Vituko Vya Kukuburudisha
Mume mgonjwa kazua mpya baada ya kuruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospitali alipokuwa kalazwa
John aliruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospital ya
Vichaa, akapakiwa ktk ambulance hadi karibu na
nyumbani kwake, akaulizwa kwako unapakumbuka?
akajibu ndio nyumba yangu ilee, mara wakatoka
watoto wawili wamevaa uniform akasema watoto
wangu walee wanakwenda shule..
Akatoka mwanamke akasema na mke wangu yulee,
Ghafla akatoka mwanaume john akasema mimi
yuleeeeeeee…. naenda kazini!! JE, NI KWELI
AMEPONA??
Kizungu nacho ni sheeeedeer
Mtalii: Do you have vegetables here.
Mtafsiri: Mnavyo vijimeza hapa.
Waiter: Vijimeza vidogo hatuna.
Mtafsiri: No sir, they don’t have.
Mtalii: OK, fine, do you have hot dogs.
Mtafsiri: Sawa, je mnao mbwa wa moto.
Waiter: Loh! Bwana we, hatupiki mbwa hapa.
Mtafsiri: They don’t cook here
Mtalii: What type of snacks do you have here.
Mtafsiri: Aina ngapi ya nyoka mnao hapa,
Waiter: We bwana we hapa hatupiki aina yeyote
ya nyoka, mwache akale nyumbani kwao.
Mtafsiri: They don’t cook any type of snacks
here,
maybe you can go back and eat at home.
Mtalii: OK, at least give us a cocktail juice.
Mtafsiri: OK, tupatie hata juisi ya mkia wa jogoo.
Waiter: Hebu tokeni na bangi zenu hapa, tena
sasa hivi kabla sijakasirika.
Mtafsiri: Lets get out of here
😝😝😝😂😂😂
Usicheke pekeyako
Mlevi kazua tafrani, angalia alichokifanya hapa
MLEVI mmoja aliingia baa akavuta kiti na kukaa mhudumu akatokea kumsikiliza.
MHUDUMU: Nikusaidie nini?
MLEVI: Eeh! nipe bia ya baridi kisaha wasikilize wote waliokaa hapa, wape bia na wao maana sipendi kunywa pombe wengine wananiangalia
Akaja mhudumu wa jikoni “nikusaidie nini?”
MLEVI: Niletee supu kisha wasikilize wote waliokaa hapa na wao wape supu sipendi kunywa supu watu wananiangalia
Safari hii watu wakapiga makofi
Baadae akamuita mhudumu
MLEVI: Niandikie bili zangu kisha waandikie wote bili zao sipendi kulipa huku watu wananiangalia
Wale wateja wakamvaa na kumshushia kichapo… teh teh teh teh teh hii kali hakuna cha bure mjini hahahaha na jasho la mtu haliliwi wandugu
Je, hili nalo ulilipitia ulipokua Shuleni?
Hakuna Kitu Kilikua Kinaniumizaga Kipindi Nipo Shuleni.
Time Mmetoka Kwenye Mitihani Wa Mathematics Halafu Mpo Kikundi Fulani Either Mnarudi Nyumbani Au Mnapumzika Kwa Ajili Ya Next Exam.
Unasikia Jamaa Wanabishana Pale Jibu Lilikua 4 Mwingine Anasema 5, Na Wewe Ulijaza 80.
Eti kwa nini Watu hawapostigi hii? Hata selfie sijaonaga
Vijana mkiwa mnaendesha magari mna post mukiwa mpo beach mna post mkiwa kwenye masherehe mna post Lakin mkiwa mmeenda kwa mganga siwaoni kupost mitunguli na vibuyu vya mganga unakuwa je wa zee tena. 😀😀😀😀
Baada ya kuumizwa kimapenzi haya ndiyo maneno
Mkishaumizwa ndo utasikia, Moyo sukuma damu sio mengine. wakati mnapenda mlizani moyo ulikuwa unasukuma kinyesi!!!!!??????😂😂😂😂
Watoto wa siku hizi ni shida! Angalia huyu mtoto anachomwambia baba yake
Ka ni wewe?
DOGO: baba mi siendi tena shule inaonekana walimu hawana uhakika na majibu yao.
BABA: Kwanini unasema hivyo?
DOGO: juzi walisema 3+4= 7, jana wakasema 1+6=7, halafu leo wanasema 5+2=7 sasa huoni kama wanatuchanganya.
ungekua wewe ungemjibu nini
Baada ya kunitumia SMS usiku ikawa hivi….
