Visa Vya Katikati Ya Wiki
Cheki huyu dingi alivyo mnoko
Unamtumia baba ako meseji ukiwa shule “Baba naomba unitumie 100,000 ya pckt mny” anakuuliza “pckt mny” ndo nini? Unamjibu ni kifupi cha “pocket money” af ankutumia 10,000, unamuuliza hiyo hela ni ya nini? Anakwambia ni kifupi cha 100,000.
Hapo ndo unatamani kuchoma shule ufe.
Cha kufanya msichana akikukimbia halafu atake kukurudia
……… Kama msichana atakutupa kwa sababu huna pesa, na baadaye unapopata pesa akarudi tena kuomba msamaha… Ndugu yangu….. Msamehe…. Mpe ahadi ya ndoa, mwambie utamuoa…. iambie familia yake unataka kufanya ukarabati wa nyumba yao…… Ondoa paa lote la nyumba yao halafu TOWEKA…..
😂……… 😂…….. 😂
Misemo 10 bora ya kuchekesha itakayokuacha mdomo wazi
1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.
2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.
3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?
4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.
5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.
6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.
7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.
8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.
9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.
10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi
kufunika sufuria.
Mambao ya saluni ni shida, cheki kilichotokea kwa huyu
DADA alienda Salon wakati anasukwa akaingia
MKAKA mtanashati,
DADA akaamua kujaribu bahati yake.
DADA:Mambo? KAKA:Poa.
DADA:Mimi na wewe tunaweza kuongea baade?
KAKA:Kuhusu nini?
DADA:Nimekupenda nataka nikutoe out.
KAKA:Sawa ila nitamwambia nini
MKE wangu?
DADA:Aah ilo sio tatizo mdanganye tu,mwambie unakwenda kumtembelea rafiki yako hospitalini.
KAKA:Mwambie mwenyewe huyo hapo anayekusuka.
Unajua nn kiliendelea?
Angalia huyu jamaa anachomwambia mwizi baada ya kumuibia simu yake
Foleni ndeeeeefu jamaa yupo kwenye daladala anaenda kazini kaona heri amuandikie boss wake msg kumtaarifu kuwa atachelewa ile anatakubofya SEND kibaka akaipitia simu. Jamaa kaishia kupga kelele “bonyeza send, bonyeza send wewe” abiria wote hawana mbavu
Hili nalo neno kwa wavulana
Hili nalo neno
Demu wako anakuja kwako kasuka nywele za 30,000 na hujampa hata mia,we unakalia kusema waooo waoooo kama king’ora cha ambulance.
Shauri yako we endelea kusema waoooo waooo na atakuwa wao kweli.
😂😂😂😂😂😂😂
Sipendi ujinga. Cheki nilichokifanya
Nimeingia chumban nikakuta panya wamekula dawa yangu ya minyoo,
Na mimi nimechukua yakwao nikanywa.
Sipendagi ujinga mm!!
😏😏😏
Namna wazazi wanavyoongea na mabinti katika umri tofauti
Miaka 13: Usipende wavulana ni wabaya.
Miaka 18: Sitaki nikuone na yule mvulana tena!
Miaka 23: Lini utatuletea mchumba wako?
Miaka 26: Wenzio wanaolewa.
Miaka 30: Tumekuambia kwamba acha
kuchagua sana wanaume, hutaki kusikia!
Miaka 33: Kuna mtu wa Mungu yupo kule
anaombea unaweza kupata mchumba
Miaka 36: At least pata mtoto mmoja.
Miaka 39: We will take care of all the wedding
bills…yeyote ni sawa sisi tutagharamia kila kitu mwanetu wee mlete tu .
Miaka 45: hivi kweli nani alikuroga.?
😂😂😂 changamkia fulsa umri ukifika
Kilichotokea nikiiwa namsaidia mtoto home work
Kusaidia Mtoto wa Nursery Homework ni Ngumu. Unamuuliza “Nina Pipi Tano, nikiwagawia Watoto Watatu, kila mmoja Pipi Mojamoja nabakiwa na ngapi? Anakwambia, “toa Kwanza nizione..”😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Jinsi Mapenzi yanavyoweza kukupa stress
Mapenzi ni balaa
Mapenzi ujue yanawez kukupa stress adi mama ako akikuuliz what’s wrong🤔-—unawez kumjib MAMA WE BADO MDOGO UWEZ ELEW🤣🤣🤣
Kilichotokea baada ya jambazi kuvamia kanisa
Jambazi mmoja aliingia kanisani na bunduki akapiga risasi juu ya bati akasema “asiyempenda YESU atoke nje” wakatoka wote ispokuwa Mchungaji na Wazee wawili.
