
Mashuleni, wanaenda kwenye
Engineering na Medical school.
02.π Wale waliokuwa wa pili, wanachukua MBA na LLB na kuja kuwa Mameneja wa
wanafunzi walioshika nafasi ya kwanza.
03.π Wale waliokuwa wa tatu, wanageukia
Siasa na kuwaongoza wote hapo juu.
Yaani wa kwanza na wa pili.
04.π Wale waliofeli, wanaenda Jeshi, hawa wakigoma, basi hao wa juu
wote hawana raha.
05.π Wale waliopata Zero na waliokataa
shule wanakuwa waganga wa kienyeji,
wote hapo juu watamtafuta huyu, pale
mambo yao yanapokwenda kombo. Tuache kudharauliana, kila mtu ni boss akiwa kwenye nafasi yake.
ππππππππππΏππΏπππππ
Wanaume wana upendo kwa kweli.
Mwanaume hata akipewa kundi la wanawake 90 achague mmoja!! Hata akichagua mzuri kupita wote bado roho itamuuma kuwaacha wale 89 waliobaki!!*
Kwa namna hii wanaume wana Upendo Sana
ππππππ
Recent Comments