Visa Vya Kuwaadisia

Hii mitoto mingine mijinga, cheki alichokifanya huyu

Nimeamka asubuhi nikiwa na elfu 1 tu mfukoni, nikamtuma mtoto wa jirani akaninunulie maandazi nipate kunywa chai. Baada ya muda namuona anarudi huku analamba askrimu ya AZAM kama Simba vile. Nikamuuliza maandazi yako wapi? Akanijibu eti wakati anafika yanapouzwa maandazi akagundua kuwa kapoteza hela yangu, hivyo akaanza kurudi, ila bahati nzuri wakati anarudi ili kuja kunitaarifu kuhusu kupotea kwa hela yangu, njiani akaokota elfu 1 ambayo kuna mtu alipoteza ndio akaamua kununua askrimu….kwa sasa niko polisi na mtoto yuko dispensari na mamake😀😀😀😀😀😀😀

Mlevi kazua tafrani, angalia alichokifanya hapa

MLEVI mmoja aliingia baa akavuta kiti na kukaa mhudumu akatokea kumsikiliza.
MHUDUMU: Nikusaidie nini?
MLEVI: Eeh! nipe bia ya baridi kisaha wasikilize wote waliokaa hapa, wape bia na wao maana sipendi kunywa pombe wengine wananiangalia
Akaja mhudumu wa jikoni “nikusaidie nini?”

MLEVI: Niletee supu kisha wasikilize wote waliokaa hapa na wao wape supu sipendi kunywa supu watu wananiangalia
Safari hii watu wakapiga makofi
Baadae akamuita mhudumu
MLEVI: Niandikie bili zangu kisha waandikie wote bili zao sipendi kulipa huku watu wananiangalia

Wale wateja wakamvaa na kumshushia kichapo… teh teh teh teh teh hii kali hakuna cha bure mjini hahahaha na jasho la mtu haliliwi wandugu

Jamaa alikuwa na tabia ya kutembea na binamu yake cheki kilichomkuta

Jamaa alikuwa na tabia ya kutembea na binamu yake….

Alikuwa anasubiri mjomba na mkewe walale tu halafu ananyata mdogo mdogo mpaka chumbani kwa binamu yake.

Siku moja umeme ulikuwa umekatika ikabidi aamue kuvua nguo kabisachumbani kwake….

Akanyata taratibua akafungua mlango akazama chumbani kwa mjomba ake bila kujua, ghafla umeme ukarudi…

MJOMBA; we mshenzi umefata nini chumbani kwangu tena uko uchi

JAMAA; nimekuja kukuaga kesho naondoka

MJOMBA; ndo uje uchi?

JAMAA; ndio kwasababu nimeshapaki kila kitu kwenye begi

😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂

Hii ndiyo sababu ya kumfanya huyu jamaa kujiita fara

MZEE:”sasa huyu mgeni sijui alale wap?”
MKE:”saa hizi ni usiku akalale na Bebi.”
jamaa akaona huyo Bebi pengne mtoto anakojoa kitandani au akalia asije msumbua usiku

JAMAA:”msipate tabu mi ntalala hapa kwenye kochi” akalala
asubh wanakunywa chai akaibuka mrembo,jamaa akapigwa bumbuwazi almanusra ajimwagie chai.
BINTI:”Naitwa BEBI,we unaitwa nani?”
Jamaa akasema mimi naitwa Fara…..!

Majibu ya mkato ya kuchekesha Kutoka Kenya

Njeri: Roysambu ni ngapi?
Makanga: Roysambu ni moja tu. Pengine kama Chinese wamejenga ingine.

Odhis: Hii gari haina watu bana.
Makanga: Kwani hao wawili wenye wamekaa hapo ndani ni ng’ombe?

Man: Wekeni nyimbo za Yesu tafadhali.
Makanga: Yesu bado hajatoa album. Akitoa tutaeka.

Mwikali: Excuse me conda…gari za Mwingi zinapandiwa wapi?
Makanga: Ziliacha kupandwa juu hazimei.

Man: Kwani mwisho wa gari ni wapi?
Makanga: Mwisho ni hapo penye number plate iko.

Karis: Ruaka ni how much?
Makanga: Sijaskia Ruaka ikiuzwa. But nikiskia nitakwambia.

Passenger: Shukisha dere.
Makanga: Tukishukisha dere utaendesha gari?

Johnny: Maze, hii gari iko na joto sana.
Makanga: Basi shuka upande fridge

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About