Jambazi likamwambia Mchungaji “unaweza kuendelea na ibada, nilikuwa nakuondolea wanafiki”, Mchungaji akasema “ungewaacha kwanza nichukue sadaka…!
Hawa wanaume wanaopenda wanawake hovyo barabarani wamepatikana, hawatarudia 😂😂😂
Marafiki wawili (Jose na Ben) walikuwa wanatembea mtaani akatokea mwanamke akarusha busu kwa mmojawapo kupitia dirishani katika jengo la ghorofa tatu.
Wakaanza kujadiliana kama ifuatavyo:
Ben: Muone yule mrembo amenirushia busu
Jose: tafadhali achana na huyo mwanamke, usimjali..
(baadae yule mwanamke akamuashiria aende)
Ben: yule mwanamke ameniita!
Jose: Rafiki yangu, usiende. Nakutafadhalisha.
Ben: Kwa nini unaniambia nisiende Wakati mrembo kama yule ananiita? Huo ni wivu
Jose: Ben, Ninakutafadhalisha tena, usiende, tafadhali usiende kule (akihisi kutotiliwa maanani)
(Rafiki yake alimpuuza na alienda kwa yule mwanamke, mwanamke alishuka kukutana naye na wakapanda juu. Ghafla wakiwa wanataka kuanza taratibu za kula uroda, wakasikia mlio WA gari getini).. 🔊🔊
Lady: _(akiangalia kupitia dirishani)_
Oooh! Yule ni mume wangu!!
Ben: Mama yangu !
Nipo matatani, kweli ? ..!!
Lady: Usiwe na khofu, jifanye kuwa Dobi na anza kupiga pasi hizo nguo
(akimuonyesha lundo la nguo)
(Ben alitumia masaa matano kukamilisha kunyoosha zile nguo kwa sababu yule mume hakutoka tena siku ile)
(Siku iliyofuatia Ben alikwenda kwa Rafiki yake)
Ben: Kaka, unaweza kuamini Jana nimepiga pasi nguo kwa masaa matano???
Jose: Lakini nilikwambia usiende. Nguo zote hizo ulizonyoosha, Nilizifua Mimi Juzi!!
😂😂😂😂😂😂😂😂😂
When an experienced person speaks … 👂you must listen..!
Cheka na methali
1.Simba mwendapole =Huyo ni Sharobaro
2.Asiyefunzwa na Mamae= Ujue Mama hajapitia Ualimu
3.Zimwi likujualo= Lilikuona Sehemu.
4.Chelewa Chelewa= Ukizikusanya utapata Ufagio.
5.Hakuna Masika= Wakati wa Kiangazi.
6.Mpanda Ngazi= Asiwe Mwoga kuanguka
7.Dua la kuku=
Bismilah rahman rahim
11.Penye wengi= Pana Ajali au Tukio
12.Ukiona vyaelea= Ujue ni vyepesi.
13.Mwenye nguvu= amekula ugal wa dona(…..)
Huyu mtoto kaongea point kweli, angalia anachomwambia baba yake
Mtoto alimwuuliza baba yake,
Mtoto: Baba unaweza kumwachia hilo gari lako house boy/girl akaliendesha?
Baba: siwezi kumwachia gari langu hili aliendeshe ni ghali sana.
Mtoto: je mnaweza kumwachia chumba chenu house boy/girl kikiwa wazi na mkaenda kazini?
Baba: haiwezekani kamwe kuna vitu vya gharama na pia heshima haitakuwepo.
Mtoto: unaweza ukampa house boy/girl ATM CARD yako na namba ya siri ukakuchulie pesa?
Baba: mtoto unatafuta balaa sasa, unataka siku akiiba hii card akachukue pesa zote tuwe maskini, sithubutu.
