Vituko Vya Juma Hili

KICHEKESHO: Ajira ngumu!! Cheki hawa walivyoamua kujiajiri

Jamaa mmoja alienda kuomba kazi Mbuga ya Wanyama, akaambiwa nafasi ya Kazi ipo ila hakuna Sokwe, “hivyo utajifanya Sokwe na tutakupa ngozi utavaa”

Jamaa siku ya kwanza akavaa, walipokuja watalii mambo yalienda vizuri, Siku iliyofuata Banda lake liliwekwa juu ya Banda la Simba, Jamaa ktk kuongeza mbwembwe akawa anarukaruka, kwa bahati mbaya si akaangukia ndani ya Banda la Simba, akawa anapiga kelele “Mama nakufaaa!”

Mara yule Simba akamwambia “Acha Ufala ww kelele za nini sasa, mimi mwenyewe Binadamu! rudi kwenye Banda lako kabla watalii hawajaja watatushtukia! chezea ajira ww”………!!

😂😂😂😂😂😂😂😂👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻

Cheka kidogo, angalia anachosema huyu mchaga

Mchaga baada ya kufa akaulizwa na malaika anayetoa roho: Mangi hapa ni njiapanda kulia ni Mbinguni na kushoto ni Jehanamu, Je unachagua kwenda wapi?

MANGI: Bwashee, mi nabaki hapa hapa njiapanda aisee.
MALAIKA: Kwa nini?
MANGI: Aisee, nikifungua duka hapa si nitapata wateja wa Mbinguni na Jehanam. Yani patakuwa senta ya hatari, supu na nyama choma muda wote. Hata we utafaidi, unavyoenda kuchukua roho unaniletea stock nakupa hela yako cash mkononi. Na kila ukipita hapa unapiga mchemsho wako wa ulimi na bia mbili chap kabla ya kuingia mbinguni.
Kwanza nashangaa Shirima alipitaje hapa bila kushika ploti, au alikufa amelewa sana?

Sababu ya jamaa kujiita fara ugenini

MZEE:”sasa huyu mgeni sijui alale wap?”
MKE:”saa hizi ni usiku akalale na Bebi.”
jamaa akaona huyo Bebi pengne mtoto anakojoa kitandani au akalia asije msumbua usiku
JAMAA:”msipate tabu mi ntalala hapa kwenye kochi” akalala
asubh wanakunywa chai akaibuka mrembo,jamaa akapigwa bumbuwazi almanusra ajimwagie chai.
BINTI:”Naitwa BEBI,we unaitwa nani?”
Jamaa akasema mimi naitwa Fara…..!

Vichekesho kumi bora vya leo vya kuvunja mbavu

1. Maswali haya je una majibi? JIBU KISHA NITUMIE MAJIBU![mtihani wa maarifa ya dunia]1. Kama hela haioti kwny miti, kwnn bank zina matawi?
2. Kwnn gundi haigandi kwenye chupa yake?
3. Kama tunatakiwa tusi-drive wkt tumekunywa, kwnn bar kuna parking?
4. Kama neno abbreviation linamaanisha ufupisho, kwnn lenyewe ni refu hvo?
5. Kama tunatakiwa kufanya sex ndani ya ndoa 2, kwnn tunabalehe kabla ya kufunga ndoa? Kazi kwako…



2.Taxi Mwanamke aliingia kwnye tax akiwa hana nguo,km alivyozaliwa!Dereva akawa anamshangaa,mwanamke akamuuliza hujawahi kuona uchi au! Dereva akajibu.ninachoshangaa c uchi wako,najiuliza pesa ya kunilipa utakuwa umeiweka wapi?


3.Siri Baba: mwanangu, enhe shika hii 500Tsh usimuambie mama yako kuwa nimelala na housegirl. Mtoto: sitaki, tatizo we baba ni mbahiri sana mwenzio mama akilala na dereva ananipaga 1,000Tsh.


4.Tendo la ndoa TENDO LA NDOA LINAVYOOMBWA:

WAMASAI: Mama Yeyo nipe ile kitu namesa mwensake

WAHAYA: Mama Koku infacti njoo tuperform

WACHAGA: Mama Manka Fungua Kibubu nitupe shilingi

WAPEMBA: Mama Ali panua paja mti waja!

WAZARAMO(hamna tafsida)andaa k*#, m*$$ yaja


5.Short na Long Call Kama haja ndogo ni ”short call” Haja kubwa ni “long call” Basi kujamba iitwe “missed call”


6.Heshima Mtoto kaona nyeti ya baba yake, Akauliza “nini hii”? Baba,akajibu “ni Heshima”, kesho yake wakaja wageni, baba akamwambia mtoto, “toa heshima kwa wageni”, mtoto akatoa Nyeti yake, akaonesha, wageni wakashangaa! mtoto akasema “mnashangaa haka kadogo, baba anayo heshima kubwaaa……!


