Vituko Vya Kukubadilisha Mood

Kilichotokea kati ya mkaka na mdada walipokutana hotelini

Mkaka aliingia kwenye hoteli moja akaketi meza moja na mdada mrembo maarufu sana;
MKAKA: Samahani dada sijui saa ngapi?
MDADA: Nani kakwambia saa yangu ndio ya kuangalia kila mtu?

MKAKA: Samahani sana….jamaa akachukua Galaxy yake akapiga simu….aise saa ngapi saa hizi? mi ndio nimeingia toka USA nataka kurekibisha saa yangu ifwate muda wa huku. Na wewe uwahi kuchukua iPad nimekuja nazo tatu tu za zawadi. Halafu ntafutie mtoto mzuri nimumwagie midola niliyokuja nayo, ok ciao tuonane badae.
MDADA: Kaka samahani saa hizi ni saa…..
MKAKA: Achana na mimi wewe

Ha ha ha ha haaaaa!!

Angalia huyu secretary anavyomjibu bosi wake

Boss mmoja aliingia kazini kwake kasahau kufunga zipu ya suruali yake sasa secretary wake akamfuata na mazungumzo yakawa hivi:

SECRETARY: Boss leo umesahau kufunga geti nyumbani kwako…

Boss akabaki anashangaa… Baadae wakati anakwenda chooni kujisaidia ile anataka kufungua zipu akaikuta iko wazi ndio akajua alichokuwa ameambiwa na Secretary wake.

Akarudi mpaka kwa secretary na mazungumzo yakaendelea:

BOSS: Bibie ulivyoona geti wazi je uliona benz langu lime paki au…?

SECRETARY: Hapana Boss niliona kitoroli kidogo kimepaki kina matairi mawili

Kisa cha mzaramo na mchaga

MZARAMO V/S MCHAGA.
Mzaramo alitangaza anatibu magonjwa yooooooote
kwa tsh. 100,000/=
Na kama akishindwa kukutibu anakurudishia laki
yako nakukuongeza laki nyingine.
MCHAGA akaona hii fursa yakujipatia hela aiwezi mpita akaenda kutibiwa.
MZARAMO: “unaumwa nini?”
MCHAGA: “Sisikii ladha ya aina yoyote mdomoni kabisaaaa..”
MZARAMO: “sawa, toa laki kabisa..”
Mchaga akatoa.
MZARAMO akamuagiza msaidizi wake; “Naomba kikopo no.27 mpe anywe huyu..”
MCHAGA akanywa akatema faster; “Puh puu puu, Aisee huu si mkojo huu..?”
MZARAMO: “Umepona karibu tena..”
Mchaga aka-mind sana Kesho yake akarudi tena hakuamini ameliwa pesa yake.
MCHAGA: aisee nina tatizo la kumbukumbu nasahau
sanaaaaa..”
MZARAMO akamwambia “hakuna tabu, toa laki tukupe tiba..’
MCHAGA akatoa pesa akijua leo lazima afanikiwe..’
MZARAMO: “nesi naomba kikopo no.27..”
MCHAGA: “ASA CHALII ANGU HICHO SI CHA JANA CHA MKOJO HICHO AISEE..?”
MZARAMO: “UMEPONA KUMBUKUMBU UNAYO.

😄😄😄😄😁😁😁😁😁😁

Cheki tabia za kuandika vimaneno vya ajabuajabu kwenye pikipiki na bodaboda ilivyomponza huyu

Jamaa mmoja dereva wa bajaji alianguka, sasa bajaji ikawa imem’bana akawa anafurukuta bila mafanikio Cha ajabu watu wakawa wanampita bila kumsaidia, Kumbe Nyuma ya Bajaji yake alikua Kaandika “NIACHENI KAMA NILIVYO, HII NDIO STYLE YANGU” 😂😂😂 Mpaka sasa nimemwacha bado yuko hapo *Sipendagi Ujinga mimi* 🚶🏽🚶🏽🚶🏽🚶🏽🚶🏽

Kuwa na mahusiano na msichana kama huyu ni changamoto, Mabinti bwana!

Binti: Hallow mpenzi, Mambo

Jamaa: Poa baby

Binti:Uko wapi?

Jamaa: Niko town napata lunch

Binti: Wow unarudi saa ngap? Nina njaa dear naomba uniletee msosi

Jamaa: Narudi baada ya nusu saa nikuletee nini?

Binti: Niletee chipsi kuku, soseji, mayai manne ya kukaangwa pembeni, baga, piza, coke take away baridi, mkate wa moto kwenye ile bekari ya wapemba na maji ya kunywa ya kiimanjaro.

Jamaa:Umesahau viti, meza, masufuria, sahani na beseni na vijiko.

Binti: Kwanini dear?

Jamaa: Naona hutaki kula unataka kufungua hoteli!

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About