Visa Vya Wanawake Na Wanaume

Mke alichomfanyia mme wake kabla ya kwenda safari, Chezea mawaifu walokole wewe!

JAMAA alimuaga mke wake mlokole kuwa anaenda semina ya siku tatu, kumbe anakwenda kwa bi mdogo.

Mke akamwambia mumewe; “Tupige magoti tusali”,

Wakapiga magoti…:
MKE: Eee baba msaidie mume wangu afike salama safari yake.
MUME: Emen…

MKE: Mpe nguvu katika yote atakayoyafanya huko.
MUME: Emen…

MKE: Akitaka kufanya uasherati ashindwe.
MUME: Kimya…

MKE: Akifanya uasherati apatwe na janga baya kwa uwezo wako bwana.
MUME: …….!!

MKE: Yaani akifanya uasherati afie hukohuko kwa mateso makali.
MUME: Maombi gani sasa hayo!!?. Haya basi siendi semina ufurahi wewe.

Chezea mawaifu walokole wewe!

Angalia sababu ya mke Mtarajiwa kuzimia kabla ya harusi

*Jihadharini* na wachapaji wa kadi za harusi. Hakikisha unasoma maandishi yaliyochapwa kabla ya kadi kuchapwa na kusambazwa!

Mchapaji aliombwa aweke 1 Yohana 4:18 katika kadi ya harusi lakini mchapaji kwa makosa aliweka Yohana 4:18.

1 Yohana 4:18 panasema, “Katika pendo hakuna hofu, lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu…”

Lakini Yohana 4:18 tunasoma, “Kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako.”

🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃😂😂😂😂_MKE MTARAJIWA AKAZIMIA HAPA, TUNAMPEPEA_

Mkalimani alivyoharibu ibada ya leo

Leo nikaamua niingie misa ya asubuhi kwenye kanisa moja la kilokole kulikua na ugeni wa mchungaji kutoka Bulgaria, Mahubiri yameanza saa 1 asubuhi hali ikawa kama hivi:

MCHUNGAJI: My name is Pastor Livingstone
MKALIMANi: Kwa jina naitwa mchungaji Jiwe linaloishi
MCHUNGAJI: We thank God for All goals we set by our hands
MKALIMANI: Tunamshukuru Mungu kwa Magoli yote tuliyoweka kwa Mkono

Hivi navyoongea kanisa halina viti waumini wote tumekimbia nje naona Mkalimani amebaki na kiatu cha kushoto tu.
Sunday joke

Mtoto ni wa baba au wa mama? Angalia hoja za baba na mama kila mmoja anadai ni wake

Mtoto ni wa baba au wa mama?

Mume alimpa mkewe talaka wakaenda mahakamani ili hakimu aamue nani akae na mtoto.

MME: Akasimama akauliza hivi: Mheshimiwa hakimu hivi nikichukua ATM card nikaingiza kwenye mashine ikatoa pesa, sasa pesa zitakuwa ni za ATM au zakwangu?

MKE: Akasimama na kusema: Mheshimiwa hakimu hivi ukimwaga mbegu ktk shamba la mtu mti ukiota utakuwa wa kwako au wa mwenye shamba?.

Hebu tumsaidie hakimu aamue kesi hii…

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About