Sipendi ujinga. Cheki nilichokifanya
Nimeingia chumban nikakuta panya wamekula dawa yangu ya minyoo,
Na mimi nimechukua yakwao nikanywa.
Sipendagi ujinga mm!!
πππ
Nimeingia chumban nikakuta panya wamekula dawa yangu ya minyoo,
Na mimi nimechukua yakwao nikanywa.
Sipendagi ujinga mm!!
πππ
Akina dada mpenzi wako akikuita MAMITO usikubali
na yeye mwite MAFORONYA kama mbwai na iwe mbwaiπ€ͺπ€ͺπ€ͺπ€ͺπ€ͺπ€ͺ
Mwanafunz alikuwa kila siku anachelewa shule, na kila siku alikuwa anachapwa, basi siku moja mwalimu akaona ngoja amuulize.
Mwalimu: Mbona unachelewa kila siku?
Mwanafunzi: Nakaa mbali mwalimu
Mwalimu: (huku ana hasira akauliza)Mbali mbinguni?
Mwanafunzi: Mbinguni kwa mbeleπππππ
Wanaume wenye kushinda vishawishi ni;
Wanaume ambao mnaweza kula wali hadi mwisho bila kugusa nyama nyie ndio mnaweza kushinda vishawishiπ€£π€£π€£π€£π€£
πββπββπββπββπββπββ
Kuna mdada nilimkopesha pesa kwa ahadi kuwa baada ya wiki moja atanirejeshea pesa zangu.
Baada ya wiki moja nampigia simu hapokei simu zangu, nimempigia zaidi ya mara kumi (10) bila ya mafanikio!
Kila nikimpigia simu hajibu simu zangu, nikahamua kumwandikia message kwa WhatsAppβ¦!
_Hello Mamu, Nakupigia simu sio kukudai pesa zangu, ila nataka kukwambia kuwa hapa Ubungo Plaza kuna wadada wawili walikuwa wanapigana kumgombea Mumeo (Baba Nang’oto). Ilikuwa vuta nikuvute na mumeo alikuwa kasimama tu anawaangalia akitabasamu. Baada ugomvi kwisha akaondoka na mmoja wao na kumwacha yule mwingine akitukana matusi kama ana akili nzuri._
β
_*Kisha nikaituma ile message*_
Baada ya dakika kama mbili hivi, akanipigia simu nami wala sikupokea simu yake⦠Akapiga tena na tena kama mara ishirini hivi wala sikupokea.
*Akatuma message akiniulizaβ¦*
_Hao wanawake unawajuwa, β¦mume wangu na huyo mwanamke wameelekea wapi, wewe unawajuwa hao wanawake waliopigana, yaani hapa nimechanganyikiwa kwa kweliβ¦!_
Nikaisoma message yake wala sikuijibu, nikamchunia kimyaaaβ¦!
Akanipigia tena simu mara tano, sikupokea simu zake, kimyaaaβ¦! Akaniandikia message nyingineβ¦.
*β¦Nakupigia jamani pokea simu basi nina pesa zako nataka nikupeβ¦ Naomba basi tukutane mjini unihadithie vizuriβ¦!*
Nami nikamjibuβ¦
_Nitumie hizo pesa kwenye Namba yangu ya Mpesa, ili nipitie sheli kujaza mafuta nije mjini kukupitia nikupeleke mahala walipoβ¦!_
Baada ya dakika 2 message ikaingia, kuangalia balance yangu ya Mpesa, nikakuta kaingiza pesa zangu zote ninazo mdaiβ¦!
Nikazima simu nikajilalia zangu kimyaaaβ¦. Kama sio mie!
πππππππππππ
π€£π€£π€£π€£
SIFA MBAYAβ¦
Jamaa alikuwa ndani ya daladala Mara simu ikaita alikuwa ni mkewe kwa sifa jamaa akaweka loud speaker ili watu wasikie wanavyopendana.
