Visa Vya Kukuburudisha

Angalia nilichokifanya Jana kumkomoa x-wangu

Mwenzenu nilikatiwa umeme jana basi leo si nikaamua kwenda kununua luku ya 10,000. Kufika njiani nikatamani fursana nikaingia kijisupermarket mara sindo nakutana na ex wangu! Mshenzi yule kaniona mimi sijui alikua na mpango wa kununua vocha ya jero eti kabadili kanunua vocha ya buku tano ilimradi nione maisha yake safi tangu tuachane. Mambo ya kijinga spendi kudadeky nimetoa buku kumi nikanunua mipampers nami nijifanye nimeowa nina mtoto halafu huyoo nikashika njia yangu.

Sasa washkaji zangu tafadhalini mwenye mtoto au shida ya pampers naomba anunue kwangu maana leo nalala tena kiza ๐Ÿ™†โ€โ™‚

Cheki huyu mwanamke anavyomkomoa mme wake baada ya kumsaliti

MKE: Mbona unanukia pafyumu ya kike?
MUME: Yaa kuna mwanamke tulikuwa tumeminyana ndani ya daladala
MKE: Na lipstiki kwenye shati?
MUME: Tulikumbatiana na wageni toka Zambia walitembelea ofisi yetu
MKE: Na ile kondom iliyotumika kwenye mfuko wa suruali?
MUME: Bwana ee acha maswali ya kijinga mi nalala nina usingizi
MKE: Lazima niulize mie huwa nahakikisha nimeacha kila kitu hukohuko ndio narudi nyumbani
MUME: Umesema nini wewe?
MKE: Bwana ee acha maswali ya kijinga mi nalala nina usingizi. ๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„

Vituko vinavyoandikwa kwenye daladala

Huwa naenjoy sana kusoma yaliyoandikwa nyuma ya daladala hasa ninapokuwa kwenye foleni. Misemo maarufu
ya kwenye daladala.

1.Yatima hadeki
2.Utamu wa chips mimba
3.Ukitaka kujua ugumu wa kudai kopesha ukweni
4. Usiyempenda kaja
5. Kobe hapimwi joto
6. Acha kazi uone kaz kupata kaz
7. Ukichezea koki utalowa
8. Heshima pesa kipara kovu tu!
9. Mtumbwi hauna saitmira.
9. Silaha pesa bastola mzigo
10. Hata uoge mjini huendi
11. Chezea mshahara usichezee kazi.
12. Ukiona manyoya ujue kishaliwa
13. Ikisimama Panda
14. Pombe pombe tuu kunywea bar mbwebwe
15. Njia ya chooni haioti nyasi
16. Likizo ya maskini ugonjwa
17. When i grow up i want to be a scania
18. Hata bibi alikuwa binti
19. Kisigino hakikai mbele
20. Kama mapenz pesa kaolewe na benki
21. Hata barabara ina matuta lakin huwez panda viazi
22. Mavi hayana miba lakin ukikanyaga lazma uchechemee
23. Paka haishi kwa msela
24. Ukipendwa ujue kuna boya kaachwa
25. NIPO NIPO KWANZA
26. Mchana nzi ucku mbu
27. Ucmshangae funza kukata viuno ndio mwendo wake
28. Kama umelipenda(gari) bonyeza nyota liwe lako
29. Supermarket hawauzi mkaa
30. We nisubiri mi nakungoja.
31. Zetu dagaa kuku tamaa
32. Hata uwe na heshima vipi huwezi kumpokea askari bunduki
H
๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜

Share na wenzako kuongeza siku za kuishi

Wanawake wa leo mbele ya hela. Hii ni hatari

MDADA: Baby nikwambie kitu
MKAKA: Yeah Baby Uko huru nambie
MDADA: nilikua naomba hela babyโ˜บ
MKAKA: WW nae kwa kupenda hela jana tu nmekupa hela Leo unaomba ya nn ๐Ÿ˜–
MDADA: hapana๐Ÿ˜Œ Bby sio hivyo nlikua nataka nikashuhudie tetemeko la ardhi BUKOBA nasikia huko linaonekana vizur .
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Wanawake kumbukeni sio vizuri

