Tenda Wema Uende Zako
Nimekuta panya ana struggle kuingia chini ya mlango wa jirani yanguโฆ
Nikagonga mlango Jirani kafungua panya akapenya mi nkaenda zanguโฆ..
Tenda Wema Uende Zako!!! Sipendi Ujinga mimi kwanini panya wa watu apate shida
Nimekuta panya ana struggle kuingia chini ya mlango wa jirani yanguโฆ
Nikagonga mlango Jirani kafungua panya akapenya mi nkaenda zanguโฆ..
Tenda Wema Uende Zako!!! Sipendi Ujinga mimi kwanini panya wa watu apate shida
Kuna siku nilichalala kipesa nikaamua kuomba dem wangu aniazime 10,000/= akanipa.
Baada ya siku mbili nikapata pesa zaidi ya laki nne hivi, nikaamua kumpa 100,000/= mpenzi wangu bila yeye kuniomba.
Baada ya siku 3 akaja kuniambia:- “Bae, ile 10,000/- niliyokuazima mwenyewe amekuja kunidai, so kama unayo naomba unipe nimrudishie maana ananisumbua leo siku ya 3.”
SAA HIZI NIPO ZANGU SINGLE NATAFUTA DEM MWINGINE
BABA: mwanangu kwenye huu mtihani uliofanya natumaini utafanya vizuri.
DOGO: ndio baba nitapata mia kwa mia.
BABA: kwanini unasema hivyo?.
DOGO: kwasababu jana kanisani tulifundishwa “Yesu ni jibu” kwahiyo kote nimejaza Yesu.
BABA: kwel kazi ipo
JE UNGEKUWA WEWE HUYO NDO MWANAO UNGEMFANYAJE?
Wanafunzi waliulizwa na mwalimu nani angependa kwenda peponi? Wote wakanyosha ila mmoja tu alipokwenda nyumbani akamuelezea mamake, mamake akamuuliza je wewe ulinyosha mtoto hapana mama yule mama akamuuliza kwanini.
mtoto kwa sababu mama uliniambia nikitoka shule nije moja kwa moja mpaka nyumbani nisiende kokote
Jamaa kavamia semina ya wasomi iliyokua inafanyika maeneo ya ubungo plaza bas wakaanza kujitambulisha
1. Naitwa Anna niko SUA mwaka3 nasoma agriculture
2. Naitwa Stella niko UDSM mwaka2 nasoma public relation
3. Naitwa Emmanuel niko UDOM mwaka3 nasoma computer science
bas jamaa nae akainuka kwa kusuasua huku akijishtukia akasema”Naitwa Elisha niko Tanesco mwaka wa 7 nasoma mita”
Mwanamke wakizaramo: Unampa hela ana nunua dela anaenda ana msutia jirani, analivaa dela bila nguo ya ndani mbele yako, unazidiwa anakupa kitu fresh unatoka unatabasamu.๐ค๐ฝ๐๐ฝ
Mwanamke wa kitanga:
Unampa hela anapika vitu mtaa mzima unasikia harufu ya chakula, chenji inayo baki ananunua kinga ukirudi unakula afu unakula..๐๐ผ๐๐ผ๐ค๐ฝ๐๐ฝ
Mwanamke wa kihaya:
Unampa hela ukirudi unakuta majirani wote wanataarifa kuwa wew uliacha hela, anakupkia vitu vzuri, usiku anakuhudumia ukimsifia anakuhudumia tena hata mara nne kwa usiku mmoja..we mle sifa tu๐๐ฝ๐๐ฝ๐คธ๐พโโ๐๐ฝ.
Mwanamke wa kichaga:
Unampa hela anaenda ananunua dagaa anapika na michuzi mingi mpaka dagaa wanafufuka unakula kwa shida, dagaa wanakula utumbo wako unakufa.. Madaktari wanajitahidi wanakutibu unafufuka. Ukiwa hujapata akili vizuri anakuletea bili ya umeme, anakukumbusha deni la kwa Massawe, anakukumbusha kodi ya nyumba.. *Unashikwa na presha unakufa moja kwa moja*๐๐ฝ๐๐๐ผโโ๐๐พ๐คธ๐พโโ
Mapenzi ni balaa
Mapenzi ujue yanawez kukupa stress adi mama ako akikuuliz what’s wrong๐ค-โunawez kumjib MAMA WE BADO MDOGO UWEZ ELEW๐คฃ๐คฃ๐คฃ
PAMOJA NA HALI NGUMU YA UCHUMI NCHINI HUWEZI AMINI MSHAHARA WA DHAMBI HAUJABADILIKA HATA KIDOGOโฆBADO NI MAUTI VILEVILE
๐๐๐๐
WALEVI WAWILI KATIKA MAZUNGUMZO YAO
MLEVI 1ย hivi rafiki yangu china ni mbali kweli
MLEVI 2ย sidhani mbona pale kazin kuna mchina anakuja na baiskeli
๐๐๐๐๐
*Jihadharini* na wachapaji wa kadi za harusi. Hakikisha unasoma maandishi yaliyochapwa kabla ya kadi kuchapwa na kusambazwa!
