Vituko Vya Juma Hili
Muda mzuri wa kulipa mahari
Amini Nawaambieni
Hakuna Muda Mzuri wa Kulipa Mahari Kama Mwezi January. Baba Mkwe Anapokea Hata Buku Kumiโฆ. ๐๐๐๐๐๐
Cheki hiki kibabu kulivyowaacha watu hoi wakati mchungaji anafungisha ndoa
Mchungaji Kauliza:ย Yeyote mwenye pingamizi la haki kwa ndoa hii asimame na aje mbele.
Mara kasimama kibabu na kwenda mbele, bibi harusi alipomuona tu yule babu akazimia.
Mchungaji akauliza:ย tueleze pingamizi lako
Kibabu kikajibu:ย Nimeamua kuja mbele kwasababu kule nyuma sisikii!!!.
kanisa zima hoi,
Hapo sasa!! Ni shida!!
Umeshawahi saidiwa homework na mzazi halafu unapata zero?
Hapo ndio unajua shida siyo wewe
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Jamaa alikuwa na tabia ya kutembea na binamu yake cheki kilichomkuta
Jamaa alikuwa na tabia ya kutembea na binamu yakeโฆ.
Alikuwa anasubiri mjomba na mkewe walale tu halafu ananyata mdogo mdogo mpaka chumbani kwa binamu yake.
Siku moja umeme ulikuwa umekatika ikabidi aamue kuvua nguo kabisachumbani kwakeโฆ.
Akanyata taratibua akafungua mlango akazama chumbani kwa mjomba ake bila kujua, ghafla umeme ukarudiโฆ
MJOMBA; we mshenzi umefata nini chumbani kwangu tena uko uchi
JAMAA; nimekuja kukuaga kesho naondoka
MJOMBA; ndo uje uchi?
JAMAA; ndio kwasababu nimeshapaki kila kitu kwenye begi
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Cheki huyu jamaa alivyoumbuka kwenye harusi
Jamaa mmoja alialikwa ktk harusi. Akafika mlango Wa 1 umeandikwa kulia ni ndugu Wa maharusi, kushoto ni wageni waalikwa, akaenda kushoto maana yy alialikwa. Akakuta mlango wa2 umeandikwa kulia wenye zawadi kushoto wasionazawadi yy hakuwa na zawadi. Mlango Wa 3 umeandikwa kulia wanawake kushoto waume akapita kushoto akajikuta ametokea mtaani
๐๐๐๐๐๐๐๐. Tujifunze kutoa wandugu
*hatupendagi ujinga sisi*
๐ถ๐ฟ๐ถ๐ฟ๐ถ๐ฟ๐ถ๐ฟ๐ถ๐ฟ๐ถ๐ฟ๐ถ๐ฟ
Kama mpezi wako akikuita MAMITO Unatakiwa umjibu hivi
Akina dada mpenzi wako akikuita MAMITO usikubali
na yeye mwite MAFORONYA kama mbwai na iwe mbwai๐คช๐คช๐คช๐คช๐คช๐คช
Huyu mme ni shida
MKE..mume wangu unaweza kuua simba kwasababu yangu???
MME: Hapana mke wangu, sema kingine
MKE:unaweza kunipa nione watsapp yako nione msgs?
MME: Haya sema huyo simba yukwap nikamuue
Eti ni kweli hii ni sababu wanaume wana Upendo Sana?
Wanaume wana upendo kwa kweli.
Mwanaume hata akipewa kundi la wanawake 90 achague mmoja!! Hata akichagua mzuri kupita wote bado roho itamuuma kuwaacha wale 89 waliobaki!!*
Kwa namna hii wanaume wana Upendo Sana
๐๐๐๐๐๐
Cha kufanya mpenzi wako akikuacha
Kumkomoaโฆ
MPENZI WAKO AKIKUACHA BILA SABABU CHUKUA SIMU MPIGIE MAMA AKE MWAMBIE MWANAO AMEKUFA UWEZIโฆ. KULIA PEKE YAKO๐ค
Alichofanya mke baada ya mme wake kupenda kumchunga sana
Alifanya hivi;
Siku ya kwanza
MUME: Halooo vipi mke wangu salama weye?.
MKE: Salama tu
MUME: Uko wapi?
MKE: Jamani si niko nyumbani
MUME: Mhh kama kweli uko nyumbani washa blender nisikieโฆ..mkeยญ akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Okay haya mi natoka kazini naja
Siku ya pili
MUME: Vipi mko salama huko?
MKE: Tupo kama ulivyotuacha
MUME: kwani uko wapi?
MKE: Niko nyumbani napika
MUME: Washa brender kama kweli uko nyumbani
Mke akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Poa ntarudi baada ya masaa mawili
Siku sita baadaeย mume akaamua kurudi bila kumtaarifu mkewe alipofika home kamkuta mdada wa kazi yuko peke yake.
MUME: We mama yako yuko wapi?
MDADA: Sijui ameondoka na blender toka asubuhi
Recent Comments