7.Kurudi shule Mtoto kamuuliza babake; ” Eti baba, Unataka kuanza tena shule? Baba akauliza: “kwa nini Umeuliza hivyo? Mtoto akamwambia: Jana uthiku, nilickia ukimnong’oneza mama” Eti, kama anapenda, Muende la pili..! ” Hivi Baba mimi niko la nne wewe na mama itakuwaje mwende la pili? Uthikubali hata kdogo”


8.Mchaga. Mchaga alipata ajali alipozinduka pale hospitali akauliza “nipo wapi hapa?” Nesi akajibu,”umepata ajali, hapa upo hospitali. Bahati mbaya umekatika mkono.” Mgonjwa: Na je saa yangu ipo wapi ya Rolex? Ipo mzee, nesi alijibu. Nesi: Mkeo na watoto wapo hapa kukufariji. Mgonjwa: Yeuwi… Wamefunga duka?


9. Kimombo na sms Jamaa katumiwa msg na dem wake,kutokana na urefu wa msg ikashindwa kufika yote mwishoni ikaandika’some text missing’jamaa kizungu hajui hivyo maneno ya mwisho hakuelewa maana yake lkn akahisi litakuwa neno la kimahaba,kusudi aonekane mjanja akajibu, “some text missing too dear”


10.Vibweka vya housegirl Mama mwenye nyumba “jamani nyie watoto wa nyumba hii, vijiti vya meno nimeleta juzi tu leo vimeisha?” Ndipo hoousgirl akadakia na kusema “mama mimi simo humo maana kila nikitumia nikimaliza tu navirudishiaga humo humo.”

Ziara za kushtukiza zinachekesha sana

Mimi Nimecheka sana
👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

ZIARA ZA KUSHTUKIZA😀😀
Mimi ni msomaji mzuri wa magazeti, na msikilizaji mzuri wa redio, huwa naangalia luninga mara chache sana kama nikibahatika kupita mahala kuna luninga. Sasa wiki hii nimesikia mengi kuhusu hizi ziara za kushtukiza za viongozi wetu, nikaona hili ni jambo zuri tena linafaa kuigwa na sisi wananchi wapenda maendeleo. Nikaona nijipange na mimi nifanye ziara kadhaa za kushtukiza katika sehemu mbalimbali zinazonihusu.

Nikaona nianze na ziara ya kushtukiza pale shuleni kwa huyu mwanangu, maana kila siku anakunywa chai na kuondoka na daftari zake na mie sijawahi kwenda shuleni kwao toka nilipomuandikisha shule mwezi Januari. Nilifika shuleni na kumuona mwalimu mkuu, ambae alianza kutetemeka nilipomuambia kuwa nimekuja pale kwa ziara ya kustukiza, sijui alidhani mi ni mmoja wa Mawaziri wapya, maana nilimuona jasho linamtiririka ghafla. Akanikaribisha ofisi yake iliyokuwa na vitabu kila kona, na kuita waalimu wote na kunitambulisha kuwa ni kiongozi nimekuja kwenye ziara ya kustukiza.

Nilipojitambulisha kuwa ni mzazi, waalimu wote nikawaona waanza kupumua kwa raha. Nikawaambia kuwa mimi nina mwanafunzi pale na nilikuja ziara ya kustukiza kujua maendeleo yake. Baada ya mwalimu mkuu kusaka jina la mwanangu nae akanambia, “Mzee huyu mtoto hajaja shule mwezi wa tatu sasa, tulijaribu kukutafuta ikashindikana, hatujui yu wapi” Jasho likaanza kunitoka mimi, yule mtoto kila asubuhi nampa nauli anaenda shule, na mara nyingi ananiomba michango kumbe hata shule haji. Niliondoka bila kuaga presha ikiwa juu.

Nikaona niende kwenye genge la mke wangu nae nikamfanyie ziara ya ghafla nimhadithie mambo ya mwanae, nilipofika pale nikakuta kuna mdada mwingine anauza genge. Nikamsalimu, na kumuuliza mwenye genge ntampataje, jibu lake lingeniua kama ningekuwa si mkakamavu, “Mume wake kaja kumchukua na gari wameenda kununua shamba Bagamoyo”. Nikaondoka nimechanganyikiwa, nikajuwa hapa dawa yangu moja tu, nayo ni Sabrina, mtoto wa Kinyaturu pale ambapo nikipata maudhi huwa naenda kubembelezwa.

Nikatwanga mguu kwa Sabrina nae nikamfanyie ziara ya ghafla ili anipoze moyo. Nilipogonga mlango wa chumba chake akatoka mbaba wa miraba minne, akanisalimia kwa upole, “Salama kaka unasemaje?” Jibu likanitoka “Samahani mie nilimkopesha huyu dada wa chumba hiki vitenge, nilikuja kuuliza kama ameshapata hela yangu” Ziara za kushtukiza zinataka moyo wa chuma jamani

Makonda wana mambo, Kila mtu ni ndugu yao

Hakuna m2 mwenye ndugu wengi kama konda wa daladala.

Utasikia,
“HAYA, DADA HAPO MBELE, MJOMBA KULE MWISHO.
MA-MDOGO UNAENDA?,
NGOJA ASHUKE BIBI.
HAYA SHEMEJI UMEIKUTA YA KUWAH.
Babu njoo ukae!
Baba angu hapo tusogee kidogo,

Shangazi maliza ngazi,
Swaiba geukia mbele,
Kaka hapo shika upande wa pili,
Mdogo wangu mpishe Ma Mkwe akae.
Subiri Shemeji yako apande…

Duh… makonda noma…!!

