Visa Vya Kukuburudisha
Angalia hawa vichaa walichokifanya, Vichaa bwana, ni noma!
Vichaa walipanga kutoroka, wakakubaliana wamnyonge mlinzi watoroke!
Walipofika getini wakakuta geti lipo wazi na hakuna mlinzi, wakasema “Turudi mipango yote imevurugikaโฆ
Kilichotokea baada ya kichaa kumfumania mke wake na mwanamme mwingine
Jay akaruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospital ya Vichaa, akapakiwa ktk ambulance hadi karibu na nyumbani kwake, akaulizwa unapakumbuka? akajibu ndio nyumba yangu ileee, mara wakatoka watoto wawili wamevaa uniform akasema watoto wangu walee wanakwenda shule.. akatoka mwanamke akasema na mke wangu yulee, ghafla akatoka mwanaume Jay akasema na mimi yule naenda kazini. hivi Jay kweli kapona?
Mchaga aliyemshangaza Mungu
Mchungaji anawaambia waumini: Fanya jambo moja la kumshangaza Munguโฆ
Dakika mbili nyingi Mchaga akakimbia na kapu la sadakaย
๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Angalia alichokifanya huyu sharobaro kanisani
Huu usharobaro mwingine uchizi. Jamaa kamzimia demu kanisani,
mara ukafika mda wa kutoa sadaka, eti jamaa akamwambia ”dont worry bby” ntakulipia!!
Kilichotokea baada ya jambazi kuvamia kanisa
Jambazi mmoja aliingia kanisani na bunduki akapiga risasi juu ya bati akasema “asiyempenda YESU atoke nje” wakatoka wote ispokuwa Mchungaji na Wazee wawili.
Jambazi likamwambia Mchungaji “unaweza kuendelea na ibada, nilikuwa nakuondolea wanafiki”, Mchungaji akasema “ungewaacha kwanza nichukue sadakaโฆ!
Angalia kile kitabia cha kufuta namba kwenye simu kilivyomponza huyu jamaa
Jana nilijipa kazi ya kufuta vitu visivyo na umuhimu kwenye sm yangu. Katika futa futa si nimefuta namba ya bosi wangu. Halafu boss mwenyew wa kike. Mida ya Saa mbili usiku nikawa chumbani kwangu. Mara simu รฝรครฑgรน ikawa inaita. Kucheki namba ngeni. Nikapokea baada ya salamu. Meโnani mwenzangu?? Bossโwe hunijui me ?? Meโusinijbu swali kwa swali Nita kublacklist sasa hiv. Sipendagi ujinga.. Kwa sasa nazurura tu mtaani na roba langu La machupa
Kingereza sio mchezo, angalia huyu anavyojichanganya
Jamaa fulani alikuwa ame2lia beach mzungu akapita akamuliza “Are u relax ? Jamaa akawa hamuelewi akamjibu No! Mzungu mwengine akapita akamuliza vilevile akajibu No!
Akaona hapa anasumbuliwa akasogea mbele kidogo ya maji akamuona mzungu mmoja alikuwa ame2lia. Akamuliza “are u relax? Mzungu akajibu yes jamaa akamkata makofi mawili na kumwambia kumbe we ndo relax inuka unatafutwa na wenzakoโฆ..Shenz mkubwa mie nasumbuliwa na wenzako kule we umejikausha!!
Hii ndiyo bongo sasa!!
Hii ndio Bongo
Ilikuwa Ijumaa mida ya saa 10 jioni, mzee mmoja aliingia na kibinti kizuri kwenye yard ya magari mapya.
MZEE: Chagua gari unalotaka mpenziโฆ.kabinti akazunguka yard yote mwisho akachagua Verrosa metallic .
BINTI: Mi naitaka hii
MZEE: Hakuna tatizo kabisaaa, mtoto mzuri kama wewe lazima upate gari uloichagua mwenyewe. Mzee akatoa kitabu cha cheki na kuandika palepale na kumpa mwenye yard
MUUZAJI: Sasa Mzee kwa kuwa umetoa cheki, gari utakuja chukua Jumatatu tukishahakikisha kuwa Account yako ina pesa benki. Naomba namba yako ya simu Mzee
MZEE: Hakuna tatizo (akampa namba). Haya twende zetu sweetie Jumatatu tunakuja wote kuchukua gari lakoโฆ
Siku ya Jumatatu mwenye yard kampigia simu Mzee.
MUUZAJI: We Mzee kavu sana, akaunti yako haina hata senti tano.
MZEE: Hilo nilijua, lakini wiki endi yangu ilikuwa tamu sana.
๐ฆ๐๐ฆ
Angalia haya mazungumzo ya msichana na mvulana, mapenzi ya ajabu haya
Demu: Hny mambo jamani!
Man: Safi nipe habari wangu wa moyo
Demu:Wafanya kazi gani vile wangu?
Man: Ni fundi wa kufunga ATM
Demu: Wow dont tel me i love you myn mwa mwa mwaaaaah
Man: Mbona wafurahia?
Demu: Nami natamani kuja kufanya kazi za kibenki.
Man: Itakua poa sana nami natamani pia
Demu: Hee si umesema wafanya kazi ya kufunga ATM?
Man: Hukunielewa mie ninafunga mashine na za kunulia condom kwenye bar
Demu: nipishe huko
Angalia Kiingereza kilivyoniponza
Shikamoo kingereza..!
Baada ya kufika Kempiski nikaona menu imeandikwa:
Sauteed white corn, rare lucy beans, garnished with rift potatoes & topped with organic unprocessed guacamole!
Price: TSH 44,000/=
Nikaagiza!
Nilipoletewa ndio nagundua kwamba:ย ni makande na parachichiย ..๐ค
hapo ndo unagundua mwalimu wa kiingereza alikuwa sio mtu wa mchezo mchezo๐ค๐จ
Recent Comments