Vihoja Vya Wajanja
Angalia huyu jamaa alivyomuweza huyu binti wa chuo
ππππ .. TABU KUDATE NA MADEMU WA CHUO
Demu ;Β Baby Safari Hii Nataka Pale Hostel Niwafunike Mashoga Zangu Wote.
Jamaa ;Β Poa Sweetie Ondoa Shaka Nitakununulia #Turubai Utawafunika Woteβ¦!!!
Demu:Β Mxiuuuuuuuu Lione Sura Kama Goti La mbuzi Na Namba yangu futa Nakublock Mpaka Sanduku la postaβ¦!!!
ππππnmecheka adi nmelazwa
Huyu bwana leo kapatikana, Jamani nyodo nyingine mbaya
Baada ya kumaliza Degree yake ya sheria Bwana Rwegashora aliamua kurudi nyumbani Bukoba mjini na kufungua ofisi yake kwa ajili ya huduma kwa wateja.
Siku moja akiwa ndani ya ofisi yake alimuona mtanashati na mdada mmoja mrembo anakuja ofisini kwake akajua ni mteja anamletea kesi.
Ndipo akanyanyua mkoni wa wa simu ya TTCL na kuanza kuongea huku anajizunguusha kwenye kiti cha kuzunguuka.
Wakati mdada alipokaribia Rwegashora alimkaribisha kwa ishara maana alijifanya yupo busy na kuongea na simu ya umuhimu.
Wakati anaongea na simu akisikika akisema No, No, Noβ¦.. Absolutely No. Wajuulishe hao lay person wa New York kua siwezi kushuhulika na kesi ambayo itanilipa chini ya 50 million. Mimi ni profesional lawyer and im crossing the border to sarve international community.
Aka pose kidogo na akanywa maji kisha akaendeleaβ¦..
Naweza kuanza kukusanya primary evidence next weak but tell them watume kwanza ten million kwa kuanzaβ¦
Hahahahaha you dont know my Account
Mr Roger. Ok waambie watume kwenye Account ileile walionitumia million 100 last monthβ¦
Aka pose tena akameza fundo la maji na kurekebisha tai yake kisha akaendelea⦠Ok usisahau kumueleza muendesha mashtaka mkuu wa marekani kua nitakuja New York mwezi ujao maana nitapita kwanza Amsterdam kuwasilisha utetezi wa yule mteja wangu mholanzi kisha nitaenda Tokyo kulipia ile gari yangu niloagiza.
Wakati anaongea hayo yote yule mdada alikua ametulia na anamuangalia Bwana Rwegashora anavyojizunguusha kwenye
kiti chake huku akiongea kwa tambo kwenye ile simu ya TTCL.
Baada ya kumaliza kuongea na simu Bwana Rwegashora aliweka mkono wa simu yake ya TTCL chini kisha akamgeukia mdada mrembo.
Samahan sana kwa kukupotezea muda wako unajua tena kazi zetu zinaumiza kichwa sana kama unavyoona mwenyewe yaani niko busy sana ninapokea simu sana mpaka nimechoka na simu nyingi ni za wateja wa njee ya nchi.
Anyway nikusaidie nn? Mdada akajibu mimi ni mfanyakazi wa kampuni ya TTCL nimekuja kuunganisha line yako ya simu kwani haipo hewani tangu wiki iliyopitaβ¦!!!
Unadhani Bwana Rwegashora alifanyaje�??
Kichekesho cha mwalimu na wanafunzi
Mtoto: Mwalimu mimi nataka nisome darasa la nne kwani hili la3 halinifai.
Mwalimu: Kwa nini unasema hivyo?
Mtoto: Nina akiliβ¦
Basi mwalimu akamueleza mkuu wa shule na mkuu kaitisha interview kwa dogo. Maswali ni hayaβ¦.
Mwalimu: Kwenye ndege kuna matofali 20 tukitoa moja tukalidondosha chini yatabaki mangapi?
Dogo: Yatabaki 19.
Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka tembo kwenye friji.
Dogo: Unafungua friji unamuweka tembo kisha unafunga.
Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka nyani kwenye friji.
Dogo: Unafungua friji unamtoa tembo ulemuweka..unamueka nyani kisha unafunga friji.
Mwalimu: Kuna sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa simba, wanyama wote wameenda kasoro mmoja. Ni nani na kwa nini?
Dogo: Ni nyani kwa sababu tumemuweka kwenye friji.
Mwalimu: Bibi kizee amevuka mto unaokuwaga na mamba na viboko wakali, aliwezaje?
Dogo: Aliweza kwani mamba na viboko nao walienda kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa simba.
Mwalimu: Ingawa bibi kizee alivuka mto, baadae alikufa. Unadhani ni kwanini alikufa?
Dogo: Alidondokewa na lile tofali tulotoa kwenye ndege na kutupa chini.
Mwalimu mkuu: Huyu dogo akasome chuo kikuuβ¦.
ππππππππ
Utoto bwana. Raha sana!
Utoto buana! eti mnacheza mpira wa makaratasi(chandimu) unapiga chenga kibao afu ukifika golini ufunge unakuta goli hamna kumbe mwenye ndala zake ameitwa kwaoπ
Mlevi kazua tafrani, angalia alichokifanya hapa
MLEVI mmoja aliingia baa akavuta kiti na kukaa mhudumu akatokea kumsikiliza.
MHUDUMU: Nikusaidie nini?
