Vihoja Vya Kujienjoy Leo

Mlevi kazua tafrani, angalia alichokifanya hapa

MLEVI mmoja aliingia baa akavuta kiti na kukaa mhudumu akatokea kumsikiliza.
MHUDUMU: Nikusaidie nini?
MLEVI: Eeh! nipe bia ya baridi kisaha wasikilize wote waliokaa hapa, wape bia na wao maana sipendi kunywa pombe wengine wananiangalia
Akaja mhudumu wa jikoni “nikusaidie nini?”

MLEVI: Niletee supu kisha wasikilize wote waliokaa hapa na wao wape supu sipendi kunywa supu watu wananiangalia
Safari hii watu wakapiga makofi
Baadae akamuita mhudumu
MLEVI: Niandikie bili zangu kisha waandikie wote bili zao sipendi kulipa huku watu wananiangalia

Wale wateja wakamvaa na kumshushia kichapo… teh teh teh teh teh hii kali hakuna cha bure mjini hahahaha na jasho la mtu haliliwi wandugu

Cheki huyu mzee alichomfanyia muuzaji wa pharmacy

Mzee kaingia pharmacy,
MZEE: Mambo mwanangu, kuna kitu naomba uonje nitakulipa
MFAMASIA: Kitu gani?….Mzee akatoa kichupa na kijiko akaweka …majimaji yaliyomo kwenye
kichupa kwenye kijiko na kumwambia mfamasia aonje, mfamasia akatia yale maji mdomoni na kuyazungusha zungusha mdomoni akionja;

MZEE: Nipe jibu, ina utamu wa sukari au chumvi au pilipili?
MFAMASIA: Kama chumvichumvi
MZEE: Hakuna sukari
MFAMASIA: Sukari hakuna kabisa
MZEE: Loh asante chukua hii alfu tano nashukuru sana, dokta alinambia nipime mkojo wangu kama nina kisukari, kumbe sina asante bwana mdogo

Hii ndio ndoto ya harusi ya kila msichana anayotamani

GIRL: Baby, hebu niambie harusi yetu itakuwaje?
BOY: Yaani hii haijawahi kushuhudiwa, ngoja nikupe kionjo kidogo tu
GIRL: Enhee…
BOY: Kwanza siku ya kupeleka mahari nitaswaga zizi zima la ng’ombe napeleka kwa babu yako
GIRL: Ooh baby u care..
BOY: Siyo hivyo tu, baba yako ntamnunulia Range Rover Sport na mama mkwe ntampa Range Rover Evoque
GIRL: Baby u are awesome…
BOY: Halagu mdogo wako wa kiume ntampa Prado Tx, na hapo nimesukutua tu mdomo sijaanza kula….
GIRL: Enhee…na sisi??

BOY: Sisi tutachukua mtaa mzima Oysterbay, kila wiki tutaishi nyumba tofauti
Halafu siku ya harusi yetu tutakodi zile meli zinabeba makontena ndiyo iwe ukumbi wetu, itatupeleka hadi Maldives
GIRL: Baby I love you
BOY: Tukitoka hapo tunaenda honeymoon Bahamas….halafu tunaenda Taiwan shopping ya fenicha, kisha Japan shopping ua electronics, halafu tunaenda Dubai nikununulie vito vya thamani
GIRL: Ooh my sweetheart…halafu tukitoka huko??
BOY: Tukitoka huko nachukua ndoo ya maji nakumwagia uzinduke usingizini na ndoto yako imeishia hapo

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About