JAMAA;wife Mara hii umenimiss jaman
WIFE; kwa nini umekunywa uji wa mtoto?!!!
πππππ
GARI YA MILIONI 50
UNALAZA NJEβ¦
mke wa laki sita
unalala nae ndaniβ¦.
BANGI SI NZURI JAMAN
ππππππππ
Stress Tupu
Unapokea Sms kwa mpenzi wako anakuambia
“Kuanzia Leo Mimi Na wewe Basi! ????”
Unashtuka ??β¦. Una muuliza kulikoni? ????
Anakujibu: “Sorry Sio Sms yako?”
Hapo Ndo utajua Kwanini Hakuna Mmasai Albino??????
Jamaa mmoja dereva wa bajaji alianguka, sasa bajaji ikawa imem’bana akawa anafurukuta bila mafanikio Cha ajabu watu wakawa wanampita bila kumsaidia, Kumbe Nyuma ya Bajaji yake alikua Kaandika “NIACHENI KAMA NILIVYO, HII NDIO STYLE YANGU”Β πππΒ Mpaka sasa nimemwacha bado yuko hapoΒ *Sipendagi Ujinga mimi* πΆπ½πΆπ½πΆπ½πΆπ½πΆπ½
Boss mmoja aliingia kazini kwake kasahau kufunga zipu ya suruali yake sasa secretary wake akamfuata na mazungumzo yakawa hivi:
SECRETARY: Boss leo umesahau kufunga geti nyumbani kwakoβ¦
Boss akabaki anashangaa⦠Baadae wakati anakwenda chooni kujisaidia ile anataka kufungua zipu akaikuta iko wazi ndio akajua alichokuwa ameambiwa na Secretary wake.
Akarudi mpaka kwa secretary na mazungumzo yakaendelea:
BOSS: Bibie ulivyoona geti wazi je uliona benz langu lime paki au�
SECRETARY: Hapana Boss niliona kitoroli kidogo kimepaki kina matairi mawili
{ NGOMA DROO}
Sikuizi utawasikia wadada wakisema kuachwa na mwanaume asie na pesa nisawa na kuluhusiwa hospital
{Sasa na sisi} wanaume tunasema
Kuachwa na demu mpenda pesa nisawa na kumaliza mkopo benk ππππππ
Wanaume atutakagi ujinga!!!! Wanaume heeeeeeππΎββππΎββππΎββππΎββ
Bibi na Babu walisafiri wakielekea kwa mtoto wao ambae hawajamuona zamani.
Walipofika njiani wakawa wamechoka Sanaa. Wakaamua kutafuta hotel ili walale.
Wakakubaliana walale kwa masaa 4. Wakalala, Walipoamka, mfanyakazi wa Hotel akawatoza Tsh. 500,000/=
Wale wazee wakashangaa hata kama ni hotel ya kisasa lakini sio laki tano kwa masaa 4.
Babu akagoma kulipa akasema aitiwe meneja.
Meneja akaja kuwasikiliza
Babu: ” Kwanini bili ni kubwa hata kama ni hotel ya kisasa?”
Manager;“kuna maswiming puli, ya kisasa “
Babu; “Lakini hatukuyatumia”
Manager; “Ah ah ah. Lakini mungeweza kama mngetaka”
Babu: “Hata hivo bado haithamini kuwa laki 5”
meneja: “Pia Kuna waimbaji kutoka sauzi, Uganda , Congo”
Babu: “Lakini sisi hatukuwasikiliza”
Meneja: “Ndiooo. Lakini mngeweza kama mngetaka”
Babu; aka give up na kumwambia mkewe andika cheki uwape,,
Bibi akaandika akampa meneja.
