Vituko Vya Kukuburudisha
Majibu ya mkato ya kuchekesha Kutoka Kenya
Njeri:ย Roysambu ni ngapi?
Makanga:ย Roysambu ni moja tu. Pengine kama Chinese wamejenga ingine.
Odhis:ย Hii gari haina watu bana.
Makanga:ย Kwani hao wawili wenye wamekaa hapo ndani ni ngโombe?
Man:ย Wekeni nyimbo za Yesu tafadhali.
Makanga:ย Yesu bado hajatoa album. Akitoa tutaeka.
Mwikali:ย Excuse me condaโฆgari za Mwingi zinapandiwa wapi?
Makanga:ย Ziliacha kupandwa juu hazimei.
Man:ย Kwani mwisho wa gari ni wapi?
Makanga:ย Mwisho ni hapo penye number plate iko.
Karis:ย Ruaka ni how much?
Makanga:ย Sijaskia Ruaka ikiuzwa. But nikiskia nitakwambia.
Passenger:ย Shukisha dere.
Makanga:ย Tukishukisha dere utaendesha gari?
Johnny:ย Maze, hii gari iko na joto sana.
Makanga:ย Basi shuka upande fridge
Dogo alivyomchomea dada wa kazi kwa mama yake kuhusu baba
Dogo: mama hivi malaika si wanapaa?
Mama: ndiyo wanapaa, kwanini umeniuliza hivyo?
Dogo: nimesikia baba jana anamuita dada (housegir) malaika wangu, kwa hiyo nae atapaa?
Mama: ndiyo atapaa kuelekea kijijini kwao kesho, pumbavu zake.
Huyu traffic noma, kweli ulevi mbaya
Trafik mlevi alisimamisha gari Mama akapaki pembeni akaona trafik anakuja akiwa anayumba! Alipofika akasema, “naomba leseni yako.”
Mama akasachi mkoba Wake akatoa kioo kidogo cha kujtazama akampatia! Trafik akakiangalia kwa dakika 2
Akasema sasa si ungesema kama wewe ni trafik mwenzangu!
Haya nenda
Ulevi sio mzuri
๐๐๐๐
Huyu jamaa kawaweza wapenda vya bure
Jamaa kaingia mgahawani kwa fujo
JAMAA :ย Nipe soda moja na kila mtu mpe yake maana ninapokunywa soda napenda kila mtu anywe
WATU :ย Ha! Ha! Ha! Haaaa!
JAMAA :ย Nipe mchemsho na kila mtu mpe wa kwake maana ninapokula mchemsho napenda kila mtu ale wake
WATU:ย Watu weweeee! Tena safari hii Na makofi juu..
JAMAA :ย Mhudumu, nipe bili na kila mtu mpe yake maana ninapolipa bili napenda kuona kila mtu analipa yake
๐๐๐๐๐๐๐
Madhara ya kwenda baa na mke ndo kama haya
Jamaa alienda Bar na mke wake wa ndoa wakakaa kwenye viti, wakati wanasubiri vinywaji akapita binti mmoja anayejiuza akamsogelea yule mke wa jamaa
akamnong’oneza:- “AKULIPE KABISA KABLA HUJALALA NAYE, NI MGUMU KULIPA HUYOO!!.
HALAFU HUWA HATUMII KONDOMUโฆ”
Unajua ni nini kilitokea?
Angalia huyu demu alivyo mbulula
Jamaa aliamua kumtoa demu wake out kwaajili ya chakula cha usiku kufika hotelini wakakaa mezani mhudumu akaja,
Mhudumu: kaka nikuhudumie nini,
Jamaa: afathal NILETEE MENU LISTI
Mhudumu: dada na wewe?
Demu akajibu kwa pozi tena kwakujishaua, “NA MIMI NILETEE MENU LIST ILA USIWEKE CHUMVI NYINGI”
Chezea mbulula weweโฆ!!!
Ameniomba nimfungulie akaunt facebook cheki nilichomjibu
Leo nimechoka zangu alafu shangazi amekuja anataka nimuunganishe facebook. Imebidi nimwambie
lazima awe na picha passport size 4 kwaajili ya kuweka profile picture, barua kutoka kwa afisa mtendaji na Atm card ya nmb bank. Alafu awe na marefa wanne ambao wamekuwa facebook for more than 3 years. Amesema
hataki tena kujiunga fb!
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Saa ivi niko zangu nimelala naendelea kupunguza uchovu
Angalia kilichotokea baada ya dogo kupewa ada na kuitumia kubeti
Dogo kampigia simu baba yake;
DOGO: Baba katika zile shilingi laki mbili ulizonipa
nikalipe ada nimetumia shilingi alfu 30 kubeti
BABA : Unasema nini we mpumbavu mshenzi
mkubwa? Nimekukanya mara ngapi kuhusu kubeti?
DOGO : Lakini baba
BABA : Lakini baba nini ngoja urudi utaona
ntakachofanya.
DOGO : Nilitaka kukwambia kuwa nimeshinda
shilingi milioni 3
BABA : Ndio hayo ninayosema wewe mpumbavu
sana kwanini hukutumia laki nzima kubeti? Si
ungepata pesa nyingi zaidi? Ngoja urudi niwataarifu
ndugu zako kuhusu uulivyo na akili za kuamua
haraka mwanangu mpenziโฆ
๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Huyu panya wa tatu ni noma
๐ ๐ ๐ย Panya watatu walikua wakibishana nani Ni noma zaidi
Panya 1:ย jamani mimi ni noma Wiki hii nimekula rat rat(sumu ya panya) mara tatu na sijadedi !!!
Panya 2ย Wewe unasema nini, mimi nimekula nyama ikiwa
kwa mtego mara 5 nasijawahi dakwa
RAT 3ย Mmemaliza? Mie hata sijui mnabishana nini? Mimi hii mimba niliyo nayo ni ya paka !!!
Panya WA 1 na 2 wakazimia๐๐๐๐๐
Panya wa 3 huwa hapendi ujinga kabisa
Sababu ya mke kupewa dawa badala ya mumewe
Dokta: Mama tumemchunguza mumeo kwa makini sana, jopo lote la madaktari tumekubaliana mumeo anahitaji mapumziko japo ya mwezi. Sasa tafadhali chukua hivi vidonge vya usingizi vitasaidia sana.
Mama: Asanteni sana, sasa niwe nampa mara ngapi?
Dokta: Unatakiwa wewe uwe unakunywa vidonge hivi kutwa mara tatu kwa mwezi mzima, mumeo atapona.
Recent Comments