Utani wa wahindi, cheka kidogo

Mhindi afaulu mtihani wa Kiswahili

(1) Mfa maji ?โ€ฆโ€ฆโ€ฆโ€ฆโ€ฆโ€ฆ.. Tampa life jacket.
(2) Mwenda pole?โ€ฆโ€ฆโ€ฆโ€ฆ Tachelewa fika.
(3) Usipoziba ufa ?โ€ฆโ€ฆโ€ฆ.. Mizi taona mpaka dani.
(4) Usilolijua ?โ€ฆโ€ฆโ€ฆโ€ฆโ€ฆโ€ฆ Uliza google.
(5) Mbio za utelezini ?โ€ฆโ€ฆ. Chafua guo yako.
(6) Ukipenda boga ?โ€ฆโ€ฆโ€ฆ Ngoja mezi ya ramzani tapata.
(7) Ukiona vinaelea ?โ€ฆโ€ฆ.. iko nyepesi hiyo.
(8) Maji yakimwagika ?โ€ฆโ€ฆ Mambie dada tapiga deki.
(9) Chelewa chelewa ?โ€ฆโ€ฆโ€ฆ Takosa guo ya sikukuuโ€ฆ
(10) Kila ndege ?โ€ฆโ€ฆโ€ฆโ€ฆ.. โ€ฆHutua Airport
(11) Bandu bandu ?โ€ฆ.. โ€ฆโ€ฆ.Rafiki yake Jecha
(12) Mtaka cha Mvunguni ?โ€ฆ Ondoa tanda
(13) Simba mwenda kimya?โ€ฆ.Kama sio gonjwa basi haina njaa.
(14) Aisifuye mvua ?โ€ฆโ€ฆโ€ฆ. Najua iko Mkulima hiyo
(15) Barabara ndefu ?โ€ฆโ€ฆ.. Ongeza mwendo au tachelewa fika.
(16) Mlanawe hafi nawe ila?โ€ฆ. Takimbia
(17) Asie sikia la mkuu ? โ€ฆโ€ฆ.. Tapeleka jela
(18) Hasira za mkizi ? โ€ฆโ€ฆโ€ฆโ€ฆ..Tatafuna veve
(19) Mchamba wima ?โ€ฆโ€ฆ.. Karibu ya Hurumzi
(20) Akumurikae mchana ?โ€ฆ.Kipofu hiyo
(21) Mficha maradhi ?โ€ฆโ€ฆ.. Taenda Loliondo
(22) Mkataa wingi ? โ€ฆโ€ฆโ€ฆ.Taenda Chadema
(23) Bendera ?โ€ฆโ€ฆโ€ฆโ€ฆโ€ฆ. Kama sio ya CCM, ya CUF
(24) Baniani mbaya ?โ€ฆโ€ฆ. Peleka Bombay Lakini sio HB kweli, naonea tu
(25) Akili nyingi ?โ€ฆโ€ฆโ€ฆ. Tapasi mtihani yote
(26) Penye kuku wengi ? โ€ฆโ€ฆ.. Chija bili tatu ivi, hapana mtu najua.

Askari na yeye kumbe muoga, cheki anachomjibu afande

Askari wametumwa nyumba iliyokuwa kuna ugomvi wakafika wakatakiwa kuripoti kwa njia ya simu juu ya walichokikuta
ASKARI: Mkuu tumekuta mama mwenye nyumba kampiga mumewe chuma cha kichwa na kumuumiza vibaya sanaa

AFANDE: Kha! kisa mkasa mpk akafanya hivyo
ASKARI: Mama mwenye nyumba alikua anapiga deki mumewe akaingia ndani viatu kabla sakafu haijakauka
AFANDE: Sasa mmesha mkamata huyo mwanamke
ASKARI: Bado mkuu
AFANDE: Kha! sasa mnangoja nini
ASKARI: Si tunangoja sakafu ikauke

Angalia huyu baba alichowafanya mtoto wake wa kike na boyfriend wake

BABA OYEEEEEE๐Ÿ’ช๐Ÿ’ช
Soma hiiโ€ฆ

Msichana alikuwa amekaa na baba yake kibarazani, mara akamuona MVULANA friend wake akija, yule mvulana alipokaribia tu, yule msichana akamwambia hivi:-

