Visa Vya Xmass
Tofauti kati ya mwanamke na mwanamme
UTOFAUTI KATI YA MWANAMKE NA MWANAUME
1. Kwenye mshituko; mwanaume hushituka halafu huangalia nini kimemshitua, mwanamke hushituka halafu huzimia hivyo ataambiwa na mwanaume kilichomshitua๐๐
2. Kwenye kupenda; mwanaume huanza kutamani alafu hupenda, mwanamke huanza kupenda moja kwa moja bila kumjua vizuri huyo ampendae๐๐๐
3.Kwenye kusaidia; mwanaume hutoa msaada alafu uhuzunika, mwanamke huuzunika badae ndo anakumbuka km msaada unahitajika๐๐๐
4.Kwenye maamuzi; mwanaume hufikiri ndipo hutenda, mwanamke hutenda halafu hufikiri๐๐๐
5.Kwenye kudanganya; Mwanaume hudanganya ili kumlinda mwanamke, mwanamke hudanganya ili kumkomoa mwanaume๐๐๐
6.Kwenye ugomvi; wanaume hupigana halafu hueshimiana, wanawake hupiga mikelele alafu kila mmoja hurud kwake, kexho tena๐๐๐
7.Kwenye ndoa; mwanaume hutafuta maixha ndipo huoa, mwanamke huolewa ndipo atafute maisha๐๐๐
8.Kwenye kukata tamaa; mwanaume hukata tamaa mapema ili jambo lisimsumbue, mwanamke hajui kukata tamaa hadi aumizwe๐๐๐
9.Kwenye kula;Mwanaume hushiba alafu huanza madoido, mwanamke huanza na madoido alafu badae hujilaumu hakushiba๐๐
10.Kwenye siri; Mwanaume hutunza siri hasa za aibu, mwanamke humueleza shoga yake badae hugombana nae baada ya kumrudia mwenyewe kwa siku 2 tu๐๐๐
Hizi ni baadhi tu ya sifa tofauti kati ya mwanaume na mwanamkeโฆ.. VIVA GENTLEMEN๐๐ฝ๐
Cheki huyu mzee alichomfanyia muuzaji wa pharmacy
Mzee kaingia pharmacy,
MZEE: Mambo mwanangu, kuna kitu naomba uonje nitakulipa
MFAMASIA: Kitu gani?โฆ.Mzee akatoa kichupa na kijiko akaweka โฆmajimaji yaliyomo kwenye
kichupa kwenye kijiko na kumwambia mfamasia aonje, mfamasia akatia yale maji mdomoni na kuyazungusha zungusha mdomoni akionja;
MZEE: Nipe jibu, ina utamu wa sukari au chumvi au pilipili?
MFAMASIA: Kama chumvichumvi
MZEE: Hakuna sukari
MFAMASIA: Sukari hakuna kabisa
MZEE: Loh asante chukua hii alfu tano nashukuru sana, dokta alinambia nipime mkojo wangu kama nina kisukari, kumbe sina asante bwana mdogo
Huyu jamaa amekomeshwa, majambazi ni shida!
CHEKA KIDOGO
Majambaz waliliteka gar moja lililokua limeshehen abiria
Baada ya abiria kusachiwa na majambaz hao na kukutwa hawana pesa, majambaz wakasema kila m2 atapigwa viboko (bakora) kutokana na namba ya shati alilovaa
Aliyekua hana namba atasalimika
Kaz ikaanza, jamaa alievaa jez ya ROONEY wa Man U akapigwa fimbo 10, mwengine alievaa nguo ya 50cent akapigwa 50, n.k, sasa kwa pemben kulikua na jamaa analia sn yaani kila akijiangalia, kumbe alikua amevaa fulana limeandikwa LOWASA 2015 duuuh! Unajua kilichotokea ngoja niweke cm chaji kwanza.
Angalia kilichonikuta nilipoenda kwa mganga
Usije ukaenda kwa mganga, mwenzako yamenikuta, yani masharti niliyopewa, acha tu,
yalikua hivi:-
1.Jasho la nyoka.
2.Manyoya ya mende.
3.Sisimizi Shoga.
4.Mbwa mjane.
5.Kuku aliye single.
6.Samaki mwenye miaka miwili bila kuoga
7.Mti wenye ujauzito.
8.Mbavu za Nzi.
9.Nywele za Kiroboto.
10.Mwanya wa Mbu.
Duuh..!! mwanangu kwa hali hii mbona itakula kwako.
Wengine wanasemaga
IGA UFE! Rizik anagawa Mungu tu shetan simuelew!
Kama simu yako ina wifi
Kama simu yako ina Wi-fi ujue uko na mke wa mtuย ๐๐๐๐๐๐๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ
Kwa nini watu hawapendi hesabu!! Sababu hii hapa!
Sababu ni hii
AL-SHABAB
AL-QAEDA
Kwenye MATHEMATICS pia kuna kundi linaitwa
“AL-GEBRA”
๐๐๐๐
๐ถ๐ป๐ถ๐ป๐ถ๐ป๐ถ๐ป๐ถ๐ป๐ถ๐ป
Kumbe ndo maana wengine hawapendi hesabu coz kuna element za ugaidi
Muda ambao unaweza kumzoea dingi
Muda pekee ambao unaweza kumzoea DINGI ni pale unapomfundisha kutumia SMARTPHONEโฆ.
