Visa Vya Jioni Hii

Je, Chuoni kwako Kukoje?

FACT!
1.Ukiona geto lina feni, sabufa, meza ya plastic na kitanda ch sita kwa sita na Pc UJUE ni jamaa wa UDSM.

2. Ukaona geto lina nguo nyingi za watu tofauti tofauti, unga mwingi, vtunguu vng, nyanya halaf pembeni, Vitabu vya kutosha na lundo la karatasi za betting ujue huyu JAMAA ni wa SAUT.

3. Ukaona geto halina kitu ndani zaidi ya mkate wa bakheresa na kopo la maji UJUE huyu jamaa ni wa UDOM😂☝

4. Ukaona geto lina visamaki vikavu mezani, Notes za kutosha mezani na jaba pembeni UJUE huyu ni MJAMAA WA MWENGE/MWECAU😜👤

5. Ukaona geto lina Mawigi mengi na dressing table pembeni, ngazi ya kuwekea viatu UJUE huyu mjamaa ni wa RUCO IRINGA😘

6. Ukaona geto lina spray za kila aina, Nguo nyingi hasa za mitumba ambazo zimemodolewa mpaka tight UJUE huyu MJAMAA ni wa USHIRIKA MOSHI.

7.Ukiona geto lina Nyanya na mikungu ya ndizi halafu halafu nje kuna jiko la Mkaa UJUE huyu mjamaa ni wa TEKU mbeya😳

8. Ukiona geto lina tranka na nje wamevulia buti, viatu vya matope UJUE huyu Mjamaa ni Wa SMUCO MWIKA.

9. Ukaona geto ndan mashuka ya kimasai kinabao, hapa usipatwe na Mashaka, Jua huyu ni Mjamaa wa MAKUMIRA. 😜😜😜😜

10. Ukaona geto lina vimodo, vimini, miwani za tittled, jiko la mafuta ya taa, kitandani mito zaidi ya Minne,Visarafu kwenye meza, Tshirt nyingi za semina za family planning, Ukimwi n.k halafu chini tv ya chogo na king’amuz cha continental Ujue huyu MJAMAA ni wa TIA DSM 😱😱😱😱😱😱😱

⏬⏬⏬⏬⏬⏬⏬⏬⤵⏬🆙🆙🆙🆙
JE, KWAKO KUKOJE? ???
😋😋😋😋😋😋😋😋😋😋😋

Cheki masifa yalivyomponza huyu, Sifa nyingine ni mbaya jamani

Mbongo, Mganda, na Mkenya walikamatwa na makosa Uchina.

Wakaambiwa adhabu ni ama kifo cha moja kwa moja au adhabu nyingine ambayo atakayeifaulu atakuwa huru, atakayeshindwa atauawa.

Basi wao wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu bahati yao.

Wakapelekwa msituni wakaambiwa kila mmoja aende kwa njia yake halafu arudi na matunda kumi ya kufanana.

Wakaingia msituni kila mtu njia yake.

… Mganda akarudi wa kwanza na machungwa kumi. Akaambiwa adhabu yake ni kumeza moja moja likiwa zima bila kufumba macho bila kulia wala kucheka wala kujitikisa mpaka yote kumi yaishe. Akameza la kwanza. Safi. Kumeza la pili, akashindwa kuvumilia akafumba macho. Akapigiwa risasi akafa.

Mkenya akaja. Ana vitunda vidogo vidogo kama pili vilaini. Akasomewa masharti. Akaanza kumeza bila kufumba macho wala kulia, wala nini… alipofika cha tisa akashindwa kuvumilia akaangua kicheko! Akapigwa risasi pia akafa.

Wakiwa kuzimu Mganda akamwuliza Mkenya, “Vipi, mbona ulishindwa kuvumilia wakati kilibaki kitunda kimoja tu?”

Mkenya akamjibu: “Mkuu, nilishindwa kuzuia kicheko maana nilimwona Mbongo anakuja na matikiti maji!”

Ufugaji wa nguruwe kazi, Cheki jamaa hawa wake walivyompa mtihani

MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalishanini?
.

MFUGAJI: Nawalisha mabaki ya chakula toka migahawa mbalimbali
.
MWANAHARAKATI: Hayo ni makosa unawatesawanyama kwa kuwalisha chakula kichafu. Akapigwa faini… Baada ya siku chache wakaja wanaharakati toka Umoja wa Mataifa
.
MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalisha nini?
.

MFUGAJI: Huwa nawaanzia siku na uji wa ulezi, halafu mikate, mchana ugali kwa kabeji na usiku viazi
.
MWANAHARAKATI: Loh watu wanakufa kwa njaa wewe unalisha nguruwe, akapigwa faini….siku chache baadae wakaja wanaharakati wa Mazingira
.
MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalisha nini?
.
MFUGAJI: (Kwanza akasita kidogo) Hawa huwa nawapa shilingi alfu tano kila mmoja kila siku halafu wao wenyewe wanaenda kununua chakula wanachokitaka.. .

Tofauti ya mke na mchepuko!!!

Mke ni kama Tv na Mchepuko ni kama Simu.
Nyumbani unaangalia Tv lakini ukitoka unatoka na simu.

Mara chache unafurahia Tv lakini Muda mrefu unacheza na simu yako.

Tv ni bure kwa maisha yako yote, lakini Simu kama hujalipia hupati huduma.

Tv ni kubwa nzito na wakati wote ni ya zamani. Lakini simu ni nzuri, nyembamba, na ni rahisi kubeba.

Gharama za huduma za tv ni ndogo sana, Lakini gharama za huduma za Simu ni kubwa na pia ni lazima kuzitimiza.

Tv ina remote lakini Simu haina.

Kitu muhimu zaidi simu ina njia mbili za kuwasiliana unaongea na unasikiliza lakini Tv unalazimika kusikiliza hata kama hutaki au unataka.

Unaweza kununua Tv mara moja na ukatumia kwa kipindi kirefu lakini Simu mara zote unabadilisha inategemea na fasheni.

Ya mwisho na ya kuzingatia

Tv haina Virusi lakini Simu inayo.

KUWA MAKINI.

Kilichotokea baada ya bibi na babu kukumbukia mahaba ya ujanani

Mzee wa miaka 60 alimwambia mkewe, leo nataka tukumbukie enzi zetu kutongozana, mke akajibu sawa, inabidi unisubiri mwembeni saa 1 usiku nitapita, mzee akafika saa 1 alikaa hadi saa 5 usiku, aliporudi nyumbani akamuuliza mkewe kwa hasira; sasa tumepanga nin halafu haujatokea ?
Mke; leo mama alinikataza nictoke nyumbani usiku nijisomee ! Babu hoii…

Ungekua wewe ni mwalimu ungemshauri nini huyu mwanafunzi?

Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.

MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?

JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.

MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?

ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga.

MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.

MWAL: Na wewe James??

JAMES: mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiwe……”

Akameza mate kisha akaendelea….

“Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali.”

MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??

JENNY: Nataka kuwa mke wa James.!!

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About