Visa Vya Ijumaa
Cheka kidogo, angalia anachosema huyu mchaga
Mchaga baada ya kufa akaulizwa na malaika anayetoa roho: Mangi hapa ni njiapanda kulia ni Mbinguni na kushoto ni Jehanamu, Je unachagua kwenda wapi?
MANGI: Bwashee, mi nabaki hapa hapa njiapanda aisee.
MALAIKA: Kwa nini?
MANGI: Aisee, nikifungua duka hapa si nitapata wateja wa Mbinguni na Jehanam. Yani patakuwa senta ya hatari, supu na nyama choma muda wote. Hata we utafaidi, unavyoenda kuchukua roho unaniletea stock nakupa hela yako cash mkononi. Na kila ukipita hapa unapiga mchemsho wako wa ulimi na bia mbili chap kabla ya kuingia mbinguni.
Kwanza nashangaa Shirima alipitaje hapa bila kushika ploti, au alikufa amelewa sana?
Nilichokifanya jana baada ya kushuka kwenye basi Ubungo
Jana nateremka kwenye BASI UBUNGO nataka nichukue TEKSI hadi KIMARA naambiwa sh.15,000/=.
Wakati niponatafakari hiyo bei, nikasikia “Moro, Moro,Morogoro sh.6,000/=”
Nikaamua nipande niende zangu MOROGORO.
Kwenda na kurudi sh.12,000/=.
Wakati wa kurudi nikamwmbia KONDA aniteremshe KIMARA.
SIPENDAGI UJINGA MIMI NA BEI ZA TEKSI.
Angalia ndoto nyingine zilivyo na Majanga
Ndoto zingine bwana usiombe zikupate
Mimi usiku wa kuamkia Leo nikiwa nimelala nimeota naendesha gari Yangu aina ya BMW mpya Mara gafla ikakwama kwenye tope .hivyo ikabidi nishuke ili kuisukuma loh! Yani kudadeki ile kuamka nikakuta nimesukuma kitanda hadi sebleni Daaa ilinisikitisha sana jiangalie sana sese hivi ndio narudisha kitanda chumbani .angalizo angalia ndoto unazo ota unaweza kuota upo baharini ukaamka unajikukuta unaogelea kwenye Jaba la Maji shauri yako.
Soma hii, Nani haelewi kati ya hawa?
Dogo: Bro naomba nitumie hela.
Bro: Tumia tu mpaka uchoke.
Dogo: Hujanielewa,nitumie hela.
Bro: We ndo hunielewi, nimesema tumia tu…!!!
Punguzeni pombe. Cheki kilichompata huyu
Jamani punguzeni pombe,kuna jirani yangu amerudi amelewa sasa nachungulia dirishani naona anagonga mlango wake takribani masaa mawili,wakati hapa anaishi peke yake, kwakuwa sipendagi ujinga nimetoka nikamwambia mwenyewe kasafiri.Nae kaondoka.
Cheki huyu jamaa alivyoumbuka akiwa ndani ya dala dala baada ya kupokea simu ya mkewe
Jamaa kapokea simu kutoka kwa mke wake ndani ya daladala
jamaa: hellow hellow ( jamaa akawa hasikii vizuri ikabidi aweke loud speaker)
Mke: Umeweka wapi soksi zako yaani nyumba nzima inanuka.
Njia 3 rahisi za kuondoa kitambi
JE, una KITAMBI na unataka kukiondoa?
FANYA HAYA;
1. Kopa mkopo mkubwa benki
2. Nunua gari bovu la biashara
3.Oana na mke mwenye kelele.
Ukiona miezi mitatu hakijaisha basi ujue umevimba BANDAMA sio kitambi..
Kwa Wadada wanaotaka kuolewa
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuni…unaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuni…😂😂😂😂
Angalia huyu Jamaa alichomfanyia mke wake jana
Jana niligombana na mke wng, Akaniambia nibebe kila kitu changu niondoke, Bas kiustaarabu tu nikachukua nguo zangu,mwishoni nikambeba na yeye nikamuweka begani nikaanza kuondoka nae
hua sipendagi ujinga, amesahau na yeye pia ni wangu
Sababu ya watu kupenda mapenzi kuliko vita
Mwalimu aliuliza swali
“Kwanini watu wanapenda MAPENZI kuliko VITA?
Mwanafunzi mmoja akajibu:-
“Kwa sababu CONDOM ni bei rahis kuliko BUNDUKI.
Wanafunzi wote: Ndiooooo…!!
Baada ya kuumizwa kimapenzi haya ndiyo maneno
Mkishaumizwa ndo utasikia, Moyo sukuma damu sio mengine. wakati mnapenda mlizani moyo ulikuwa unasukuma kinyesi!!!!!??????😂😂😂😂
Cheki jinsi huyu mwanaume alivyomuweza mwanamke wake
Demu alimpigia simu jamaa yake ilikua weekend mazungumzo yalikua hivi:-
Demu: hello baby wangu leo bata wapi?
Jamaa: jamani bby si bandani kwao….
Demu: mmmmmmmh!
Kilichotokea baada ya babu mzee kuibiwa nauli kwenye daladala
Mzee mmoja alipanda Gari Stend;
Wakati wa kugombania Siti,
Akaibiwa Nauli.
Akasimama katikati ya Gari-Akasema; “Jamani Naomba Aliyeniibia Pesa yangu Arudishe Haraka,
Tena Fasta kabla Sijafanya Tukio kama Nililofanya 1977″
Abiria kuskia hivyo wakaogopa.
Ikabidi Mwizi Ajitokeze,
Akarudisha Pesa na Kuomba Msamaha! Mtu Mmoja akauliza,
Mzee,
Kwani 1977 Ulifanya nn?
Si nilienda kwa Miguu mpaka Nyumbani!
