Januari kweli ngumu, soma hii
Januari kweli kiboko
Hii january sabuni za kuogea ni zile za kuoshea vyombo, yani unakutana mjini na mtu ana mchicha shingoniโฆ๐
Januari kweli kiboko
Hii january sabuni za kuogea ni zile za kuoshea vyombo, yani unakutana mjini na mtu ana mchicha shingoniโฆ๐
Chizi kakaa ukingoni mwa bahari analia kwa masikitiko na huku kakamata kijiko cha chai. Mwezake akamuuliza mbona unalia mwenzangu. Chizi akajibu nimetia vijiko vitatu vya sukari baharini, kila nikionja bado ina chumvi. Mwenzake akacheka sanaaaaaa akamwambia. Hujakoroga!!!!๐๐๐๐๐๐
BABA: mwanangu kwenye huu mtihani uliofanya natumaini utafanya vizuri.
DOGO: ndio baba nitapata mia kwa mia.
BABA: kwanini unasema hivyo?.
DOGO: kwasababu jana kanisani tulifundishwa “Yesu ni jibu” kwahiyo kote nimejaza Yesu.
BABA: kwel kazi ipo
JE UNGEKUWA WEWE HUYO NDO MWANAO UNGEMFANYAJE?
UNAMNG’ANG’ANIZA MPENZI WAKO AKUWEKE KWNY PROFILE PICHA MLOPIGA PAMOJA
HIVI ULIDHANI MWL.NYERERE ALISHINDWA KUKAA NA MKEWE MARIA KWNY NOTI YA BUKU
๐๐๐๐๐๐๐
Acha Usumbufuโฆ..
๐๐๐๐๐
*UCHAWI* ni nini?
`Uchawi ni pale mpenzi wako anapokupeleka kwao kufika tyu ghafla unakutana na dada yake getini ambaye alikuwa ni mpenzi wako wa zamani, ile kuingia ndani unamuona kaka yake ambaye mlipigana baada ya kukufumania na mke wake, hujakaa vizuri unamuona mama yake ambaye ndiye jimama shangingi lako anayekuweka mjini akupaye jeuri ya kutamba ambapo hata gari unalolitumia alikupa yeye na hataki upajue anapoishi, wakati unataka kuondoka unakutana uso kwa uso na baba yake ambaye alikuwaga wakili wako kwenye kesi ya ubakaji`
๐คฃ๐๐๐๐๐คฃ
HAHAHAHAHAAAAAA DUH TAMAA MBAYA
Muokota makopo katika uokotaji wake wa makopo akaona chupa ambayo ndani kuna ki2, alipoifungua likatoka jitu la ajabu. Huku akitetemeka lile jitu likamwambia kijana asante sana kwa kuniokoa omba vi2 viwili sasa hivi. Kijana kwa hofu akaomba pesa za kumiliki magari na majumba ya kifahari. Ghafla fuko la hela na pete ya bahati vikadondoka. Akaambiwa ombi la pili,akasema nibadilishe niwe kivutio ili nipendwe sana nakina dada Hapohapo akageuzwa akawa chipsi yai.!!๐๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuniโฆunaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuniโฆ๐๐๐๐
1.Simba mwendapole =Huyo ni Sharobaro
2.Asiyefunzwa na Mamae= Ujue Mama hajapitia Ualimu
3.Zimwi likujualo= Lilikuona Sehemu.
4.Chelewa Chelewa= Ukizikusanya utapata Ufagio.
5.Hakuna Masika= Wakati wa Kiangazi.
6.Mpanda Ngazi= Asiwe Mwoga kuanguka
7.Dua la kuku=
Bismilah rahman rahim
11.Penye wengi= Pana Ajali au Tukio
12.Ukiona vyaelea= Ujue ni vyepesi.
13.Mwenye nguvu= amekula ugal wa dona(โฆ..)
Wasiopanda dalaladala wanakosa uhondo wa kauli hizi
1. nitakupa
2. Atapewa mbele
3. Hujapewa mbele?
4. Utapewa nyuma
5. Nitakupa nikikaa vizuri
6. Ngoja isimame nikupe
7. subiri asimamishe nikupe
8. hivi nlivyo kaa ntakupaje?
9. Utapewa tulia
10. Nikupe mara ngapi?
HABARI MPASUKO..
jana katika taasisi ya wanyama pori ya Nat Geo ilitangazwa kuwa ametokea Nyoka hatar san Ambaye hajawah kutokea duniania.. wanadai kwamba nyoka huyo anaongezeka ulrefu wa 0.5sm kila akila chakula na huwa anakula chakula kuanzia sekunde 30 kurudi nyuma.. mpaka sasa hakuna siraha ya kuweza kumuua nyoka huyo isipokuwa akiji uma mwenye ndo anaweza kufa, wanasayansi hao walieleza japo uchunguz zaid bado unaendeleaโฆ huyu ni nyoka anayeua kuliko nyoka wote waliowah kutokea katika historia ya maisha ya mwanadam..
nyoka huyu hupatikana katika simu pekee za nokia toch katika sehem ya game inaitwa snake xenzia..
asanteni kwa kufurah na umakin mkubwa katika usomaji wa matini hiiโฆ
haya ni mambo ya wikiend jaman na iwe njema kwenu wote
Recent Comments