Wanakuwaga wapole sana aisee unaweza hata kumuagiza maji ya kunywa akakuleteaโฆ.
๐๐๐๐๐๐๐
Nimeitoa sehemu
Ifโฆ
99 is: Ninety nine,
88 is: Eighty eight,
77 is: Seventy seven,
66 is: Sixty six,
55 is: Fifty five,
44 is: Forty four,
33 is: Thirty three,
22 is: Twenty two,
Why 11 not Onety one?
Wazungu msitufanye Vilazaโฆ.!! ๐ ๐ ๐ ๐
๐ ๐ ๐ ๐ ๐ ๐
Mungu anawaona
Hii sasa kali kweli kweli!!
MCHUNGAJI alitangaza kila mwanaume aliye na mke atoe sadaka kulingana na uzuri wa mke wakeโฆbac watu wakaanza kutoa 50,000/= 30,000/= na 20,000/=.
Kuna jamaa akatoa 500/=.
MCHUNGAJI akamuita ofisin akamuuliza.
MCHUNGAJI:Ina maana mkeo siyo mzuri?. Jamaa akajibu: Ukimuona utanirudishia na chenji.
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Kifahamu Kidada kimbea kilichofukuzwa kazi
Unafahamu?
Kile kidada kimbea kinachosemaga salio lako halitoshi kimefukuzwa kazi saivi kupiga simu ni bure mjulishe na mwenzako
๐ฒ ๐ฒ
Nani Mkali Hapa kati ya DEMU na MSHIKAJI?
“MAENEO FLANI ya KISHUA”
-Mshikaji kamwona demu mkali
anakatiza kitaa akamkubali akaamua
amfuate amtemee cheche
MSHIKAJI- mambo dada?
DEMU- pouwa
MSHIKAJI-
umependezaa!!!
DEMU- asante.
MSHIKAJI- unaweza ukanisaidia
namba
yako ya simuโฆโฆ..
maana duh
nmekukubali
kinyama.
Demu baada ya kuambiwa vile
akazama kwenye pochi lake akatoa
noti ya
sh.10000 akaandika namba yake
kwenye
noti akampa mshikaji.
Mshikaji kapokea ile noti kachana
sehem
iliyoandikwa namba halafu
kamrudishia
Demu noti yake..!!!
NANI ANA DHARAU
NA NANI JEURI..
DEMU AU MSHIKAJI??!
Mabinti wengine kwa kupenda hela! cheki huyu anachokifanya
Phone call
gal: hellow
Boy: sweety mambo vipi?
Girl: poa
Boy: utakuwa free weekend? nilikuwa nataka uje nyumbani
Girl: oh sorry ctoweza kuja sababu kuna haruc ya aunt yangu
Boy: kama ni hivyo sawa nilikuwa nataka nikufanyie sapraiz nimekununulia BLACKBERRY.
Girl: oh ucjal ntakuja na hata ntalala huko huko
Boy: na haruc je?
Girl: nilikuwa nakutania
Boy: hata mi nilikuwa nakutania
Hapo sasa!! Ni shida!!
Umeshawahi saidiwa homework na mzazi halafu unapata zero?
Hapo ndio unajua shida siyo wewe
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Madhara ya kwenda baa na mke ndo kama haya
Jamaa alienda Bar na mke wake wa ndoa wakakaa kwenye viti, wakati wanasubiri vinywaji akapita binti mmoja anayejiuza akamsogelea yule mke wa jamaa
akamnong’oneza:- “AKULIPE KABISA KABLA HUJALALA NAYE, NI MGUMU KULIPA HUYOO!!.
HALAFU HUWA HATUMII KONDOMUโฆ”
Unajua ni nini kilitokea?
Huyu mke kwa kupenda hela! Cheki anachomwambia mume wake
Jamaa karudi toka kazini mpole na hana furaha!
MKE; Vipi leo mbona mpole?
MUME; Ofisi yetu imeungua na watu wote waliokuwemo wamekufa.
MKE; Ilikuaje wewe ukapona?
MUME; Nilikua chooni jirani na ofisi najisaidia.
MKE; Loh maskini, familia zao itakuaje?
MUME; Watalipwa million 100 kila mfiwa.
MKE; KWA HASIRA, Ona sasa na wewe kunya kunya kwako umetukosesha mihela.. Ungeenda kunya akhera.
Haya ndiyo madhara ya kutowapeleka watoto kanisani โช
MTOTO aliibiwa yeboyebo KANISANI akawa analia sana kwa uchungu mpaka MCHUNGAJI akamwambia usilie mwachie MUNGU. MTOTO akajibu Mungu hazimtoshi zile yebo ni ndogo! Usicheke,
Huu ni Mtihani Tuwapeleke Watoto KANISANI Wamjue MUNGU.
Huku ndiko kuumbuka bila chuki
Umeenda kutembea ukweni kwako baada ya chakula chausiku unapewa chumba chakulala inapofika usiku unatakakutoka kwenda kujisaidi kwasababu taa zimezimwa unapamia vyombo vya chakula sebleni kipindi unajalibu kupapasa uviweke sawa mala taa inawashwa na mama mkwe anaona umeshika vyombo anakwambia, baba kama ukushiba ungesema
Recent Comments