Huyu mgeni wa huyu jamaa ni shida

Pale unapokuwa umefulia sana…

Mgeni anakutembelea Maskani kwako….Unaamua Kuchukua Ile Sh 600 iliyobaki na kwenda Dukani Kumnunulia Soda Unaondoka na Chupa Mbili Unanunua Fanta Moja kwaajil ya Mgeni na Ile Chupa ya Sprite Unaijaza Maji ili Ukirudi Uweze kumpa Kampani Mgeni……Unafika Seblen Unampa Ile soda ya Fanta Mgeni anakuambia Fanta huwa situmii Nipe hiyo sprite …..Bwana….Bwana. …Bwana….Weee 😂😂😂😂😂😂😂😂

Kilichowakuta boss, mke wake na mfanyakazi wao

Bakari ni house boy mara nyingi huiba wine ya boss wake na kisha kuongeza maji kwenye chupa ili boss asigundue.
Mara kadhaa boss alihisi ladha tofauti anapokunywa wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu alihisi tu Bakari anahusika.
Ilikua ni bahati tu alimvizia na
kumbamba Bakari akichakachua wine, kwa kuwa mkewe alikua
anamtetea Bakari, ili kumthibitishia mkewe kuwa Bakari ndo culprit, boss alianza kwa kumuuliza Bakari maswali.
Siku hiyo Bakari alikua jikoni, boss na mkewe walikua sebuleni.

Boss: Bakariiii!
Bakari: Naam baba!
Boss: nani anakunywa wine yangu?
Bakari kimyaaaa hajibu kitu!
Boss: Bakariiiii !
Bakari: naam baba!
Boss: nauliza nani anakunywa wine yangu halafu anajazia majiii!
Bakari kimyaaaaa!

Boss akaamua amfuate hukohuko jikoni.
Boss: Kwanini nikikuita unaitikia, nikikuuliza unanyamaza?
Bakari: baba huku jikoni ndo kulivyo, unasikia jina tu likiitwa lakini maneno menginehusikii, na kama huamini baki jikoni mi niende sebuleni.

Bakari akaenda sebuleni akaanza kuita.
Bakari:Babaa!
Boss: naam Bakari!
Bakari: Saa sita usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl?

Boss kimyaaaa!
Bakari: Baba babaa!
Boss:ndio Bakari!
Bakari: Nauliza hivii, chumbani kwa house girl saa sita za usiku huwa wafuata nini?

Boss kimyaaaaaaa!
Boss akatoka nje: Bakari huku jikoni ni kweli husikii kitu zaidi ya jina!

Mke wa Boss akaingilia kati
Mama: nyie msinitanie kabisa mnasemaje?
Bakari: kweli mama ukiwa jikoni husikii kitu nenda uone

Mama akaenda na Bakari akaanza

Bakari: mamaaaa!
Mama: abeee!
Bakari: hebu niambie hiyo mimba ni ya baba au yangu?
Mama kimya

Bakari: mamaaaa!
Mama: abeeee!
Bakari: hebu niambie ukweli hiyo mimba ni ya baba au yangu??
Mama kimya

Mama akatoka nje: kweli humu jikoni kuna tatizo nilikuwa nasikia jina tu

Hii ndiyo Ladha ya bia zote usiyoijua

Ladha ya bia ya 1 hadi ya 6..

Kwa wanywaji wazuri wa bia,

chupa ya kwanza 🍺 huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza koo… Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.

chupa ya pili 🍺🍺 kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihi….

Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wachezaji wa Yanga bila kukosea.. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.

Bia ya tatu 🍺🍺🍺 huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sana…. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokeza…..

Bia ya nne 🍺🍺🍺🍺 huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikia….. bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.

Bia ya tano 🍺🍺🍺🍺🍺 ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipu……na kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; ‘Mi sipendwi mpaka leo sijaolewa’ au ‘ Mume wangu sijui yukoje hanijali’

Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.

Kuanzia bia ya sita 🍺🍺🍺🍺🍺🍺 na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana. ……. …Kuna watu husema ukilewa ndipo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamueleza ukweli jinsi alivyo fala na hajui kuendesha kampuni.

Au unasema ukweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Kimsingi uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao pia uchumba unaweza kuvunjika…….

Jinsi ya Kubana matumizi X-mass

Badala yakupika PILAU tutapika TAMBI kwenye Xmas maana tutakua tumeokoa sh.15,000/= Vitunguu swaumu 2000, Vitunguu maji 1000, hiliki 1000, Magome 1000, Michele wa 2000, Soda 3000, Nyama 5000 . Fedha hizi zitatumika kununua mfuko wa cement ili tuanze kujaza kibubu cha ujenzi wa nyumba badala ya kupanga. Karibuni saana maji ya kunywa tumechemsha ndoo nzima.

🎀✨Marry Xmas & Happy new year.✨🎀

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About