Visa Vya Kukuparaha

Ndege ya Tanzania

Kuna maprofesa 40 walipanda AIR TANZANIA ili wasafari. Kabla ndege haijaanza kuondoka, Lilipita tangazo kama ifuatavyo:

Ndugu wasafiri wote, ndege unayotarajia kusafiri nayo imetengenezwa na wanafunzi wa Kitanzania.
Baada ya tangazo maprofesa wote waliteremka isipokuwa mmoja alibaki kwenye kiti chake
Walipomuuliza ni kwanini hakuondoka akajibu kwa haraka na furaha kuwa:
Kama ndege hii imetengenezwa na watanzania, hata kuwaka haitawaka!

Jinsi mzunguko wa elimu ulivyo

01.๐Ÿ‘‰ Wale wanafunzi walioongoza
Mashuleni, wanaenda kwenye
Engineering na Medical school.

02.๐Ÿ‘‰ Wale waliokuwa wa pili, wanachukua MBA na LLB na kuja kuwa Mameneja wa
wanafunzi walioshika nafasi ya kwanza.

03.๐Ÿ‘‰ Wale waliokuwa wa tatu, wanageukia
Siasa na kuwaongoza wote hapo juu.
Yaani wa kwanza na wa pili.

04.๐Ÿ‘‰ Wale waliofeli, wanaenda Jeshi, hawa wakigoma, basi hao wa juu
wote hawana raha.

05.๐Ÿ‘‰ Wale waliopata Zero na waliokataa
shule wanakuwa waganga wa kienyeji,
wote hapo juu watamtafuta huyu, pale
mambo yao yanapokwenda kombo. Tuache kudharauliana, kila mtu ni boss akiwa kwenye nafasi yake.
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‰๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿƒ๐Ÿฟ๐Ÿƒ๐Ÿฟ๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜œ

Angalia huyu Jamaa alivyomuweza huyu mrembo

Nipo kwenye daladala siti ya nyuma kabisa nimekaa na mrembo mzurii.sasa nikawa namtongoza kwa sauti ya chini sana watu wengine wasiskie,akawa hanijibu kitu,mala gafra akapayuka kwanguvu na kwa sauti ya juu iliyomshtua kila mtu.โ€‹
โ€‹”Nimesema stakii,stakii tena unikome”โ€‹๐Ÿ˜ณ๐Ÿ˜ณ

โ€‹Nami nikamjibu kwa sauti ya juu vile vileโ€‹
โ€‹”Kama umejamba nisikwambie bhanaa,kwani ww nani?”โ€‹โ˜น

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
โ€‹โ€‹MIMI SIO MTU WA MCHEZO MCHEZOโ€‹
Sipendag ujuinga mim

Jinsi ya Kubana matumizi X-mass

Badala yakupika PILAU tutapika TAMBI kwenye Xmas maana tutakua tumeokoa sh.15,000/= Vitunguu swaumu 2000, Vitunguu maji 1000, hiliki 1000, Magome 1000, Michele wa 2000, Soda 3000, Nyama 5000 . Fedha hizi zitatumika kununua mfuko wa cement ili tuanze kujaza kibubu cha ujenzi wa nyumba badala ya kupanga. Karibuni saana maji ya kunywa tumechemsha ndoo nzima.

๐ŸŽ€โœจMarry Xmas & Happy new year.โœจ๐ŸŽ€

Kilichotokea baada ya kuzamia sherehe

Pale unapozamia kwenye Dinner Party ya Jumuiya Fulani, sasa Lengo la Jumuiya hiyo ni kupata Fedha za kutunisha Mfuko wa Jumuiyaโ€ฆsasa unakakaa mbele kabisa ili Muda wa Msosi usichelewe na kukuta kwenye Buffee yamebaki maharage!

MC : “Papai zuri kabisa kutoka Newala, Papai Mwendokasi, hili ni Shilingi laki 1..jamani Papai,nipeni ofa!”

MOSHA : “Laki 3 hapaaa!”

“Jamani laki 3 pale kwa Mosha, Papai linaondoka jamani, papai hili ni self contained kabisaโ€ฆ.papai jamani”

KIBOLIBO: “Milioni 1 hapaaa”

“Jamani Mambo yanazidi kunoga hapa!โ€ฆBenedict Kibolibo anataka papai kwa milioni 1 jamani, linaondoka papai!”

RWEYEMAMU : “nitanunua Papai hilo kwa Milioni 5”

Haya sasa jamani Rweyemamu ametoa ofa ya Milioni 5 Jamani, nani mweingineee?”

Kimyaaaโ€ฆ

Haya jamani Papai kama hakuna Ofa basi Papai linakwenda kwa Rweyemamu!โ€ฆโ€ฆ..haya sasa Kuna Kuku hapa Jogoo kabisa, bei yake ni laki 6 jamani Jogoo twitter huyu!”

WEWE “Milioni Mojaaa!”( hapa umejiwahi wa kwanza na wewe uonekane upo huku ukijua kabisa Wakina Mosha na Rweyemamu lazima watampandia Dau Jogoo, tena dau kubwa”

MC: ee sasa Kumekucha Jamani, Kabasele anamtaka Jogoo kwa Milioni 1 jamani!โ€ฆ.ofa nyingineeee!”

