Vihoja Vya Krismass

Hii mitoto mingine mijinga, cheki alichokifanya huyu

Nimeamka asubuhi nikiwa na elfu 1 tu mfukoni, nikamtuma mtoto wa jirani akaninunulie maandazi nipate kunywa chai. Baada ya muda namuona anarudi huku analamba askrimu ya AZAM kama Simba vile. Nikamuuliza maandazi yako wapi? Akanijibu eti wakati anafika yanapouzwa maandazi akagundua kuwa kapoteza hela yangu, hivyo akaanza kurudi, ila bahati nzuri wakati anarudi ili kuja kunitaarifu kuhusu kupotea kwa hela yangu, njiani akaokota elfu 1 ambayo kuna mtu alipoteza ndio akaamua kununua askrimuโ€ฆ.kwa sasa niko polisi na mtoto yuko dispensari na mamake๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€

Cheki huyu mzee alichomfanyia muuzaji wa pharmacy

Mzee kaingia pharmacy,
MZEE: Mambo mwanangu, kuna kitu naomba uonje nitakulipa
MFAMASIA: Kitu gani?โ€ฆ.Mzee akatoa kichupa na kijiko akaweka โ€ฆmajimaji yaliyomo kwenye
kichupa kwenye kijiko na kumwambia mfamasia aonje, mfamasia akatia yale maji mdomoni na kuyazungusha zungusha mdomoni akionja;

MZEE: Nipe jibu, ina utamu wa sukari au chumvi au pilipili?
MFAMASIA: Kama chumvichumvi
MZEE: Hakuna sukari
MFAMASIA: Sukari hakuna kabisa
MZEE: Loh asante chukua hii alfu tano nashukuru sana, dokta alinambia nipime mkojo wangu kama nina kisukari, kumbe sina asante bwana mdogo

Kilichotokea Baada ya mlevi na mchungaji kukutana

MCHUNGAJI; “Unakunywa bia!?
MLEVI; “Ndio.
MCHUNGAJI; “Kwa siku unakunywa bia ngapi!?

MLEVI; “Nakunywa bia tano!
MCHUNGAJI; “Bia moja bei gani!?
MLEVU; “2500/
MCHUNGAJI; “Ulianza lini kunywa bia!?
MLEVI; “Miaka 18 iliyopita!

MCHUNGAJI; “Kwa hiyo kwa siku unatumia zaidi ya 10,000??
MLEVI; “Ndio!
MCHUNGAJI; “Kama u gekuwa unatunza hiyo pesa 10,000 kwa siku leo hii si ungekuwa na Range Rover!?
MLEVI; “Samahani, naweza kukuuliza swali!?
MCHUNGAJI; “Uliza!
MLEVI; “Unakunywa bia!?
MCHUNGAJI; “Hapana!
MLEVI; “Nionyeshe Range Rover yako!
MCHUNGAJI; “akasepa”

Misemo 10 bora ya kuchekesha itakayokuacha mdomo wazi

1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.

2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.

3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?

4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.

5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.

6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.

7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.

8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.

9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.

10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi
kufunika sufuria.

Ziara za kushtukiza zinachekesha sana

Mimi Nimecheka sana
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

ZIARA ZA KUSHTUKIZA๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€
Mimi ni msomaji mzuri wa magazeti, na msikilizaji mzuri wa redio, huwa naangalia luninga mara chache sana kama nikibahatika kupita mahala kuna luninga. Sasa wiki hii nimesikia mengi kuhusu hizi ziara za kushtukiza za viongozi wetu, nikaona hili ni jambo zuri tena linafaa kuigwa na sisi wananchi wapenda maendeleo. Nikaona nijipange na mimi nifanye ziara kadhaa za kushtukiza katika sehemu mbalimbali zinazonihusu.

Nikaona nianze na ziara ya kushtukiza pale shuleni kwa huyu mwanangu, maana kila siku anakunywa chai na kuondoka na daftari zake na mie sijawahi kwenda shuleni kwao toka nilipomuandikisha shule mwezi Januari. Nilifika shuleni na kumuona mwalimu mkuu, ambae alianza kutetemeka nilipomuambia kuwa nimekuja pale kwa ziara ya kustukiza, sijui alidhani mi ni mmoja wa Mawaziri wapya, maana nilimuona jasho linamtiririka ghafla. Akanikaribisha ofisi yake iliyokuwa na vitabu kila kona, na kuita waalimu wote na kunitambulisha kuwa ni kiongozi nimekuja kwenye ziara ya kustukiza.