MSICHANA: Umekuja kuchukua kile kitabu chako, kinachoitwa “DADDY IS AT HOME?” by Ngozi Okafor

MVULANA: Hapana!, Nimekuja kuazima kitabu cha maombi kama kinaitwa “WHERE SHOULD I WAIT FOR YOU?” by Ngลฉgฤฉ wa Thiong’o

MSICHANA: Aaah! Hicho sina ila ninacho kimoja kinaitwa “UNDER THE MANGO TREE” by Chimamanda Adichie

MVULANA: Ooh! Vizuri, Basi usisahau kuja nacho kesho kitabu cha Okot p’Bitek kile kinachoitwa “CALL ME IN 5 MINUTES BEFORE” Utakapokuja shule.

MSICHANA: Usijali, tena nina kitabu kipya kinaitwa “I WON’T LET YOU DOWN” by Chinua Achebe

Baba mtu akawatazama kisha akasema

BABA: Vitabu vyote hivyo, mbona vingi sana, atavisoma vyote kweli

MSICHANA: Ndio Daddy, huyu mvulana yupo smart sana na ana akili atavisoma vyote hivyo!

BABA: Sawa! Usisahau kumpatia na kile ambacho nimekiweka pale juu ya meza, kinaitwa “I AM NOT STUPID, I UNDERSTOOD EVERYTHING YOU’VE BEEN SAYING” by Shakespeare!

Na kuna kingine nimekiweka juu ya kabati la vyombo, kinaitwa “IF YOU GET PREGNANT PREPARE TO GET MARRIED” by Wole Soyinka.

Unakumbuka hizi enzi za utoto?

Kitambo tukiwa watoto ulikuwa unaitwa uje ule kwa lugha tofauti kulingana na chakula kilichopikwa siku na muda husika

1. UGALI NA KUNDE
Mwitaji : ๐Ÿ—ฃJoniiiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Uje ukule

2. UGALI NA SAMAKI
Mwitaji: ๐Ÿ—ฃ we Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Unaitwa na Mama

3. WALI NA NYAMA/KUKU
Mwitaji: ๐Ÿ—ฃ Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Shauri yako!
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Ujanja alioutumia msichana wa kazi ili apandishiwe mshahara na mama mwenye nyumba

Msichana wa kazi alitaka mama mwenye nyumba ampandishie mshaharaโ€ฆ.. Mama mwenye nyumba akamwambia msichana ampe sababu tatu za kutaka kupandishiwa mshahara.

Msichana: Napika vizuri kuliko wewe.

Mama: Nani kakuambia?
Msichana: Baba kaniambia.

Mama: ok. Sababu ya pili?
Msichana: Napasi nguo vizuri kuliko wewe

Mama: Nani kakuambia na hili?

Msichana: Baba pia kaniambia

Mama: ok, na sababu ya tatu?

Msichana: Najitahidi kitandani kuliko wewe.

(Hapa mama kaonekana kutaka kujua zaidi na akawa tayari kujiandaa kumrukia akate kichwa cha binti mara moja)

Mama: Mume wangu kakuambia na hili pia?

Msichana: Hapana ni Shamba boy kaniambia mimi najitahidi kitandani kuliko wewe.

Mama: Tafadhali punguza sauti baba yako asisikie. Nitakupandishia mshahara wako mara tatuโ€ฆโ€ฆ.

Angalia sababu ya mke Mtarajiwa kuzimia kabla ya harusi

*Jihadharini* na wachapaji wa kadi za harusi. Hakikisha unasoma maandishi yaliyochapwa kabla ya kadi kuchapwa na kusambazwa!

Mchapaji aliombwa aweke 1 Yohana 4:18 katika kadi ya harusi lakini mchapaji kwa makosa aliweka Yohana 4:18.

1 Yohana 4:18 panasema, “Katika pendo hakuna hofu, lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofuโ€ฆ”

Lakini Yohana 4:18 tunasoma, “Kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako.”

๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚_MKE MTARAJIWA AKAZIMIA HAPA, TUNAMPEPEA_

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About