Vituko Vya Kisasa Tuu

Cheki hawa washikaji wanachokifanya baada ya kuvuta bangi, Bangi si mchezo

Kuna washikaji walikuwa wakivuta bangi… kiberiti kikawaishia… wakamtuma mwenzao akatafute kingine… bangi lilikuwa limemkolea… akazungukazunguka hatimaye akarudi palepale kijiweni…

MSHIKAJI: oyaaa wanangu eeeh… niazimeni kiberiti mwanangu mwenyewe …..

WENZAKE: baharia ee subiria kimtindo kuna mwana tumemtuma akatafute kiberiti.

Angalia kilichotokea baada ya dogo kupewa ada na kuitumia kubeti

Dogo kampigia simu baba yake;
DOGO: Baba katika zile shilingi laki mbili ulizonipa
nikalipe ada nimetumia shilingi alfu 30 kubeti
BABA : Unasema nini we mpumbavu mshenzi
mkubwa? Nimekukanya mara ngapi kuhusu kubeti?
DOGO : Lakini baba
BABA : Lakini baba nini ngoja urudi utaona
ntakachofanya.
DOGO : Nilitaka kukwambia kuwa nimeshinda
shilingi milioni 3
BABA : Ndio hayo ninayosema wewe mpumbavu
sana kwanini hukutumia laki nzima kubeti? Si
ungepata pesa nyingi zaidi? Ngoja urudi niwataarifu
ndugu zako kuhusu uulivyo na akili za kuamua
haraka mwanangu mpenzi…

😂😂😂😂😂😂😂😂😂

Misemo 10 bora ya kuchekesha itakayokuacha mdomo wazi

1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.

2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.

3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?

4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.

5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.

6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.

7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.

8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.

9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.

10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi
kufunika sufuria.

Unakumbuka hizi enzi za utoto?

Kitambo tukiwa watoto ulikuwa unaitwa uje ule kwa lugha tofauti kulingana na chakula kilichopikwa siku na muda husika

1. UGALI NA KUNDE
Mwitaji : 🗣Joniiiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Uje ukule

2. UGALI NA SAMAKI
Mwitaji: 🗣 we Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Unaitwa na Mama

3. WALI NA NYAMA/KUKU
Mwitaji: 🗣 Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Shauri yako!
😂😂😂😂😂😂

Usichokijua kuhusu sungura, panya na jamii yao

JE WAJUA?

Sungura, panya na Jamii zao huwa na mwendo wa kukimbia na kuruka muda wote na umri wao wa kuishi ni miaka 15. Kobe ni mnyama mwenda pole, asiye na papara wala pilika, muda mwingi hujificha na kupumzika ndani ya jumba lake akikwepa maadui. Umri wa kuishi kobe hufikia hadi miaka 300.
FUNZO: Mazoezi ni kiinimacho na uongo mtupu. Jipumzikie mwaya!!!
🏃🏾🏃🏿‍

Chezea paka wewe, Angalia kilichomkuta huyu na paka wake

Jamaa alichukua paka wake na kwenda kumtupa
mbal,aliporudi nyumban alimkuta paka
amekwisharudi,jamaa alikasirika sana.

Siku ya 2
akamchukua na kwenda naye zaid ya kilometa 50
akapiga chochoro za kutosha kisha
akamtupa,akaanza safar ya kurud nyumban
baada ya muda akampigia cm mkewe.Vp mke
wangu huyo paka yupo? MKE:Ndio mume wangu
tena ametulia hapa kwan imekuaje? JAMAA:hebu
mpe cm anielekeze njia ya kurud nimepotea😳

😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂

Cheki masifa yalivyomponza huyu, Sifa nyingine ni mbaya jamani

Mbongo, Mganda, na Mkenya walikamatwa na makosa Uchina.

Wakaambiwa adhabu ni ama kifo cha moja kwa moja au adhabu nyingine ambayo atakayeifaulu atakuwa huru, atakayeshindwa atauawa.

Basi wao wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu bahati yao.

Wakapelekwa msituni wakaambiwa kila mmoja aende kwa njia yake halafu arudi na matunda kumi ya kufanana.

Wakaingia msituni kila mtu njia yake.

… Mganda akarudi wa kwanza na machungwa kumi. Akaambiwa adhabu yake ni kumeza moja moja likiwa zima bila kufumba macho bila kulia wala kucheka wala kujitikisa mpaka yote kumi yaishe. Akameza la kwanza. Safi. Kumeza la pili, akashindwa kuvumilia akafumba macho. Akapigiwa risasi akafa.

Mkenya akaja. Ana vitunda vidogo vidogo kama pili vilaini. Akasomewa masharti. Akaanza kumeza bila kufumba macho wala kulia, wala nini… alipofika cha tisa akashindwa kuvumilia akaangua kicheko! Akapigwa risasi pia akafa.

Wakiwa kuzimu Mganda akamwuliza Mkenya, “Vipi, mbona ulishindwa kuvumilia wakati kilibaki kitunda kimoja tu?”

Mkenya akamjibu: “Mkuu, nilishindwa kuzuia kicheko maana nilimwona Mbongo anakuja na matikiti maji!”

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About