Vihoja Vya Wajanja
Cheki wanachokisema vichaa baada ya kuona ndege inapita angani
Vichaa wawili walikuwa wamekaa sehemu ghafla ikapita ndege angani kichaa mmoja akasema ndege ile hitakua imembeba rais kichaa mwenzake akajibu hapana ile imebeba wazungu kama ingekuwa imembeba rais ungeona mapikipiki mbele
Kilichotokea baada ya babu mzee kuibiwa nauli kwenye daladala
Mzee mmoja alipanda Gari Stend;
Wakati wa kugombania Siti,
Akaibiwa Nauli.
Akasimama katikati ya Gari-Akasema; “Jamani Naomba Aliyeniibia Pesa yangu Arudishe Haraka,
Tena Fasta kabla Sijafanya Tukio kama Nililofanya 1977″
Abiria kuskia hivyo wakaogopa.
Ikabidi Mwizi Ajitokeze,
Akarudisha Pesa na Kuomba Msamaha! Mtu Mmoja akauliza,
Mzee,
Kwani 1977 Ulifanya nn?
Si nilienda kwa Miguu mpaka Nyumbani!
Uscheke Peke Yako, wa2mie na wengine ili nao wacheke!
Cheka kidogo: Majibu ya mhindi kwenye mtihani wa Kiswahili alipoambiwa ajibu methali
Mhindi kwenye mtihani wa kiswahili anaambiwa amalizie methali:
(a)Nyani haoniโฆ..valisa miwani!
(B)Debe tupuโฆ.weka dengu!
(c)Masikini akipataโฆ.iko acha iba!
(d)Penye kuku wengiโฆchinja bili,tatu!
(e)Asiyesikia la mkuuuโฆ.peleka yeye polisi!
(f)Penye wengiโฆโฆiko kutano ya chadema!
Haya ndiyo madhara ya kulala kanisani
Tukiwa kanisani mdada alikuwa amelala , akaamka akasikia Pastor anasema
” SIMAMA”
Yule dada akasimama akashangaaa kanisa zima linamtizima kwa mshangao akiwemo mumewe, akaangalia kanisa zima akashtuka kujiona yeye peke yake ndiye aliesimama
Pastor akaendelea vizur endelea kusimama, tumepata mmoja hadi sasa aliyesimama narudia kwa mara ya mwisho kama hujasikia vizuri
” kama wew umewahi kumsaliti au bado unasaliti ndoa yako SIMAMA”
Binti akazimia
Cheki kilichotokea stesheni ya treni, mambo mengine ukipaniki inakula kwako kama huyu jamaa
Jamaa Wawili Walifika Stesheni, wakakuta Treni ndo kwanza inaondoka. Wakaanza Kuikimbiza. Mmoja akafanikiwa kupanda akaondokaโฆ
Yule aliyebaki akaanza kucheka sanaa mpaka machozi yakamtoka. Watu wakamuullza, unacheka nini sasa wakati umeachwa? Akawajibu: “kinachonichekesha, yule aliyepanda alikuwa ananisindikiza.
Jambo la kufanya ukitaka mwanaume akusaidie kazi jikoni
Fanya hivi
Ukitaka mwanaume akusaidie kazi jikoni mwambie “NAOMBA CM YAKO NIWASHE TOCHI TAA IMEUNGUA”
atakusaidia kumulika mpaka unamaliza kazi zako zoote๐
Kilichotokea baada ya mzungu na mbongo kukaa siti moja, bongo wasanii wengi
Mzungu akamdharau sana Mbongo nakujiona anajua kila kitu duniani!,
Akamwambia Mbongo waulizane maswali na Mbongo akishindwa anatoa sh.500 na endapo yeye atashindwa atatoa 100,000/=.
Mzungu akauliza ni nchi ipi ilishindwa kwenye vita kuu ya kwanza ya Dunia?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hajui.
Na yeye akamuuliza Mzungu ni kitu gani kikienda juu kina miguu minne na kikirudi chini kina miguu mitatu?
Mzungu akafikiria akakosa jibu akatoa 100,000/= kuashiria hajui ila akataka kujua, akauliza ni nini hicho?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hata yeye hajui!.
SHARE na marafiki kama umemkubali Mbongo kwa ujanja. Lakini unafikiri Mbongo huyu kwa akili hizi atakuwa ametokea mkoa gani!?.
Mke anamwambia mme wake kuwa angetamani mme wake awe tajiri cheki alichojibiwa
Mke; mme wangu ungekuwa tajiri ningefurahi
Mimi; kwa nini?
Mke; ungekuta na sisi tuna gari nzuri hatutembeu kwa mguu
Mimi; ah wap,unadhani ningekuwa tajiri ningekuwa na wewe?ungekuta natoka na kina wema,zariโฆ
๐๐๐
naona anakusanya nguo zake itakuwa anaenda kufua
Baada ya kunitumia SMS usiku ikawa hiviโฆ.
Jana usiku kuna Jirani yangu..kanitumia text “mambo vipi?”โฆhalafu tunakaa nae mtaa mmoja nikaona nikimjibu ni uharibifu wa hela nikaenda kumgongea mlango saa 7 usiku. Alipofungua nikamjibu “shwari”halafu nikarudi nyumbani kulala zangu..
Sipendagi kuchezea salio..
๐๐๐๐๐
Simu ilivyozua utata
Mama alichukuwa simu akampa mwanawe. Mama..Mpigie babako mwambie chakula tayari. (Mtoto akachukuwa na kupiga) MtotoโฆMama simu ya baba imepokelewa na mwanamke. (Mama kwa hasira) Akirud atanitambua leo. (Baada ya muda kidogo baba akarud,kufika mlangon tu kapokewa na sufuria ya kichwa. Hajakaa vzur mwiko wa pua) Mama..Mwanangu ulipopiga simu ya babako mwanamke wake alisemaje?? Mtoto..Alisema mteja unaempigia hapatikan kwa sasaโฆ..
Recent Comments