Vihoja Vya Kushare
Ameniomba nimfungulie akaunt facebook cheki nilichomjibu
Leo nimechoka zangu alafu shangazi amekuja anataka nimuunganishe facebook. Imebidi nimwambie
lazima awe na picha passport size 4 kwaajili ya kuweka profile picture, barua kutoka kwa afisa mtendaji na Atm card ya nmb bank. Alafu awe na marefa wanne ambao wamekuwa facebook for more than 3 years. Amesema
hataki tena kujiunga fb!
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Saa ivi niko zangu nimelala naendelea kupunguza uchovu
Angalia huyu secretary anavyomjibu bosi wake
Boss mmoja aliingia kazini kwake kasahau kufunga zipu ya suruali yake sasa secretary wake akamfuata na mazungumzo yakawa hivi:
SECRETARY: Boss leo umesahau kufunga geti nyumbani kwakoโฆ
Boss akabaki anashangaaโฆ Baadae wakati anakwenda chooni kujisaidia ile anataka kufungua zipu akaikuta iko wazi ndio akajua alichokuwa ameambiwa na Secretary wake.
Akarudi mpaka kwa secretary na mazungumzo yakaendelea:
BOSS: Bibie ulivyoona geti wazi je uliona benz langu lime paki auโฆ?
SECRETARY: Hapana Boss niliona kitoroli kidogo kimepaki kina matairi mawili
Raha ya kuoa kijijini
Kuoa vijijini raha sana Hata ukiulizwa unafanya kazi gani ukiwaambia mimi ni admin basi daaaah wanaona wewe ni bonge la boss๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Mwizi kawezwa ki kwelii
Et jana usiku mwiz kavunja mlango kwangu akaanza kutafuta kitu kila kona ikabid na mie niamke namuuliza unatafuta nini ananijibu hela ndipo nilipoanza na mie kutafuta nae maana hta hela ya kula Jana sikua nayo alichoka zaid nilipomuliza una uhakika uliweka humu? sipendagi ujinga๐ถ๐ป na kitu hela mm!
Cheka kidogo, angalia anachosema huyu mchaga
Mchaga baada ya kufa akaulizwa na malaika anayetoa roho: Mangi hapa ni njiapanda kulia ni Mbinguni na kushoto ni Jehanamu, Je unachagua kwenda wapi?
MANGI: Bwashee, mi nabaki hapa hapa njiapanda aisee.
MALAIKA: Kwa nini?
MANGI: Aisee, nikifungua duka hapa si nitapata wateja wa Mbinguni na Jehanam. Yani patakuwa senta ya hatari, supu na nyama choma muda wote. Hata we utafaidi, unavyoenda kuchukua roho unaniletea stock nakupa hela yako cash mkononi. Na kila ukipita hapa unapiga mchemsho wako wa ulimi na bia mbili chap kabla ya kuingia mbinguni.
Kwanza nashangaa Shirima alipitaje hapa bila kushika ploti, au alikufa amelewa sana?
Jamaa alikuwa na tabia ya kutembea na binamu yake cheki kilichomkuta
Jamaa alikuwa na tabia ya kutembea na binamu yakeโฆ.
Alikuwa anasubiri mjomba na mkewe walale tu halafu ananyata mdogo mdogo mpaka chumbani kwa binamu yake.
Siku moja umeme ulikuwa umekatika ikabidi aamue kuvua nguo kabisachumbani kwakeโฆ.
Akanyata taratibua akafungua mlango akazama chumbani kwa mjomba ake bila kujua, ghafla umeme ukarudiโฆ
MJOMBA; we mshenzi umefata nini chumbani kwangu tena uko uchi
JAMAA; nimekuja kukuaga kesho naondoka
MJOMBA; ndo uje uchi?
JAMAA; ndio kwasababu nimeshapaki kila kitu kwenye begi
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Angalia alichokifanya huyu mtu baada ya kuokota wallet ya thamani
Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station “naitwa Juma nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki7, ATM card na karatasi yenye PIN ya ATM card na kijimfuko cha dhahabu” Mtangazaji akasema, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe kama anakusikiliza? Jamaa akajibu; hapana, ninaomba kumuombea dedication wimbo wa R.Kelly usemao “U SAVED ME” umfikie popote alipo!!
Hii ndiyo bongo sasa!!
Hii ndio Bongo
Ilikuwa Ijumaa mida ya saa 10 jioni, mzee mmoja aliingia na kibinti kizuri kwenye yard ya magari mapya.
MZEE: Chagua gari unalotaka mpenziโฆ.kabinti akazunguka yard yote mwisho akachagua Verrosa metallic .
BINTI: Mi naitaka hii
MZEE: Hakuna tatizo kabisaaa, mtoto mzuri kama wewe lazima upate gari uloichagua mwenyewe. Mzee akatoa kitabu cha cheki na kuandika palepale na kumpa mwenye yard
MUUZAJI: Sasa Mzee kwa kuwa umetoa cheki, gari utakuja chukua Jumatatu tukishahakikisha kuwa Account yako ina pesa benki. Naomba namba yako ya simu Mzee
MZEE: Hakuna tatizo (akampa namba). Haya twende zetu sweetie Jumatatu tunakuja wote kuchukua gari lakoโฆ
Siku ya Jumatatu mwenye yard kampigia simu Mzee.
MUUZAJI: We Mzee kavu sana, akaunti yako haina hata senti tano.
MZEE: Hilo nilijua, lakini wiki endi yangu ilikuwa tamu sana.
๐ฆ๐๐ฆ
Duh, hii sasa kazi
Wakati unafikiria dingi yako afe ili urithi nyumba, dingi nae anafikiria uanze kufa ili apangishe chumba unacholala.. hiyo inaitwa kufa kufaana.. ๐๐๐๐๐๐๐๐๐ #Hatutaki ujinga
Cheki huyu jamaa anavyoungama kwa padri sasa
JAMAA: Baba Padri nimekuja kuungama
PADRI: Haya
JAMAA: Niliiba kamba
PADRI: Kamba?
JAMAA: Ndio, kamba lakini kule mwisho kulikuwa kumefungwa ng’ombe
PADRI: Kwa hiyo uliiba ng’ombe?
JAMAA: Kiukweli nilikuwa nina lengo la kuiba kamba, kwa bahati mbaya mwisho kulikuwa na ng’ombe
PADRI: Mi naona mueleze Mungu direct, mi sikuelewi kabisaaa
๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Recent Comments