Vihoja Vya Kushare
Namna wazazi wanavyoongea na mabinti katika umri tofauti
Miaka 13: Usipende wavulana ni wabaya.
Miaka 18: Sitaki nikuone na yule mvulana tena!
Miaka 23: Lini utatuletea mchumba wako?
Miaka 26: Wenzio wanaolewa.
Miaka 30: Tumekuambia kwamba acha
kuchagua sana wanaume, hutaki kusikia!
Miaka 33: Kuna mtu wa Mungu yupo kule
anaombea unaweza kupata mchumba
Miaka 36: At least pata mtoto mmoja.
Miaka 39: We will take care of all the wedding
billsโฆyeyote ni sawa sisi tutagharamia kila kitu mwanetu wee mlete tu .
Miaka 45: hivi kweli nani alikuroga.?
๐๐๐ changamkia fulsa umri ukifika
Simu ilivyozua utata
Mama alichukuwa simu akampa mwanawe. Mama..Mpigie babako mwambie chakula tayari. (Mtoto akachukuwa na kupiga) MtotoโฆMama simu ya baba imepokelewa na mwanamke. (Mama kwa hasira) Akirud atanitambua leo. (Baada ya muda kidogo baba akarud,kufika mlangon tu kapokewa na sufuria ya kichwa. Hajakaa vzur mwiko wa pua) Mama..Mwanangu ulipopiga simu ya babako mwanamke wake alisemaje?? Mtoto..Alisema mteja unaempigia hapatikan kwa sasaโฆ..
Nilichokifanya baada ya kualikwa na mchumba wangu kwao
Mchumba wangu amenialika kwao nikawaone wazazi wake lakini akaniambia nisiende mikono mitupuโฆ
Nikaamua kuvaa glovesโฆ
Sipendagi aibu ndogo ndogo ukweni.๐๐๐
Mbele ya hela binti usharobaro achia mbali
Boy:- hallow
Dem:- hellow
Boy:- ivi jina lako nani vile
Dem:- am miss precious A. K. A dope girl
Boy:-Okay, nmekutumia 50,000 nimeona Jina tofauti ngoja nipige customer care
Dem:-no no baby usipige Ah ah Hapana baby mi naitwaย Andongolile Mwakasakafyukaย ๐๐๐๐๐
Wazo la jioni hii
๐ขWAZO LA JIONI HII ๐ข
KAMA MWAKA JANA ULIPIGA HATUA NA HUJAFIKIA MALENGO MWAKA HUU PIGA MSAMBA๐
Je, Chuoni kwako Kukoje?
FACT!
1.Ukiona geto lina feni, sabufa, meza ya plastic na kitanda ch sita kwa sita na Pc UJUE ni jamaa wa UDSM.
2. Ukaona geto lina nguo nyingi za watu tofauti tofauti, unga mwingi, vtunguu vng, nyanya halaf pembeni, Vitabu vya kutosha na lundo la karatasi za betting ujue huyu JAMAA ni wa SAUT.
3. Ukaona geto halina kitu ndani zaidi ya mkate wa bakheresa na kopo la maji UJUE huyu jamaa ni wa UDOM๐โ
4. Ukaona geto lina visamaki vikavu mezani, Notes za kutosha mezani na jaba pembeni UJUE huyu ni MJAMAA WA MWENGE/MWECAU๐๐ค
5. Ukaona geto lina Mawigi mengi na dressing table pembeni, ngazi ya kuwekea viatu UJUE huyu mjamaa ni wa RUCO IRINGA๐
6. Ukaona geto lina spray za kila aina, Nguo nyingi hasa za mitumba ambazo zimemodolewa mpaka tight UJUE huyu MJAMAA ni wa USHIRIKA MOSHI.