Uscheke Peke Yako, wa2mie na wengine ili nao wacheke!
Mambo ya kijijini haya!
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuni…unaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuni…😂😂😂😂
Mme amemfuma fundi wa kitanda na mke wake, cheki walichokua wanafanya
Kuna mama mmoja ameolewa na wanapendana sana na mmeo. siku moja mme wake alisafiri kikazi (safari ya zaidi ya mwezi) nje ya mkoa. Siku mmeo anarudi, yule mama alimtafuta fundi seremala amrekebishie chaga za kitanda zilikuwa zimeharibika, kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya above +18.
Wakati fundi anaendelea na kazi kumbe mmeo huyu dada alishafika. hakutaka kumjulisha mkeo, kwa nia nzuri tu ya kumfanyia suprise, kwani alikuja na mazaga zaga kibao. Hiyo aliingia kwa kunyatia hadi kwenye mlango wa chumbani kwao. Ghafla akasikia mazungumzo ya mkeo na fundi ndani. Mazungumzo yalikuwaje? fuatilia hapa chini
Mama X: Fanya haraka mme wangu amekaribia
Fundi: Nakaribia kumaliza, nisaidie kuchomeka vizuri upande wako (akikusudia chaga)
Mama X: Mbona haiingii
Fundi: Ingiza kwa upande upande
Mama X: Sukuma kwa nguvu
Fundi: Angalia usiumie
Mama X: Hamna shida imeingia
Wakati jamaa akiendelea kusikiliza mlangoni, fundi akaweza godoro juu ya kitanda na mama x akajitupa kitandani kujaribu kama kimetengamaa. mara chaga akachomoka na kuanguaka chini. Nini kilifuata
Mama x: Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii iiiii(miguno) “my God, mbona hivi”
Fundi : Pole sana
Mama X: sasa?
Fundi: Ngoja nichomeke tena
Mama X: Yaan wewe, utaacha mme wangu afike hatujamaliza
Fundi: Usijali namaliza sasa hivi
Baada ya dakika chache, fundi akamuaga mama na kumwambia tayari, sasa naona umefurahi. Kutoka tu mlangoni akakutana uso kwa uso na jamaa amekunja ndita kama matuta ya viatu. Gues what happened?
Kitu gani kitatokea kisia toa maoni yako kama ni ww ungefanyaje?
Angalia huyu mwanamke mwenye wivu kwa mumewe alivyoumbuka, Mme wake kamuweza kweli
WIVU HUU NI NOMA
Mke: Hivi mume wangu una wanawake wangapi huko nje?
Mume: Kama nywele za kichwa changu.
Mke akachukua nguo zake akaondoka, Kufika njiani akakumbuka mumewe alikuwa na kipara Akaanza kurudi kwa mumewe.
Cheka kidogo hapa. Huyu Chizi Kachizika Kweli
Mvaa milegezo alizidiwa na pombe akaenda kulala dampo,
Chizi mwingne naye akaenda hukohuko, alipofika dampo akakuta mlevi kalala matako wazi,
chizi akaanza kuyashikashika huku akisema, kweli duniani kuna watu matajiri, haya matako si mazima kabisa wao wameyatupa!😆😆😆
Baada ya kunitumia SMS usiku ikawa hivi….
Jana usiku kuna Jirani yangu..kanitumia text “mambo vipi?”…halafu tunakaa nae mtaa mmoja nikaona nikimjibu ni uharibifu wa hela nikaenda kumgongea mlango saa 7 usiku. Alipofungua nikamjibu “shwari”halafu nikarudi nyumbani kulala zangu..
Sipendagi kuchezea salio..
😂😂😂😂😂
Padri Akimbia wakati wa kuungamisha, chanzo ni hiki
Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani
peke yake.
Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa
pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama
{confess}
“Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya
dhambi kubwa sana.”
Padri, “Endelea…”
“Bosi wangu aliniita nyumbani kwake, akaniambia
amegundua nimeiba shilingi millioni 100 kazini. Akasema
nisipozitoa atanipeleka polisi, sa kwa ukweli mi naogopa
kufungwa.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu,nikatoa bastola nikamuua….. Yesu atanisamehe?”
Padri: “Utasamehewa.”
“Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango
unafunguliwa kutazama, Loh! Mke wa bosi, alipoona
kilichotokea akasema anapiga polisi simu.
Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuua na yeye pia… Yesu atanisamehe hilo?”
Padri: “Utasamehewa.”
Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke, lakini mlinzi
akakataa kunifungulia, ati amesikia mlio wa
bastola. Nikaona ataniletea kizuizi huyu.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuua….. Yesu atanisamehe?”
Padri:”Utasamehewa.”
“Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda
nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi
akabisha hodi, nikawaza mambo gani tena, akasema alirudi
nyumbani na kukuta yaliyotokea akanionesha diary ya
babake, inayoonesha nilikuwa na appointment naye
wakati nilipomuua. Nikamuuliza nani mwingine anayejua?
Akasema ameanzia kwangu kisha anaenda polisi.
Nikatazama huku na huku nikakuta tuko wawili peke
yetu, nikamuua….. Yesu atanisamehe na hilo?”
Kimyaa….
“Padri yesu atanisamehe?”
kimya….
Jamaa akatazama kwenye confession booth padri
hayupo, lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo
za mapadri linatikisika. Kufungua akaona padri kajificha ndani anatetemeka huku akitokwa na jasho.
Jamaa, “Sasa baba mbona umekimbia?”
Padri kwa taabu akajibu, “Nilitazama huku na huku
nikagundua tuko wawili peke yetu…….”






































































I’m so happy you’re here! 🥳





Recent Comments