Mtoto: aahaaaaaa, kumbe hauwezi kumkabidhi chochote chenye thamani house boy/ girl, sasa kwa nini mnanikabidhi mimi kwa house boy/girl na nyie mnaenda kazini mpaka mnarudi kumbe mimi sina thamani kwenu eeeeh!
Kilichotokea baada ya kumdanganya mchungaji wangu
Jumapili baada ya kutoka KANISANI, Pastor akaona simu yangu niliyonunua LAKI 5,akaniuliza hiyo simu umenunua Bei gani?
Kwakuwa natoaga sadaka kidogo,na ZAKA ndo sijawahi kutoa,Nikamjibu nimenunua JANA,ELFU 50, akanipa LAKI MOJA,nikanunue mbili,yake na ya mke wake. Sa najaribu kumuuliza Mungu,kwanini kaamua kuniadhibu mbele ya mchungaji bila hata kunionya!
Acha usumbufu…
UNAMNG’ANG’ANIZA MPENZI WAKO AKUWEKE KWNY PROFILE PICHA MLOPIGA PAMOJA
HIVI ULIDHANI MWL.NYERERE ALISHINDWA KUKAA NA MKEWE MARIA KWNY NOTI YA BUKU
😂😂😂😂😂😂😂
Acha Usumbufu…..
Ndoa zina mambo, cheki haya mambo ya mtu na mke wake
Mke: mume wangu leo 2badilishe stail kwani nimechoka kla siku hiyo hiyo tu
Mme: kwel mke wang hata mimi nilikuwa nataka nikuambie hivyo hivyo
Mke: sasa stail ya leo wewe utaosha vyombo mimo nitaangalia tv
Mme: huna haya wala hujui baya…!!!
we unadhani ni xtail gani mume aldhani???
Utani wa wahindi, cheka kidogo
Mhindi afaulu mtihani wa Kiswahili
(1) Mfa maji ?……………….. Tampa life jacket.
(2) Mwenda pole?………… Tachelewa fika.
(3) Usipoziba ufa ?……….. Mizi taona mpaka dani.
(4) Usilolijua ?……………… Uliza google.
(5) Mbio za utelezini ?……. Chafua guo yako.
(6) Ukipenda boga ?……… Ngoja mezi ya ramzani tapata.
(7) Ukiona vinaelea ?…….. iko nyepesi hiyo.
(8) Maji yakimwagika ?…… Mambie dada tapiga deki.
(9) Chelewa chelewa ?……… Takosa guo ya sikukuu…
(10) Kila ndege ?………….. …Hutua Airport
(11) Bandu bandu ?….. …….Rafiki yake Jecha
(12) Mtaka cha Mvunguni ?… Ondoa tanda
(13) Simba mwenda kimya?….Kama sio gonjwa basi haina njaa.
(14) Aisifuye mvua ?………. Najua iko Mkulima hiyo
(15) Barabara ndefu ?…….. Ongeza mwendo au tachelewa fika.
(16) Mlanawe hafi nawe ila?…. Takimbia
(17) Asie sikia la mkuu ? …….. Tapeleka jela
(18) Hasira za mkizi ? …………..Tatafuna veve
(19) Mchamba wima ?…….. Karibu ya Hurumzi
(20) Akumurikae mchana ?….Kipofu hiyo
(21) Mficha maradhi ?…….. Taenda Loliondo
(22) Mkataa wingi ? ……….Taenda Chadema
(23) Bendera ?……………. Kama sio ya CCM, ya CUF
(24) Baniani mbaya ?……. Peleka Bombay Lakini sio HB kweli, naonea tu
(25) Akili nyingi ?………. Tapasi mtihani yote
(26) Penye kuku wengi ? …….. Chija bili tatu ivi, hapana mtu najua.
Angalia alichojibu huyu mwanafunzi, Ungekua wewe ni mwalimu wake ungemfanyaje?
Mwanafunz alikuwa kila siku anachelewa shule, na kila siku alikuwa anachapwa, basi siku moja mwalimu akaona ngoja amuulize.
Mwalimu: Mbona unachelewa kila siku?
Mwanafunzi: Nakaa mbali mwalimu
Mwalimu: (huku ana hasira akauliza)Mbali mbinguni?
Mwanafunzi: Mbinguni kwa mbele😂😂😂😂😂
Recent Comments