Vituko Vya Ijumaa

Kilichompata sista duu bishoo wakati akijidai kununua pete

Mwanamke mmoja aliingia duka la vito vya thamani, akaona pete moja ya dhahabu nzuri sana amabayo ilikuwa kwenye shelf ya chini, wakati anainama apate kuitazama vizuri kwa bahati mbaya (au nzuri!), shuzi likamtoka- druuuuuu, soni ikamuingia huku akigeuka haraka kuangalia kama kuna yeyote dukani pale ameliskia shuzi lake, macho yakagongana na mwenye duka ambaye alikuwa karibu huku uso ukiwa umejaa tabasamu zito, mwana mama hakuwa na uhakika kama amesikika au hakusikika, akaona atumie nafasi ile kuyeyusha…Akauliza “Hii pete bei gani?” . Jamaa mwenye duka, huku akiangua kicheko, akajibu “Umeiona tu umejamba, je nikikuambia bei yake si utakunya kabisa?”

Tofauti ya mke na mchepuko!!!

Mke ni kama Tv na Mchepuko ni kama Simu.
Nyumbani unaangalia Tv lakini ukitoka unatoka na simu.

Mara chache unafurahia Tv lakini Muda mrefu unacheza na simu yako.

Tv ni bure kwa maisha yako yote, lakini Simu kama hujalipia hupati huduma.

Tv ni kubwa nzito na wakati wote ni ya zamani. Lakini simu ni nzuri, nyembamba, na ni rahisi kubeba.

Gharama za huduma za tv ni ndogo sana, Lakini gharama za huduma za Simu ni kubwa na pia ni lazima kuzitimiza.

Tv ina remote lakini Simu haina.

Kitu muhimu zaidi simu ina njia mbili za kuwasiliana unaongea na unasikiliza lakini Tv unalazimika kusikiliza hata kama hutaki au unataka.

Unaweza kununua Tv mara moja na ukatumia kwa kipindi kirefu lakini Simu mara zote unabadilisha inategemea na fasheni.

Ya mwisho na ya kuzingatia

Tv haina Virusi lakini Simu inayo.

KUWA MAKINI.

Baada ya mwanamke kukataa kufungua mlango angalia kilichomkuta

MUME: Fungua mlango!

MKE: Leo sifungui! Nimechoshwa na ulevi wako.

MUME: kama hufungui najitupa kwenye hili shimo nife kabisa.

MKE. Kufa huna faida yoyote duniani!

MUME kachukua jiwe kubwa kalitupa kwenye shimo chubwiiiiiii!

MKE kajifunga kanga, kafungua mlango. Ghafla mume kaingia ndani na kumfungia mke nje.

MKE: Nifungulie la sivyo nitapiga kelele majirani waje.

MUME: Piga kelele na wakija uwambie unakotoka usiku huu na khanga moja.

Angalia sababu ya mwanamme kubadili jina na Kuitwa jina la kike, hii dunia ina mambo kweli

Rashidi alimpa ujauzito mwanafunzi, akashtakiwa.
Kumbe Rashidi ana bibi yake mtaalamu wa yale mambo yao ya Sumbawanga, akampachika Rashidi i jinsia ya kike.

Alipofika mahakamani kuhojiwa Rashidi akasema sijampa ujauzito kwa sababu mimi pia nina jinsia ya kike.
Kwa kuthibitisha Rashid wakaenda kumkagua basi akashinda kesi, kufika nyumbani Rashid akawakuta watu wamejaa wanalia, akauliza kulikoni?
Akaambiwa bibi yako amefariki. 😭😭😭😭😭😭😰😰😰😆😆😆😆😆😆
Kwa sasa Rashid anaitwa Leila😀😀😀

Cheki kilichonipata sasa, ungekua wewe ungefanyaje?

Siku moja katika pitapita zangu nikakutana na mtoto mmoja mkali balaa yaani ni mzuri sanaaaa, moyo ukanituma nimuimbishe mtoto akakubali kwamba nitafute siku tukae tuongee vizuri akasema nimpe namba yangu ya simu.

 

Ebwana si akatoa simu hiyo inauzwa laki sita mimi hapa nina kisimu cha tochi tena nimefunga na rababendi
Je, wewe ungeendelea kumtajia namba zako!!!

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About