Vituko Vya Kukuondoa Mawazo

Angalia wadada walivyoumbuka kwenye hii test

Ticha katangaza test , Akatoa Masharti; Ukiandika jibu hamna kufuta au kukata.

Swali la kwanza,
Taja vyakula vi3 ambavyo ukienda hotelini umelipiwa utapenda kula (marks 1)

WAVULANA wakajaza; wali, ugali, mihogo.
WADADA wakajaza; burger, pizza, egg chop. Swali la

2: Eleza jinsi ya kupika kila chakula ulichotaja hapo juu. (marks 99)
wacha wadada waanze kuhangaika kukata majibu ya mwanzo!

Angalia huyu jamaa alivyowafanyia watu uhuni bar

Jamaa kaingia Bar;
Jamaa: Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji, maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji. Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,

Jamaa: Muhudumu nipe supu na kila mtu humu ndani mpe supu maana ninapokunywa supu kila mtu lazima anywe supu. Watu wakapewa supu tena safari hii wakapiga makofi.
Jamaa: Muhudumu nipe bili, na kila mtu humu ndani mpe bili maana wakati nalipa bili yangu kila mtu lazima alipe yake. Zogo lilianzia hapo…….

Ulevi noma! Angalia huyu mlevi alichomfanyia huyu jamaa usiku! Ungekua wewe ungefanyaje?

Jamaa alikuwa amelaa na mkewe saa tisa ya usiku akastuka baada ya kusikia mtu anabisha hodi kwenda kufungua mlango
Akamkuta jamaa kalewa sana mlangoni kwao
JAMAA: Nini tena mheshimiwa kuamshana saa hizi?
MLEVI: Naomba uje unisukume.
Jamaa akiamini kuwa pengine kuna gari la huyu mlevi limezima jirani akamwambia subiri nikavae viatu. Baada ya kuvaa viatu akatoka na wakaanza kusindikizana na mlevi. Mlevi akaongoza njia
mpaka kwenye mabembea ya jirani akakaa kwenye bembea moja na kumgeukia jamaa na kumwambia.. Okay nisukume basi.

Haya ndiyo madhara ya kulala kanisani

Tukiwa kanisani mdada alikuwa amelala , akaamka akasikia Pastor anasema
” SIMAMA”
Yule dada akasimama akashangaaa kanisa zima linamtizima kwa mshangao akiwemo mumewe, akaangalia kanisa zima akashtuka kujiona yeye peke yake ndiye aliesimama
Pastor akaendelea vizur endelea kusimama, tumepata mmoja hadi sasa aliyesimama narudia kwa mara ya mwisho kama hujasikia vizuri
” kama wew umewahi kumsaliti au bado unasaliti ndoa yako SIMAMA”
Binti akazimia

Mabinti wengine kwa kupenda hela! cheki huyu anachokifanya

Phone call
gal: hellow
Boy: sweety mambo vipi?
Girl: poa
Boy: utakuwa free weekend? nilikuwa nataka uje nyumbani
Girl: oh sorry ctoweza kuja sababu kuna haruc ya aunt yangu
Boy: kama ni hivyo sawa nilikuwa nataka nikufanyie sapraiz nimekununulia BLACKBERRY.
Girl: oh ucjal ntakuja na hata ntalala huko huko
Boy: na haruc je?
Girl: nilikuwa nakutania
Boy: hata mi nilikuwa nakutania

Cheki masifa yalivyomponza huyu, Sifa nyingine ni mbaya jamani

Mbongo, Mganda, na Mkenya walikamatwa na makosa Uchina.

Wakaambiwa adhabu ni ama kifo cha moja kwa moja au adhabu nyingine ambayo atakayeifaulu atakuwa huru, atakayeshindwa atauawa.

Basi wao wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu bahati yao.

Wakapelekwa msituni wakaambiwa kila mmoja aende kwa njia yake halafu arudi na matunda kumi ya kufanana.

Wakaingia msituni kila mtu njia yake.

… Mganda akarudi wa kwanza na machungwa kumi. Akaambiwa adhabu yake ni kumeza moja moja likiwa zima bila kufumba macho bila kulia wala kucheka wala kujitikisa mpaka yote kumi yaishe. Akameza la kwanza. Safi. Kumeza la pili, akashindwa kuvumilia akafumba macho. Akapigiwa risasi akafa.

Mkenya akaja. Ana vitunda vidogo vidogo kama pili vilaini. Akasomewa masharti. Akaanza kumeza bila kufumba macho wala kulia, wala nini… alipofika cha tisa akashindwa kuvumilia akaangua kicheko! Akapigwa risasi pia akafa.

Wakiwa kuzimu Mganda akamwuliza Mkenya, “Vipi, mbona ulishindwa kuvumilia wakati kilibaki kitunda kimoja tu?”

Mkenya akamjibu: “Mkuu, nilishindwa kuzuia kicheko maana nilimwona Mbongo anakuja na matikiti maji!”

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About