Vihoja Vya Kukupa Mudi Mpya

Wadada acheni hizo

Mfalme Sulemani alikuwa na wake 700 na alichepuka(cheated)na vimada 300 . Mpenzi wako/Mume wako unamfumania na kimada mmoja tu ugomvi na amani imapotea ndani ya nyumba,unasimulia kuanzia padri,mchungaji,ukoo wako mzima,mashoga, stress,vidonda vya tumbo,inapelekea mpaka unaokoka,eti kisa kamuonjesha mmojaโ˜ sasa akionjesha 700 si utakutwa Mirembe๏ฟฝ

Wadada acheni HIZO
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚.

Cheka kidogo, angalia anachosema huyu mchaga

Mchaga baada ya kufa akaulizwa na malaika anayetoa roho: Mangi hapa ni njiapanda kulia ni Mbinguni na kushoto ni Jehanamu, Je unachagua kwenda wapi?

MANGI: Bwashee, mi nabaki hapa hapa njiapanda aisee.
MALAIKA: Kwa nini?
MANGI: Aisee, nikifungua duka hapa si nitapata wateja wa Mbinguni na Jehanam. Yani patakuwa senta ya hatari, supu na nyama choma muda wote. Hata we utafaidi, unavyoenda kuchukua roho unaniletea stock nakupa hela yako cash mkononi. Na kila ukipita hapa unapiga mchemsho wako wa ulimi na bia mbili chap kabla ya kuingia mbinguni.
Kwanza nashangaa Shirima alipitaje hapa bila kushika ploti, au alikufa amelewa sana?

Angalia huyu jamaa alivyowafanyia watu uhuni bar

Jamaa kaingia Bar;
Jamaa: Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji, maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji. Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,

Jamaa: Muhudumu nipe supu na kila mtu humu ndani mpe supu maana ninapokunywa supu kila mtu lazima anywe supu. Watu wakapewa supu tena safari hii wakapiga makofi.
Jamaa: Muhudumu nipe bili, na kila mtu humu ndani mpe bili maana wakati nalipa bili yangu kila mtu lazima alipe yake. Zogo lilianzia hapoโ€ฆโ€ฆ.

Ufugaji wa nguruwe kazi, Cheki jamaa hawa wake walivyompa mtihani

MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalishanini?
.

MFUGAJI: Nawalisha mabaki ya chakula toka migahawa mbalimbali
.
MWANAHARAKATI: Hayo ni makosa unawatesawanyama kwa kuwalisha chakula kichafu. Akapigwa fainiโ€ฆ Baada ya siku chache wakaja wanaharakati toka Umoja wa Mataifa
.
MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalisha nini?
.

MFUGAJI: Huwa nawaanzia siku na uji wa ulezi, halafu mikate, mchana ugali kwa kabeji na usiku viazi
.
MWANAHARAKATI: Loh watu wanakufa kwa njaa wewe unalisha nguruwe, akapigwa fainiโ€ฆ.siku chache baadae wakaja wanaharakati wa Mazingira
.
MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalisha nini?
.
MFUGAJI: (Kwanza akasita kidogo) Hawa huwa nawapa shilingi alfu tano kila mmoja kila siku halafu wao wenyewe wanaenda kununua chakula wanachokitaka.. .

Cheki huyu mwanamke anavyomkomoa mme wake baada ya kumsaliti

MKE: Mbona unanukia pafyumu ya kike?
MUME: Yaa kuna mwanamke tulikuwa tumeminyana ndani ya daladala
MKE: Na lipstiki kwenye shati?
MUME: Tulikumbatiana na wageni toka Zambia walitembelea ofisi yetu
MKE: Na ile kondom iliyotumika kwenye mfuko wa suruali?
MUME: Bwana ee acha maswali ya kijinga mi nalala nina usingizi
MKE: Lazima niulize mie huwa nahakikisha nimeacha kila kitu hukohuko ndio narudi nyumbani
MUME: Umesema nini wewe?
MKE: Bwana ee acha maswali ya kijinga mi nalala nina usingizi. ๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„

Huyu jamaa kawaweza wapenda vya bure

Jamaa kaingia mgahawani kwa fujo
JAMAA :ย Nipe soda moja na kila mtu mpe yake maana ninapokunywa soda napenda kila mtu anywe
WATU :ย Ha! Ha! Ha! Haaaa!
JAMAA :ย Nipe mchemsho na kila mtu mpe wa kwake maana ninapokula mchemsho napenda kila mtu ale wake
WATU:ย Watu weweeee! Tena safari hii Na makofi juu..
JAMAA :ย Mhudumu, nipe bili na kila mtu mpe yake maana ninapolipa bili napenda kuona kila mtu analipa yake
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

MAJIBU YA MAKONDA WA DALADALA ZETU GONGOLAMBOTO HUKU

1. wewe Dada unaturingia nini na matiti yako mawili , mbwa pia ana matiti nane na haturingii eboo !!!!