Kimyaaaโ€ฆ

Jamani Jogoo anakwenda kwa Kabasele jamani!โ€ฆofa nyinginee!

Kimyaaaโ€ฆ.

Kimyaaaโ€ฆ.

๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜โ€ฆhapa sasa ndio mfukoni kuna Buku jero,..huko kwengineko NMB nill balanceโ€ฆsasa unageuza mimacho kumtazama Mosha kama atapanda dau kwa jogoo๐Ÿ‘€(mama wee Mosha anachezea Simu!)โ€ฆ..unamtazama Rweyemamu (teh anatafuna Kuku)โ€ฆ..mama weee๐Ÿ˜

MC: Haya jamani kama hakuna Mwingine basi zoezi letu liishie hapa na limekwenda kwa Mafanikio, Mpatieni Kabasele Jogoo wake!

Hapa sasa unapokea jogoo wako wa MILIONI kwa Tabasamu la Maitiโ€ฆ.kule nyumbani Jogoo wako Mkubwa unauza elfu 20 lakini sasa haka kajogoo kapya Mkononi kanakuwa kazito utadhani umembeba John Cena๐Ÿ‘€โ€ฆMama weee hapa sasa vidari ulivyotafuna unaviona kama vimerudi kwenye Ulimiโ€ฆ.Chicken wings zinataka kutokea Masikioniโ€ฆ..Uuuuwiiiii,๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜

Na hapa sasa kabla Dinner haijaisha ndipo unapojikuta Umebuni Cocktail ya Sparetta na Tomato๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜‚.
chiel wie okee

Kilichotokea baada ya kichaa kumfumania mke wake na mwanamme mwingine

Jay akaruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospital ya Vichaa, akapakiwa ktk ambulance hadi karibu na nyumbani kwake, akaulizwa unapakumbuka? akajibu ndio nyumba yangu ileee, mara wakatoka watoto wawili wamevaa uniform akasema watoto wangu walee wanakwenda shule.. akatoka mwanamke akasema na mke wangu yulee, ghafla akatoka mwanaume Jay akasema na mimi yule naenda kazini. hivi Jay kweli kapona?

Huyu mke kwa kupenda hela! Cheki anachomwambia mume wake

Jamaa karudi toka kazini mpole na hana furaha!
MKE; Vipi leo mbona mpole?
MUME; Ofisi yetu imeungua na watu wote waliokuwemo wamekufa.
MKE; Ilikuaje wewe ukapona?
MUME; Nilikua chooni jirani na ofisi najisaidia.
MKE; Loh maskini, familia zao itakuaje?
MUME; Watalipwa million 100 kila mfiwa.
MKE; KWA HASIRA, Ona sasa na wewe kunya kunya kwako umetukosesha mihela.. Ungeenda kunya akhera.

Duh, Ukisikia ngoma droo ndio hii

Ni noma!

Baada ya Talaka mke kamtumia mume meseji:- “Nasikitika kukujulisha kuwa binti uliyemlea kwa miaka 20 sio mtoto wako” Mume akamjibu:- “Duh! Nashukuru Mungu kwani nilikuwa nikiumia rohoni kila siku kwamba nazini na binti yangu” ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ

Huyu mchungaji ni noma, cheki alichomwambia pedeshe

Mchungaji kamfuata pedeshe moja maarufu kwa
kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki;
MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za
kujenga kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa
mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na Mungu
atakubariki zaidi

PEDESHE: Samahani Mchungaji haitakuwa vizuri
mimi kuchangia kanisa, fedha zangu ni haramu,
huwa nazipata kwa utapeli na kuuza madawa ya
kulevya.
MCHUNGAJI: Yote ni heri, pesa yako tutatumia
kwa kujenga eneo la choo we toa tu!!!

Safari ni safari

FUNDISHO : SAFARI NI SAFARI

Maisha ni ya ajabu sana, wakati mwingine maisha ni mazuri na mwingine ni mabaya, katika maisha yetu tumeshapitia safari nyingi sana na za aina mbalimbali kwa nyakati mbalimbali. Lakin kiukweli kila safari ni safari tuu.

Japokua kila safari ina changamoto zake lakini mwisho wake ni ule ule , kila safari ina uzuri na upekee wake.

Vile vile kila safari ina ubaya wake, kwa mfano kila safari ina gharama yake kulingana na upekee wake.

Usiwe na wasiwasi na mashaka na aina ya safari ulionayo, jipe moyo utaimaliza na kupata ulichokitarajia. Haya ndio maisha na wote tunatakiwa tuyafurahie.

Ingawa kila mtu ana safari yake bado wote tunatakiwa tufurahie pamoja kwa safari tuliyo nayo. Hata Uwe Na safar ya aina gani wewe furahi tuu. Hii ni kwa sababu safari mwisho wake ni mmoja kwa wote burudani ni ile ile

Safari๐Ÿบ ni safari ๐Ÿบhata kama ni ya chupa au ya kopo mwisho wake ๐Ÿ’ค๐Ÿ’ค

๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Ulijua ni nn??

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About