Mchapaji aliombwa aweke 1 Yohana 4:18 katika kadi ya harusi lakini mchapaji kwa makosa aliweka Yohana 4:18.
1 Yohana 4:18 panasema, “Katika pendo hakuna hofu, lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofuโฆ”
Lakini Yohana 4:18 tunasoma, “Kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako.”
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐_MKE MTARAJIWA AKAZIMIA HAPA, TUNAMPEPEA_
*TEACHER*: _nielezee biashara ambayo imefeli kutokana na uzembe
*STUDENT*: Changudoa akipata mimbaโฆ
*TEACHER*: _get Out!!!!!!!!!!!!!!_
๐๐
Mume kaingia duka la nguo na kamnunulia mke wake chupi dazeni moja zote za rangi nyeusi, akaenda kumzawadia. Mpenzi akashukuru lakini alipogundua kuwa zote ni nyeusi si akaropoka.
MY HONEY: Sasa umeninunulia chupi zote nyeusi, sasa watu si watadhani nina chupi moja tu sibadili,
Jamaa alifura akawa kama mbogo na hapo ndipo zogo kuu lilipoanza
MUME:Watu gani hao watakaokuambia unachupi moje, inamaana unawaonyesha kitumbua changu? Leo utanambia’
Ungekuwa wewe ungefanya nini?
NIMEKAA NIKAWAZA ๐๐ผ KUWA KUNA MAMBO KAMA MATATU HIVI๐๐ป WAAFRIKA HATUYAJUI ๐
KAMA TUNGEKUWA TUNAYAJUA HATA HAWA WAMAREKANI,๐บ๐ธWACHINA๐ฏ๐ต NA HATA WATU WA ULAYA TUNGEKUWA๐ฝ๐ช TUNAWAPITA KIMAENDELEO
MAMBO YENYEWE,,
HATA MIMI SIYAJUI MAANA NA MIMI NI MWAFRIKA ๐๐๐๐
Chizi kakaa ukingoni mwa bahari analia kwa masikitiko na huku kakamata kijiko cha chai. Mwezake akamuuliza mbona unalia mwenzangu. Chizi akajibu nimetia vijiko vitatu vya sukari baharini, kila nikionja bado ina chumvi. Mwenzake akacheka sanaaaaaa akamwambia. Hujakoroga!!!!๐๐๐๐๐๐
MASSAWE alienda na marafiki zake bar kunywa, baada ya kumaliza kutumia akaletewa bili kama ifuatavyo:
Manka 35,000
Marieta 20,000
Kekuu 30,000
Kitime 15,000
Kinabo 10,000
TOTAL 110,000/=
MASSAWE akaicheki akasema “Wote nitawalipia lakini huyo “TOTAL” Yesuu simlipii.
Kwansa anamiliki sheli kibao sa mafuta hapa bongo. Shensi taip ! Na amekunywa nyingi kuliko wote alipe mwenyeweโฆ
Akina dada mpenzi wako akikuita MAMITO usikubali
na yeye mwite MAFORONYA kama mbwai na iwe mbwai๐คช๐คช๐คช๐คช๐คช๐คช
Zuzu: Mambo Anna!
Anna: Poa!
Zuzu: Kuna kitu nataka nikuonyesheโฆ
Anna: Kitu gan?
Zuzu: Twende chumbani kwako (wakaenda)
Anna: Haya nionyesheโฆ
Zuzu: Funga mlango na madirisha kwanza (akafunga)
Anna: Haya nionyeshe sasa!..
Zuzu: Zima taa kwanza (akazima)
Anna: Mhmโฆnionyeshe sasa!
Zuzu: Haya njoo hapa kitandaniโฆ
Anna: Ok, nionyeshe!
Zuzu: Ona nimenunua saa ambayo inawaka yenyewe gizaniโฆ Acha mawazo mabaya ww???
Tukiwa kanisani mdada alikuwa amelala , akaamka akasikia Pastor anasema
” SIMAMA”
Yule dada akasimama akashangaaa kanisa zima linamtizima kwa mshangao akiwemo mumewe, akaangalia kanisa zima akashtuka kujiona yeye peke yake ndiye aliesimama
Pastor akaendelea vizur endelea kusimama, tumepata mmoja hadi sasa aliyesimama narudia kwa mara ya mwisho kama hujasikia vizuri
” kama wew umewahi kumsaliti au bado unasaliti ndoa yako SIMAMA”
Binti akazimia
Recent Comments