2. Ka wafikiri Una haraka sana Shuka ukimbie.

3. Nauli kulipa lazima ,Chenji ukikumbuka.

4. Kutapika ndani ndani ya Daladala fain 250/= ,ukijamba pia 250/= ,Sasa jamba tukujue viti vina alarm!โ€ฆ

5.Hatujasema wewe ni Mnene ila Ukikalia SITI mbili Lipiaโ€ฆ.

6. Hio Elfu kumi yako nenda nunua avocado upake alafu uteleze hadi posta ,nauli ya daladala ni 350/=.

7. usifungue dirisha ungetaka upepo ungepanda pikipiki..

8. wewe Dada hebu sogea hukoo, Unaringa nini wakati asubuhi hii umeoga na sabuni ya kuoshea vyomboโ€ฆ

Kilichotokea baada ya kuzamia sherehe

Pale unapozamia kwenye Dinner Party ya Jumuiya Fulani, sasa Lengo la Jumuiya hiyo ni kupata Fedha za kutunisha Mfuko wa Jumuiyaโ€ฆsasa unakakaa mbele kabisa ili Muda wa Msosi usichelewe na kukuta kwenye Buffee yamebaki maharage!

MC : “Papai zuri kabisa kutoka Newala, Papai Mwendokasi, hili ni Shilingi laki 1..jamani Papai,nipeni ofa!”

MOSHA : “Laki 3 hapaaa!”

“Jamani laki 3 pale kwa Mosha, Papai linaondoka jamani, papai hili ni self contained kabisaโ€ฆ.papai jamani”

KIBOLIBO: “Milioni 1 hapaaa”

“Jamani Mambo yanazidi kunoga hapa!โ€ฆBenedict Kibolibo anataka papai kwa milioni 1 jamani, linaondoka papai!”

RWEYEMAMU : “nitanunua Papai hilo kwa Milioni 5”

Haya sasa jamani Rweyemamu ametoa ofa ya Milioni 5 Jamani, nani mweingineee?”

Kimyaaaโ€ฆ

Haya jamani Papai kama hakuna Ofa basi Papai linakwenda kwa Rweyemamu!โ€ฆโ€ฆ..haya sasa Kuna Kuku hapa Jogoo kabisa, bei yake ni laki 6 jamani Jogoo twitter huyu!”

WEWE “Milioni Mojaaa!”( hapa umejiwahi wa kwanza na wewe uonekane upo huku ukijua kabisa Wakina Mosha na Rweyemamu lazima watampandia Dau Jogoo, tena dau kubwa”

MC: ee sasa Kumekucha Jamani, Kabasele anamtaka Jogoo kwa Milioni 1 jamani!โ€ฆ.ofa nyingineeee!”

Kimyaaaโ€ฆ

Jamani Jogoo anakwenda kwa Kabasele jamani!โ€ฆofa nyinginee!

Kimyaaaโ€ฆ.

Kimyaaaโ€ฆ.

๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜โ€ฆhapa sasa ndio mfukoni kuna Buku jero,..huko kwengineko NMB nill balanceโ€ฆsasa unageuza mimacho kumtazama Mosha kama atapanda dau kwa jogoo๐Ÿ‘€(mama wee Mosha anachezea Simu!)โ€ฆ..unamtazama Rweyemamu (teh anatafuna Kuku)โ€ฆ..mama weee๐Ÿ˜

MC: Haya jamani kama hakuna Mwingine basi zoezi letu liishie hapa na limekwenda kwa Mafanikio, Mpatieni Kabasele Jogoo wake!

Hapa sasa unapokea jogoo wako wa MILIONI kwa Tabasamu la Maitiโ€ฆ.kule nyumbani Jogoo wako Mkubwa unauza elfu 20 lakini sasa haka kajogoo kapya Mkononi kanakuwa kazito utadhani umembeba John Cena๐Ÿ‘€โ€ฆMama weee hapa sasa vidari ulivyotafuna unaviona kama vimerudi kwenye Ulimiโ€ฆ.Chicken wings zinataka kutokea Masikioniโ€ฆ..Uuuuwiiiii,๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜

Na hapa sasa kabla Dinner haijaisha ndipo unapojikuta Umebuni Cocktail ya Sparetta na Tomato๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜‚.
chiel wie okee

Kuwa na mahusiano na msichana kama huyu ni changamoto, Mabinti bwana!

Binti: Hallow mpenzi, Mambo

Jamaa: Poa baby

Binti:Uko wapi?

Jamaa: Niko town napata lunch

Binti: Wow unarudi saa ngap? Nina njaa dear naomba uniletee msosi

Jamaa: Narudi baada ya nusu saa nikuletee nini?

Binti: Niletee chipsi kuku, soseji, mayai manne ya kukaangwa pembeni, baga, piza, coke take away baridi, mkate wa moto kwenye ile bekari ya wapemba na maji ya kunywa ya kiimanjaro.

Jamaa:Umesahau viti, meza, masufuria, sahani na beseni na vijiko.

Binti: Kwanini dear?

Jamaa: Naona hutaki kula unataka kufungua hoteli!

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About