Vituko Vya Kisasa

Utoto raha..! Angalia hawa watoto wanachokifanya sasa

Leo nimepulizia Air Fresh yenye Harufu ya Pilau nyumbani kwangu sasa watoto wa Jirani wamehamia Mlangoni kwangu ndio wanacheza hapo. Kila nikitoka wananisalimia. Mama yao ndio kanimaliza kabisa nimetoka akaniambia

“Kumbe wewe ni Mpishi mzuri, Hongera”

Imebidi nisirudi nyumbani maana wale watoto wanaweza kuingia ndani kabisa na pilau hakuna.

#UTOTO RAHA 😂

😂😂😂😂👆🏻👆🏻👆🏻

Angalia huyu secretary anavyomjibu bosi wake

Boss mmoja aliingia kazini kwake kasahau kufunga zipu ya suruali yake sasa secretary wake akamfuata na mazungumzo yakawa hivi:

SECRETARY: Boss leo umesahau kufunga geti nyumbani kwako…

Boss akabaki anashangaa… Baadae wakati anakwenda chooni kujisaidia ile anataka kufungua zipu akaikuta iko wazi ndio akajua alichokuwa ameambiwa na Secretary wake.

Akarudi mpaka kwa secretary na mazungumzo yakaendelea:

BOSS: Bibie ulivyoona geti wazi je uliona benz langu lime paki au…?

SECRETARY: Hapana Boss niliona kitoroli kidogo kimepaki kina matairi mawili

Mjini shule. Soma hii

Kuna mdada nilimkopesha pesa kwa ahadi kuwa baada ya wiki moja atanirejeshea pesa zangu.

Baada ya wiki moja nampigia simu hapokei simu zangu, nimempigia zaidi ya mara kumi (10) bila ya mafanikio!

Kila nikimpigia simu hajibu simu zangu, nikahamua kumwandikia message kwa WhatsApp…!

_Hello Mamu, Nakupigia simu sio kukudai pesa zangu, ila nataka kukwambia kuwa hapa Ubungo Plaza kuna wadada wawili walikuwa wanapigana kumgombea Mumeo (Baba Nang’oto). Ilikuwa vuta nikuvute na mumeo alikuwa kasimama tu anawaangalia akitabasamu. Baada ugomvi kwisha akaondoka na mmoja wao na kumwacha yule mwingine akitukana matusi kama ana akili nzuri._


_*Kisha nikaituma ile message*_

Baada ya dakika kama mbili hivi, akanipigia simu nami wala sikupokea simu yake… Akapiga tena na tena kama mara ishirini hivi wala sikupokea.

*Akatuma message akiniuliza…*

_Hao wanawake unawajuwa, …mume wangu na huyo mwanamke wameelekea wapi, wewe unawajuwa hao wanawake waliopigana, yaani hapa nimechanganyikiwa kwa kweli…!_

Nikaisoma message yake wala sikuijibu, nikamchunia kimyaaa…!

Akanipigia tena simu mara tano, sikupokea simu zake, kimyaaa…! Akaniandikia message nyingine….

*…Nakupigia jamani pokea simu basi nina pesa zako nataka nikupe… Naomba basi tukutane mjini unihadithie vizuri…!*

Nami nikamjibu…

_Nitumie hizo pesa kwenye Namba yangu ya Mpesa, ili nipitie sheli kujaza mafuta nije mjini kukupitia nikupeleke mahala walipo…!_

Baada ya dakika 2 message ikaingia, kuangalia balance yangu ya Mpesa, nikakuta kaingiza pesa zangu zote ninazo mdai…!

Nikazima simu nikajilalia zangu kimyaaa…. Kama sio mie!

Kilichompata huyu jamaa akiwa anaangalia mpira mechi kali na mke wake

WIFE: Baibie, yule ni nani? Ni Chris Brown??
HUSBAND: Yule ni Theo Walcott
WIFE: ile Yellow Card ni ya nini?

HUSBAND: ile ni ya Onyo, na Red Card inamaanisha mchezaji awache kucheza na atoke inje ya uwanja.
WIFE: Oooooh! Inakaa kama traffic light! Yellow- Ilani na Red – Simama
HUSBAND: Yeah yeah swity! Ndio hivyo.
WIFE: Na je Green Card??
HUSBAND: Aaaah! Hakuna kitu kama hicho.

WIFE: Nataka Arsenal ishinde world cup.
HUSBAND: [kimya]
WIFE: Ni nani yule mzee anakaa kama Mr. Bean??
HUSBAND: Yeees swity, yule ni kocha wa Arsenal, anaitwa Arsene Wenger.
WIFE: Oooooh! inamaanisha yule kocha mwengine ni Chelsea Wenger??
HUSBAND: [Kabadilisha channel]

Shopping Cart
2
    2
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About