Vihoja Vya Kujienji Leo
Ujanja alioutumia msichana wa kazi ili apandishiwe mshahara na mama mwenye nyumba
Msichana wa kazi alitaka mama mwenye nyumba ampandishie mshaharaโฆ.. Mama mwenye nyumba akamwambia msichana ampe sababu tatu za kutaka kupandishiwa mshahara.
Msichana: Napika vizuri kuliko wewe.
Mama: Nani kakuambia?
Msichana: Baba kaniambia.
Mama: ok. Sababu ya pili?
Msichana: Napasi nguo vizuri kuliko wewe
Mama: Nani kakuambia na hili?
Msichana: Baba pia kaniambia
Mama: ok, na sababu ya tatu?
Msichana: Najitahidi kitandani kuliko wewe.
(Hapa mama kaonekana kutaka kujua zaidi na akawa tayari kujiandaa kumrukia akate kichwa cha binti mara moja)
Mama: Mume wangu kakuambia na hili pia?
Msichana: Hapana ni Shamba boy kaniambia mimi najitahidi kitandani kuliko wewe.
Mama: Tafadhali punguza sauti baba yako asisikie. Nitakupandishia mshahara wako mara tatuโฆโฆ.
Mambo ya mke na mume haya, chezea mchepuko!?
Mume akamwambia mke wake:
“Funga macho yako tufanye maombi”
Akaanza kwa Kimombo:-
“โฆ Lord I pray for Grace, I pray for Mercy, I pray 4 Joy, I pray 4 Love, I pray 4 Hope, I pray 4 GLORY, I pray 4 Faith, I pray 4โฆ.”
Mke akadakia, “Unadhani mimi sina ee” akaanza:-
I pray 4 Felix, I pray 4 Temu, I pray 4 Rweyemamu, I pray 4 Masawe, I pray 4 Benson, I pray 4 Onyango, I pray 4 Swai, I pray kwa wote niliowasahau!!
Chezea mchepukoโฆ!!
Wazo la asubuh – penzi la kuku
Wazo la asubui
๐Penzi la kuku sekunde 2 ila vifaranga kibao.Lakini binadamu masaa kibao mtoto 1 au 2. Sasa binadam na kuku nani JEMBE? Ukimwona JOGOO popote piga SALUTI!๐๐๐๐๐๐๐๐ukinuna poa tu!!!!!๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Huyu dogo nimsaidieje? Cheki alivyojichanganya
Nimekutana na dogo mmoja hivi hapa analia,namuliza analia nin??ananambia ”ALIPEWA MIA TANO ZIPO MBILI,MIA TANO MOJA YA NYANYA na MIA TANO NYINGINE YA VITUNGUU sasa KAKOSEA KAZICHANGANYA HAJUI TENA IPI NI YA NYANYA na IPI NI YA VITUNGUU!!!
.
.
NA PESA ZOTE ANAZO KAZISHIKA MKONONI,
Haya ndiyo madhara ya kutowapeleka watoto kanisani โช
MTOTO aliibiwa yeboyebo KANISANI akawa analia sana kwa uchungu mpaka MCHUNGAJI akamwambia usilie mwachie MUNGU. MTOTO akajibu Mungu hazimtoshi zile yebo ni ndogo! Usicheke,
Huu ni Mtihani Tuwapeleke Watoto KANISANI Wamjue MUNGU.
Ulevi noma! Angalia huyu mlevi alichomfanyia huyu jamaa usiku! Ungekua wewe ungefanyaje?
Jamaa alikuwa amelaa na mkewe saa tisa ya usiku akastuka baada ya kusikia mtu anabisha hodi kwenda kufungua mlango
Akamkuta jamaa kalewa sana mlangoni kwao
JAMAA: Nini tena mheshimiwa kuamshana saa hizi?
MLEVI: Naomba uje unisukume.
Jamaa akiamini kuwa pengine kuna gari la huyu mlevi limezima jirani akamwambia subiri nikavae viatu. Baada ya kuvaa viatu akatoka na wakaanza kusindikizana na mlevi. Mlevi akaongoza njia
mpaka kwenye mabembea ya jirani akakaa kwenye bembea moja na kumgeukia jamaa na kumwambia.. Okay nisukume basi.
Mkwe kazua mpya, Hii dunia ina mambo sana
Mama mkwe alimuuliza mkwewe “binti” samahani mbona mtoto hajafanana na mwanangu kabisa?
Binti akajibu, “bila samahani mama huku chini nina njia ya uzazi sio mashine ya photocopy”
mama mkwe hoii!! Chezea Wakwe Wa Bongo wewe.
Mambo ya pesa haya..
MAMBO YA FEDHA AISEEโฆโฆ. Kuna jamaa alipewa shilingi 983628763600/= โฆacha uvivu, najua hujasoma ni kiasi gani hicho cha fedha na mbaya zaidi hujagundua kwamba katikati ya namba hizo kuna herufi Aโฆ safi sana, najua umeangalia tena kuiona hiyo herufi, bahati mbaya hujaiona. ๐๐๐๐๐๐๐
Recent Comments