MLEVI: Eeh! nipe bia ya baridi kisaha wasikilize wote waliokaa hapa, wape bia na wao maana sipendi kunywa pombe wengine wananiangalia
Akaja mhudumu wa jikoni “nikusaidie nini?”
MLEVI: Niletee supu kisha wasikilize wote waliokaa hapa na wao wape supu sipendi kunywa supu watu wananiangalia
Safari hii watu wakapiga makofi
Baadae akamuita mhudumu
MLEVI: Niandikie bili zangu kisha waandikie wote bili zao sipendi kulipa huku watu wananiangalia
Wale wateja wakamvaa na kumshushia kichapo⦠teh teh teh teh teh hii kali hakuna cha bure mjini hahahaha na jasho la mtu haliliwi wandugu
Aina mojawapo ya watoto ambao ni hasara kuwa nao
Alipelekwa Hospitali na baba yake, baada ya vipimo Doctor akawa anamuandikia dawa, baba yake akatoka nje kuongea na cm.
Mtoto akamwinamia Doctor na kusema kwa sauti ya chini:- “Doctor Kwenye dozi ya dawa niandikie na FANTA BARIDII, CHIPS na MISHIKAKI kutwa mara 2 kwa siku 30.
Angalia alichojibu huyu mwanafunzi, Ungekua wewe ni mwalimu wake ungemfanyaje?
Mwanafunz alikuwa kila siku anachelewa shule, na kila siku alikuwa anachapwa, basi siku moja mwalimu akaona ngoja amuulize.
Mwalimu: Mbona unachelewa kila siku?
Mwanafunzi: Nakaa mbali mwalimu
Mwalimu: (huku ana hasira akauliza)Mbali mbinguni?
Mwanafunzi: Mbinguni kwa mbeleπππππ
BREAKING NEWS!!! Nyoka wa ajabu agundulika
HABARI MPASUKO..
jana katika taasisi ya wanyama pori ya Nat Geo ilitangazwa kuwa ametokea Nyoka hatar san Ambaye hajawah kutokea duniania.. wanadai kwamba nyoka huyo anaongezeka ulrefu wa 0.5sm kila akila chakula na huwa anakula chakula kuanzia sekunde 30 kurudi nyuma.. mpaka sasa hakuna siraha ya kuweza kumuua nyoka huyo isipokuwa akiji uma mwenye ndo anaweza kufa, wanasayansi hao walieleza japo uchunguz zaid bado unaendelea⦠huyu ni nyoka anayeua kuliko nyoka wote waliowah kutokea katika historia ya maisha ya mwanadam..
nyoka huyu hupatikana katika simu pekee za nokia toch katika sehem ya game inaitwa snake xenzia..
asanteni kwa kufurah na umakin mkubwa katika usomaji wa matini hiiβ¦
haya ni mambo ya wikiend jaman na iwe njema kwenu wote
Wanaume wote ni waaminifu
Hii ni kwa wanaume ila mwanamke anaweza kusoma na kujifunza kuwa wanaume wote ni waaminifu.
Mwanaume mmoja alienda kukata miti kwa ajili ya mkaa, bahati mbaya panga likadondokea mtoni, akaanza kulia sana. Malaika akatokea na kumuuliza kwanini analia. Jamaa akajibu; “Panga langu limedondokea mtoni na ndilo ninalotegemea kuendeshea maisha yangu”.
Malaika akazama mtoni na kuibika na panga la DHAHABU na kumuuliza, ndio hili?
Jamaa: Hapana.
Malaika akazama tena na kuibuka na panga la SHABA na kuuliza, ndio hili?
Jamaa: Hapana.
Malaika akazama tena mara hii akaibuka na panga la CHUMA na kuuliza ndio hili?
Jamaa: NDIYO.
Malaika akafurahishwa sana na uaminifu wake hivyo akampa mapanga yote matatu. Jamaa akafurahi sana.
Siku nyingine jamaa alikuwa anatembea na mkewe njiani ghafla mke akadondokea mtoni, jamaa akaanza kulia. Malaika akatokea na kumuuliza: Kwanini unalia?
Jamaa: Mke wangu kadondokea mtoni na nampenda sana.
Malaika akazama mtoni akaibuka na WEMA SEPETU na kuuliza; “huyu ndiye mkeo?”
Jamaa: NDIYO.
Malaika akakasirika sana na kumuuliza: kwa nini umenidanganya?
Jamaa: Nimesema ndiyo kwa sababu ningesema hapana ungezama tena na kuibuka na AUNT EZEKIEL na ningesema hapana tena ungezama na kuibuka na MKE wangu alafu ningesema ndiyo ungenipa wote watatu!
Sasa mimi maskini sina uwezo wa kuhudumia wote hao, ndio maana nikasema NDIYO kwa Wema Sepetu.
*FUNDISHO*
Wanaume huwa hatusemi uongo bila sababu na inakuwa sababu maalumu kwa faida ya wote.
WANAUME WOTE NI WAAMINIFU. Hii ndiyo kauli mbiu yetu.
ππππ
Mcheki Chizi na daktari
Tafakari na ujumbe huuuu!!!β¦
DAKTARI :- Unajisikiaje?
CHIZI:-Kila siku naota nyani wanacheza mpira wa miguu.
DAKTARI :- Nitakupa dawa leo hautaota tena.
CHIZI:-hiyo dawa nipe kesho sababu leo wanacheza fainali. na nilibet
ππππ
Recent Comments