Vihoja Vya Kukupa Mood Mpya

Angalia kilichojiri katika semina ya wanandoa kuhusu upendo

Kulikuwa na semina ya wanawake kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa.
Mwalimu aliwauliza ni wangapi wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha mikono kama ishara ya kuwa wanawapenda waume zao.
Mwalimu akauliza tena, “Ni lini mara ya mwisho umemwambia mumeo “Nakupenda Mpenzi”?

Majibu yalikuwa kama ifuatavyo:
Wengine wakisema Asubuhi ya leo,
Wengine jana,
Wengine wiki iliyopita
Wengine mwezi uliopita
Na wengine wakasema hawakumbuki!
Mwalimu aliwapa kazi kila mwanasemina achukue simu yake na kumtumia mume wake meseji yenye neno “NAKUPENDA MPENZI”
Baada ya meseji kwenda aliwaamuru kubadilishana simu kila mtu na jirani yake.
Kila mwanasemina aliambiwa kusoma meseji za majibu kwenye simu aliyoshika

Simu ya 1 – “Samahani, nani mwenzangu”!
Simu ya 2 – “Samahani, wrong number”!
Simu ya 3 – “Si nimekuambia usinitumie messages kwenye namba hii”!
Simu ya 4 – “Mh! leo mvua itanyesha”!
Simu ya 5 – “Nikija tutaongea zaidi”!
Simu ya 6 – “……Imedhibitishwa umepokea Tsh300,000 kutoka kwa ……”!
Simu ya 7 – “Me too”!
Simu ya 6 – “Huu ujumbe ndio ulikuwa unamtumia huyo hawara yako ee, leo utanikoma”!

Huyu mchungaji ni noma, cheki alichomwambia pedeshe

Mchungaji kamfuata pedeshe moja maarufu kwa
kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki;
MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za
kujenga kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa
mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na Mungu
atakubariki zaidi

PEDESHE: Samahani Mchungaji haitakuwa vizuri
mimi kuchangia kanisa, fedha zangu ni haramu,
huwa nazipata kwa utapeli na kuuza madawa ya
kulevya.
MCHUNGAJI: Yote ni heri, pesa yako tutatumia
kwa kujenga eneo la choo we toa tu!!!

Ungekua wewe ni mwalimu ungemshauri nini huyu mwanafunzi?

Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.

MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?

JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.

MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?

ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga.

MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.

MWAL: Na wewe James??

JAMES: mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiwe……”

Akameza mate kisha akaendelea….

“Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali.”

MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??

JENNY: Nataka kuwa mke wa James.!!

Shopping Cart
19
    19
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About