Visa Vya Jumapili
Alichojibu dalali baada ya kufumwa na mke wa mtu ndani ya nyumba ya kupanga
Dalali aliwatafutia jamaa chumba Buguruni karibu na reli, nyumba nzuri sana. Jamaa na mkewe wakahamia kwa furaha, lakini furaha yao iliisha walipokuja gudundua nyumba ile iko karibu mno na reli treni ikipita mpaka kitanda kinacheza.
Siku hiyo dalali akapita mke akamwita na kumwambia tatizo wakati treni inapita, wakaanza kubishana, yule mama akamwambia dalali kwa kuwa kuna treni itapita sasa hiviโฆ njoo ndani uone mwenyewe.
Bahati mbaya wakiwa wamejilaza kitandani ili dalali aone adhabu wanayopata, Mzee mwenye mali alirudi ghafla, akauliza,
‘Nyie mnafanya nini hapa?’
Masikini dalali kwa woga mkubwa akajibu’ Tunangoja treni’
Mambo ya pesa haya..
MAMBO YA FEDHA AISEEโฆโฆ. Kuna jamaa alipewa shilingi 983628763600/= โฆacha uvivu, najua hujasoma ni kiasi gani hicho cha fedha na mbaya zaidi hujagundua kwamba katikati ya namba hizo kuna herufi Aโฆ safi sana, najua umeangalia tena kuiona hiyo herufi, bahati mbaya hujaiona. ๐๐๐๐๐๐๐
Tofauti ya ukopaji wa mzungu na mswahili
MZUNGU: Hi, I need $100, will pay back on Monday
MSWAHILI: Kaka vipi, shwari? Dah.. hatuonani mzee, mishe vipi, mnatunyima nini? Juzi nimekuona kwa mbaaaliโฆ mzee shavu dodo, full kipupwe! Sie tupo bwana, shida tu, afu misiba mingi tu, wife nae kajifungua ghafla. Sasa, kuna cheque naisubiri haijatoka hadi leo, wanasema itatoka next week, hapa nimekwama kweli. Naweza pata ‘Laki Moja’ ya karibu hapo nitarudisha mwisho wa mweziโฆ?๐๐๐๐๐
Padri Akimbia wakati wa kuungamisha, chanzo ni hiki
Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani
peke yake.
Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa
pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama
{confess}
“Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya
dhambi kubwa sana.”
Padri, “Endeleaโฆ”
“Bosi wangu aliniita nyumbani kwake, akaniambia
amegundua nimeiba shilingi millioni 100 kazini. Akasema
nisipozitoa atanipeleka polisi, sa kwa ukweli mi naogopa
kufungwa.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu,nikatoa bastola nikamuuaโฆ.. Yesu atanisamehe?”
Padri: “Utasamehewa.”
“Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango
unafunguliwa kutazama, Loh! Mke wa bosi, alipoona
kilichotokea akasema anapiga polisi simu.
Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuua na yeye piaโฆ Yesu atanisamehe hilo?”
Padri: “Utasamehewa.”
Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke, lakini mlinzi
akakataa kunifungulia, ati amesikia mlio wa
bastola. Nikaona ataniletea kizuizi huyu.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuuaโฆ.. Yesu atanisamehe?”
Padri:”Utasamehewa.”
“Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda
nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi
akabisha hodi, nikawaza mambo gani tena, akasema alirudi
nyumbani na kukuta yaliyotokea akanionesha diary ya
babake, inayoonesha nilikuwa na appointment naye
wakati nilipomuua. Nikamuuliza nani mwingine anayejua?
Akasema ameanzia kwangu kisha anaenda polisi.
Nikatazama huku na huku nikakuta tuko wawili peke
yetu, nikamuuaโฆ.. Yesu atanisamehe na hilo?”
Kimyaaโฆ.
“Padri yesu atanisamehe?”
kimyaโฆ.
Jamaa akatazama kwenye confession booth padri
hayupo, lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo
za mapadri linatikisika. Kufungua akaona padri kajificha ndani anatetemeka huku akitokwa na jasho.
Jamaa, “Sasa baba mbona umekimbia?”
Padri kwa taabu akajibu, “Nilitazama huku na huku
nikagundua tuko wawili peke yetuโฆโฆ.”
Chezea kufulia!
Huu Mwezi jinsi nilivyofulia yaani hata nikikuta mende wamesimama wawili najua wananisema
๐๐๐
Angalia wadada walivyoumbuka kwenye hii test
Ticha katangaza test , Akatoa Masharti; Ukiandika jibu hamna kufuta au kukata.
Swali la kwanza,
Taja vyakula vi3 ambavyo ukienda hotelini umelipiwa utapenda kula (marks 1)
WAVULANA wakajaza; wali, ugali, mihogo.
WADADA wakajaza; burger, pizza, egg chop. Swali la
2: Eleza jinsi ya kupika kila chakula ulichotaja hapo juu. (marks 99)
wacha wadada waanze kuhangaika kukata majibu ya mwanzo!
Sababu za kumuacha mke kama umemchoka
Ukimchoka mkeo, waweza kumtaftia sababu za kumuacha kama hizi
_
1. Missed calls 16? Umeua betri la simu yangu. Kwa hiyo hata mimi unaweza kuniuaโฆ It’s Over!!!
_
2. Hata hunieshimu. Mi naongea na wewe lakini we upo bize unavuta pumzi? It’s over!
_
3. Nimekupigia umepokea simu hapohapo. Huna subira. Itโs over!!
_
4. Nilikwambia huwa napenda chakula cha moto lakini hujanipashia ice cream. Hunijali. It’s over!
_
5. Nimekupa mayai mawili, moja uchemshe jingine ukaange. We umekaanga ambalo ulitakiwa kuchemsha na umechemsha ulilotakiwa kukaanga. Huniheshimu, Itโs over!
_
6. Nimekuita DARLING na wewe ukaniita HONEY. Yani kwa maana nyingine unamuita mama yangu NYUKI. Huheshimu wazazi wangu, fungasha kilicho chako. its over.
๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Recent Comments