Jana usiku kuna Jirani yangu..kanitumia text “mambo vipi?”…halafu tunakaa nae mtaa mmoja nikaona nikimjibu ni uharibifu wa hela nikaenda kumgongea mlango saa 7 usiku. Alipofungua nikamjibu “shwari”halafu nikarudi nyumbani kulala zangu..
Sipendagi kuchezea salio..
😂😂😂😂😂
Wabongo ni noma! Angalia huyu mbongo anachokifanya
Basi juzi kati hapa sehemu ndogo ya ukuta wa Ikulu ya Magogoni ilianguka!..
Wakapelekwa contractors watatu ili achaguliwe mmoja atakayejenga vzr na kwa bei nafuu!..
Wakwanza alikuwa MUHINDI, wa pili MCHINA na MBONGO!…
MUHINDI: “ntajenga kwa milioni 90!.., 40 za vifaa, 40 za mafundi na milioni 10 faida yangu”
MCHINA: “mi ntajenga kwa milioni 70!.., 30 za vifaa, 30 za mafundi na milioni 10 faida yangu”
MBONGO kuona vile akamvuta chemba msimamizi wa Magogoni!..
MBONGO: “mi ntajenga kwa milioni 270”
MSIMAMIZI WA MAGOGONI: “we una wazimu nn!.. yaani unathubutu kusema hivyo na unaona wenzako wametaja kiwango kidogo?!.”
MBONGO: “milioni 100 zako, 100 zangu alafu hiyo milioni 70 tunaajiri yule mchina”
Ziara za kushtukiza zinachekesha sana
Mimi Nimecheka sana
👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
ZIARA ZA KUSHTUKIZA😀😀
Mimi ni msomaji mzuri wa magazeti, na msikilizaji mzuri wa redio, huwa naangalia luninga mara chache sana kama nikibahatika kupita mahala kuna luninga. Sasa wiki hii nimesikia mengi kuhusu hizi ziara za kushtukiza za viongozi wetu, nikaona hili ni jambo zuri tena linafaa kuigwa na sisi wananchi wapenda maendeleo. Nikaona nijipange na mimi nifanye ziara kadhaa za kushtukiza katika sehemu mbalimbali zinazonihusu.
Nikaona nianze na ziara ya kushtukiza pale shuleni kwa huyu mwanangu, maana kila siku anakunywa chai na kuondoka na daftari zake na mie sijawahi kwenda shuleni kwao toka nilipomuandikisha shule mwezi Januari. Nilifika shuleni na kumuona mwalimu mkuu, ambae alianza kutetemeka nilipomuambia kuwa nimekuja pale kwa ziara ya kustukiza, sijui alidhani mi ni mmoja wa Mawaziri wapya, maana nilimuona jasho linamtiririka ghafla. Akanikaribisha ofisi yake iliyokuwa na vitabu kila kona, na kuita waalimu wote na kunitambulisha kuwa ni kiongozi nimekuja kwenye ziara ya kustukiza.
Nilipojitambulisha kuwa ni mzazi, waalimu wote nikawaona waanza kupumua kwa raha. Nikawaambia kuwa mimi nina mwanafunzi pale na nilikuja ziara ya kustukiza kujua maendeleo yake. Baada ya mwalimu mkuu kusaka jina la mwanangu nae akanambia, “Mzee huyu mtoto hajaja shule mwezi wa tatu sasa, tulijaribu kukutafuta ikashindikana, hatujui yu wapi” Jasho likaanza kunitoka mimi, yule mtoto kila asubuhi nampa nauli anaenda shule, na mara nyingi ananiomba michango kumbe hata shule haji. Niliondoka bila kuaga presha ikiwa juu.
Nikaona niende kwenye genge la mke wangu nae nikamfanyie ziara ya ghafla nimhadithie mambo ya mwanae, nilipofika pale nikakuta kuna mdada mwingine anauza genge. Nikamsalimu, na kumuuliza mwenye genge ntampataje, jibu lake lingeniua kama ningekuwa si mkakamavu, “Mume wake kaja kumchukua na gari wameenda kununua shamba Bagamoyo”. Nikaondoka nimechanganyikiwa, nikajuwa hapa dawa yangu moja tu, nayo ni Sabrina, mtoto wa Kinyaturu pale ambapo nikipata maudhi huwa naenda kubembelezwa.
Nikatwanga mguu kwa Sabrina nae nikamfanyie ziara ya ghafla ili anipoze moyo. Nilipogonga mlango wa chumba chake akatoka mbaba wa miraba minne, akanisalimia kwa upole, “Salama kaka unasemaje?” Jibu likanitoka “Samahani mie nilimkopesha huyu dada wa chumba hiki vitenge, nilikuja kuuliza kama ameshapata hela yangu” Ziara za kushtukiza zinataka moyo wa chuma jamani
Recent Comments