Visa Vya Mwaka Mpya

Hali za ndoa

Kuna kijana alikua anajua kuwa mke wake
anatoka nje ya ndoa basi akamwuliza mke,
mkewe akakataa, akamwambia baba yake
akaambiwa na babaake tulia mwanangu ndoa
zina mengi! akawa kila siku analalamika kwa
babaake, mwisho babaake akamwambia basi
ntakusaidia. Itabidi ujifanye unaumwa sana hoi
hujiwez halafu nitakuonyesha jawabu!

Basi kijana akajifanya anaumwa mzee akaitisha
kikao cha ndugu wote pande 2,
Mzee akaanza kueleza jaman kijana wetu
anaumwa amepata ugonjwa wa utata hospital
zote umeshindikana hivyo tumeenda kwa mganga
wa jadi amenipa dawa na ina masharti, inatakiwa
atakaye iandaa hii dawa awe mwanamke mwenye
ndoa ambaye hajawah kutoka nje ya ndoa tangu
alipoolewa ndo kijana wetu atapona!
Kama ametoka nje ya ndoa asiandae dawa hii
kwa sababu tukimpa kjana wetu watakufa wote!
Je kina mama nani ataandaa? Walitoka nje
wamama mmoja mmoja hadi mkewe na mamake
mzazi wakatoka, akafata mama ake kijana,
mashangazi na dada zake, mwisho wakabakia
wanaume peke yao! Mzee akamwambia
mwanangu umeona hali za ndoa zilivyo?
Acha kujisumbua tulia na mkeo nadhani
umejionea hali halisi.
Cha zaidi omba Mungu sana juu ya ndoa yako!
Kijana akazimia!
SOMA TENA KISHA MTUMIE NA MWENZIO.

Alichofanya mke baada ya mme wake kupenda kumchunga sana

Alifanya hivi;
Siku ya kwanza

MUME: Halooo vipi mke wangu salama weye?.
MKE: Salama tu
MUME: Uko wapi?
MKE: Jamani si niko nyumbani
MUME: Mhh kama kweli uko nyumbani washa blender nisikie…..mke­ akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Okay haya mi natoka kazini naja

Siku ya pili
MUME: Vipi mko salama huko?
MKE: Tupo kama ulivyotuacha
MUME: kwani uko wapi?
MKE: Niko nyumbani napika
MUME: Washa brender kama kweli uko nyumbani
Mke akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Poa ntarudi baada ya masaa mawili

Siku sita baadae mume akaamua kurudi bila kumtaarifu mkewe alipofika home kamkuta mdada wa kazi yuko peke yake.
MUME: We mama yako yuko wapi?
MDADA: Sijui ameondoka na blender toka asubuhi

Cheki nilichomfanyia boss wangu

Bosi wangu karudi safari yake kutoka serengeti..! Si akanitumia picha, lakini ilikuwa network yenyewe tabu.. kwahio picha haikufunguka na kwa vile niliona itachelewa kufunguka na ataona sikumjibu basi nami..

Nikampelekea msg nikamuandikia umependeza saana bosi mashaallah…!!
sasa baada tu ya kumfika msg.. na huku picha ikafunguka kumbe picha ya Sokwe..!!
Basi Kaniambia kesho niende ofsini kwake kuna barua yangu..
Nahisi hyo barua ina pesa, hapa cjalala, nmekosa usingizi kabisa,nawaza ninunulie nn hyo pesa.Na kesho asubuhi sa 12 asubuhi atanikuta ofisini kwake naisubiri barua, sipendagi ujinga mimi.

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About