Nilipojitambulisha kuwa ni mzazi, waalimu wote nikawaona waanza kupumua kwa raha. Nikawaambia kuwa mimi nina mwanafunzi pale na nilikuja ziara ya kustukiza kujua maendeleo yake. Baada ya mwalimu mkuu kusaka jina la mwanangu nae akanambia, โ€œMzee huyu mtoto hajaja shule mwezi wa tatu sasa, tulijaribu kukutafuta ikashindikana, hatujui yu wapiโ€ Jasho likaanza kunitoka mimi, yule mtoto kila asubuhi nampa nauli anaenda shule, na mara nyingi ananiomba michango kumbe hata shule haji. Niliondoka bila kuaga presha ikiwa juu.

Nikaona niende kwenye genge la mke wangu nae nikamfanyie ziara ya ghafla nimhadithie mambo ya mwanae, nilipofika pale nikakuta kuna mdada mwingine anauza genge. Nikamsalimu, na kumuuliza mwenye genge ntampataje, jibu lake lingeniua kama ningekuwa si mkakamavu, โ€œMume wake kaja kumchukua na gari wameenda kununua shamba Bagamoyoโ€. Nikaondoka nimechanganyikiwa, nikajuwa hapa dawa yangu moja tu, nayo ni Sabrina, mtoto wa Kinyaturu pale ambapo nikipata maudhi huwa naenda kubembelezwa.

Nikatwanga mguu kwa Sabrina nae nikamfanyie ziara ya ghafla ili anipoze moyo. Nilipogonga mlango wa chumba chake akatoka mbaba wa miraba minne, akanisalimia kwa upole, โ€œSalama kaka unasemaje?โ€ Jibu likanitoka โ€œSamahani mie nilimkopesha huyu dada wa chumba hiki vitenge, nilikuja kuuliza kama ameshapata hela yanguโ€ Ziara za kushtukiza zinataka moyo wa chuma jamani

Huyu bwana leo kapatikana, Jamani nyodo nyingine mbaya

Baada ya kumaliza Degree yake ya sheria Bwana Rwegashora aliamua kurudi nyumbani Bukoba mjini na kufungua ofisi yake kwa ajili ya huduma kwa wateja.
Siku moja akiwa ndani ya ofisi yake alimuona mtanashati na mdada mmoja mrembo anakuja ofisini kwake akajua ni mteja anamletea kesi.

Ndipo akanyanyua mkoni wa wa simu ya TTCL na kuanza kuongea huku anajizunguusha kwenye kiti cha kuzunguuka.
Wakati mdada alipokaribia Rwegashora alimkaribisha kwa ishara maana alijifanya yupo busy na kuongea na simu ya umuhimu.
Wakati anaongea na simu akisikika akisema No, No, Noโ€ฆ.. Absolutely No. Wajuulishe hao lay person wa New York kua siwezi kushuhulika na kesi ambayo itanilipa chini ya 50 million. Mimi ni profesional lawyer and im crossing the border to sarve international community.

Aka pose kidogo na akanywa maji kisha akaendeleaโ€ฆ..
Naweza kuanza kukusanya primary evidence next weak but tell them watume kwanza ten million kwa kuanzaโ€ฆ
Hahahahaha you dont know my Account
Mr Roger. Ok waambie watume kwenye Account ileile walionitumia million 100 last monthโ€ฆ

Aka pose tena akameza fundo la maji na kurekebisha tai yake kisha akaendeleaโ€ฆ Ok usisahau kumueleza muendesha mashtaka mkuu wa marekani kua nitakuja New York mwezi ujao maana nitapita kwanza Amsterdam kuwasilisha utetezi wa yule mteja wangu mholanzi kisha nitaenda Tokyo kulipia ile gari yangu niloagiza.

Wakati anaongea hayo yote yule mdada alikua ametulia na anamuangalia Bwana Rwegashora anavyojizunguusha kwenye
kiti chake huku akiongea kwa tambo kwenye ile simu ya TTCL.
Baada ya kumaliza kuongea na simu Bwana Rwegashora aliweka mkono wa simu yake ya TTCL chini kisha akamgeukia mdada mrembo.

Samahan sana kwa kukupotezea muda wako unajua tena kazi zetu zinaumiza kichwa sana kama unavyoona mwenyewe yaani niko busy sana ninapokea simu sana mpaka nimechoka na simu nyingi ni za wateja wa njee ya nchi.

Anyway nikusaidie nn? Mdada akajibu mimi ni mfanyakazi wa kampuni ya TTCL nimekuja kuunganisha line yako ya simu kwani haipo hewani tangu wiki iliyopitaโ€ฆ!!!

Unadhani Bwana Rwegashora alifanyajeโ€ฆ???

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About