Meneja anaangalia anaona sh. 50,000
Akashangaa na kusema. “VP mbona hamsini'”
Bibi akajibu “450,000 ya kulala na mimi”
Meneja akajibu; “Lakini sijalala”
Bibi :“ungeweza kama ungetaka”
Jamaa kavamia semina ya wasomi iliyokua inafanyika maeneo ya ubungo plaza bas wakaanza kujitambulisha
1. Naitwa Anna niko SUA mwaka3 nasoma agriculture
2. Naitwa Stella niko UDSM mwaka2 nasoma public relation
3. Naitwa Emmanuel niko UDOM mwaka3 nasoma computer science
bas jamaa nae akainuka kwa kusuasua huku akijishtukia akasema”Naitwa Elisha niko Tanesco mwaka wa 7 nasoma mita”
LEO NIMEPITA MTAA FULANI NIKAKIMBIZWA NA MBWA, NDIO NIKAJUA NINA KIPAJI KINAPOTEA TUβ¦β¦β¦
SIO CHA KUKIMBIA, NI KUPIGA KELELEππππππ
Bakari ni house boy mara nyingi huiba wine ya boss wake na kisha kuongeza maji kwenye chupa ili boss asigundue. Mara kadhaa boss alihisi ladha tofauti anapokunywa wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu alihisi tu Bakari anahusika. Ilikua ni bahati tu alimvizia na kumbamba Bakari akichakachua wine, kwa kuwa mkewe alikua anamtetea Bakari, ili kumthibitishia mkewe kuwa Bakari ndo culprit,
boss alianza kwa kumuuliza Bakari maswali. Siku hiyo Bakari alikua jikoni,boss na mkewe walikua sebuleni.
Boss:- Bakariiii!
Bakari:- Naam baba!
Boss:- Nani anakunywa wine yangu?
Bakari:- Kimyaaaa hajibu kitu! Boss:- Bakariiiii !
Bakari:- naam baba! Boss:- nauliza nani anakunywa wine yangu halafu anajazia majiii!
Bakari:- kimyaaaaa!
Boss akaamua amfuate hukohuko jikoni.
Boss: Kwanini nikikuita unaitikia, nikikuuliza unanyamaza?
Bakari: Baba huku jikoni ndo kulivyo, unasikia jina tu likiitwa lakini maneno menginehusikii, na kama huamini baki jikoni mi niende sebuleni.
Bakari akaenda sebuleni akaanza kuita.
Bakari:Babaa!
Boss: Naam Bakari!
Bakari: Saa sita usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl?
Boss:- kimyaaaa!
Bakari:- Baba babaa!
Boss:- Ndio Bakari!
Bakari:- Nauliza hivii, chumbani kwa house girl saa sita za usiku huwa wafuata nini?
Boss:- kimyaaaaaaa!
Boss akatoka nje: Bakari huku jikoni ni kweli husikii kitu zaidi ya jina!.
Mama akasema msinizingue nyieβ¦Mbona siwaelewi..
Bakar: mama kama uamini na ww nenda uone.
Mama akaenda jikoni..
Bakari: akaita mamaa
Mama : bee bakari
Bakari: eti hiyo mimba niya baba au yangu.?
Mama kimya
Bakari; mama nakauliza tena hiyo mimba niyababa au yangu.
Mama akatoka aisee kweli humu unasikia jina tuβ¦..πππππ
1:Mkimaliza kuongea niambieni niendelee kufundisha
2:Baba yako kauza ng’ombe ili alete ng’ombe mwingine shule
3:Kama unajua kuliko mimi njoo ufundishe wewe
4:Ulikuja peke yako na utaondoka peke yako
5:Hata msiponisikiliza mshahara wangu uko pale pale
6:Baba yako anahangaika kulipa ada wewe unafanya utumbo tu
7:Hata nikeshe nafundisha wengine ni mizigo hawatoki na lolote
8:Tunavisaidia tu kwan vikifanikiwa mbelen hata salam vinatoa?
9:Bichwa kubwa ubongo nukta
10:Wengine hapa wamekuja kukua tu
SHARE NA MARAFIKI ZAKO WAKUMBUKE ENZI ZA SHULE KIDOGO
Recent Comments