7.Ukiona geto lina Nyanya na mikungu ya ndizi halafu halafu nje kuna jiko la Mkaa UJUE huyu mjamaa ni wa TEKU mbeya๐ณ
8. Ukiona geto lina tranka na nje wamevulia buti, viatu vya matope UJUE huyu Mjamaa ni Wa SMUCO MWIKA.
9. Ukaona geto ndan mashuka ya kimasai kinabao, hapa usipatwe na Mashaka, Jua huyu ni Mjamaa wa MAKUMIRA. ๐๐๐๐
10. Ukaona geto lina vimodo, vimini, miwani za tittled, jiko la mafuta ya taa, kitandani mito zaidi ya Minne,Visarafu kwenye meza, Tshirt nyingi za semina za family planning, Ukimwi n.k halafu chini tv ya chogo na king’amuz cha continental Ujue huyu MJAMAA ni wa TIA DSM ๐ฑ๐ฑ๐ฑ๐ฑ๐ฑ๐ฑ๐ฑ
โฌโฌโฌโฌโฌโฌโฌโฌโคตโฌ๐๐๐๐
JE, KWAKO KUKOJE? ???
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Duh! Wanaume jamaniโฆ
Lakini sisi wanaume hatuko fair โฆ Yani demu anang’ng’ana kujipodoa uso na sisi tunaangalia matako. ๐๐๐mungu anatuona jaman๐๐๐๐๐๐Makeup ya matako iletwe
Eti kwa nini Watu hawapostigi hii? Hata selfie sijaonaga
Vijana mkiwa mnaendesha magari mna post mukiwa mpo beach mna post mkiwa kwenye masherehe mna post Lakin mkiwa mmeenda kwa mganga siwaoni kupost mitunguli na vibuyu vya mganga unakuwa je wa zee tena. ๐๐๐๐
Padri Akimbia wakati wa kuungamisha, chanzo ni hiki
Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani
peke yake.
Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa
pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama
{confess}
“Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya
dhambi kubwa sana.”
Padri, “Endeleaโฆ”
“Bosi wangu aliniita nyumbani kwake, akaniambia
amegundua nimeiba shilingi millioni 100 kazini. Akasema
nisipozitoa atanipeleka polisi, sa kwa ukweli mi naogopa
kufungwa.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu,nikatoa bastola nikamuuaโฆ.. Yesu atanisamehe?”
Padri: “Utasamehewa.”
“Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango
unafunguliwa kutazama, Loh! Mke wa bosi, alipoona
kilichotokea akasema anapiga polisi simu.
Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuua na yeye piaโฆ Yesu atanisamehe hilo?”
Padri: “Utasamehewa.”
Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke, lakini mlinzi
akakataa kunifungulia, ati amesikia mlio wa
bastola. Nikaona ataniletea kizuizi huyu.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuuaโฆ.. Yesu atanisamehe?”
Padri:”Utasamehewa.”
“Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda
nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi
akabisha hodi, nikawaza mambo gani tena, akasema alirudi
nyumbani na kukuta yaliyotokea akanionesha diary ya
babake, inayoonesha nilikuwa na appointment naye
wakati nilipomuua. Nikamuuliza nani mwingine anayejua?
Akasema ameanzia kwangu kisha anaenda polisi.
Nikatazama huku na huku nikakuta tuko wawili peke
yetu, nikamuuaโฆ.. Yesu atanisamehe na hilo?”
Kimyaaโฆ.
“Padri yesu atanisamehe?”
kimyaโฆ.
Jamaa akatazama kwenye confession booth padri
hayupo, lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo
za mapadri linatikisika. Kufungua akaona padri kajificha ndani anatetemeka huku akitokwa na jasho.
Jamaa, “Sasa baba mbona umekimbia?”
Padri kwa taabu akajibu, “Nilitazama huku na huku
nikagundua tuko wawili peke yetuโฆโฆ.”
Angalia pombe ilichomfanya huyu jamaa, kweli pombe haimuachi mtu salama
Leo nimeiogopa pombe.
Nimetokea kuiogopa pombe baada ya kumwona jirani yangu akicheza muziki kwa sauti ya jenereta langu, akidhani yuko clubโฆ..nkamsikia anasema “wee dj noomaaaa”
Baada ya kuzima jenereta akaniuliza uo mziki kaimba nan?
Nlivyokuwa na roho mbaya Nikamwambia iyo ni collabo ya Yamaha na Petrol
๐๐๐๐๐
Recent Comments