Vihoja Vya Kileo
Angalia anachojibu huyu babu. Wazee wengine bwana
Babu: Mjukuu wangu ngoja nikusimulie hadithi ya mimi babu yako kwenye vita ya kagera
Mjukuu: Niambie babu
Babu: Kwenye vita ya kagera tulienda sehemu tukakamatwa wote askari na maadui wakatuambia chagueni kuuliwa au kubakwa.
Mjukuu: Sasa babu wewe ulichagua nn?
Babu: Niliuliwa!!!
Mke alichomfanyia mme wake kabla ya kwenda safari, Chezea mawaifu walokole wewe!
JAMAA alimuaga mke wake mlokole kuwa anaenda semina ya siku tatu, kumbe anakwenda kwa bi mdogo.
Mke akamwambia mumewe; “Tupige magoti tusali”,
Wakapiga magoti…:
MKE: Eee baba msaidie mume wangu afike salama safari yake.
MUME: Emen…
MKE: Mpe nguvu katika yote atakayoyafanya huko.
MUME: Emen…
MKE: Akitaka kufanya uasherati ashindwe.
MUME: Kimya…
MKE: Akifanya uasherati apatwe na janga baya kwa uwezo wako bwana.
MUME: …….!!
MKE: Yaani akifanya uasherati afie hukohuko kwa mateso makali.
MUME: Maombi gani sasa hayo!!?. Haya basi siendi semina ufurahi wewe.
Chezea mawaifu walokole wewe!
Unakumbuka hizi enzi za utoto?
Kitambo tukiwa watoto ulikuwa unaitwa uje ule kwa lugha tofauti kulingana na chakula kilichopikwa siku na muda husika
1. UGALI NA KUNDE
Mwitaji : 🗣Joniiiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Uje ukule
2. UGALI NA SAMAKI
Mwitaji: 🗣 we Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Unaitwa na Mama
3. WALI NA NYAMA/KUKU
Mwitaji: 🗣 Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Shauri yako!
😂😂😂😂😂😂
Aina mojawapo ya watoto ambao ni hasara kuwa nao
Alipelekwa Hospitali na baba yake, baada ya vipimo Doctor akawa anamuandikia dawa, baba yake akatoka nje kuongea na cm.
Mtoto akamwinamia Doctor na kusema kwa sauti ya chini:- “Doctor Kwenye dozi ya dawa niandikie na FANTA BARIDII, CHIPS na MISHIKAKI kutwa mara 2 kwa siku 30.
Ungekua wewe ndio baba wa Huyu mtoto ungemjibu nini?
MTOTO: Hivi Baba wewe umezaliwa wapi?????
BABA: Mbeya
MTOTO: Mama nae kazaliwa wapi????
BABA: Tanga
MTOTO: Mimi jee?????
BABA: Dar
MTOTO: Sasa tulikutanaje????
😂😂 hapo wee kama baba ungemjibuje mwanao😳😳😳
Ungekua wewe ni mwalimu ungemshauri nini huyu mwanafunzi?
Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.
MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?
JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.
MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?
ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga.
MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.
MWAL: Na wewe James??
JAMES: mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiwe……”
Akameza mate kisha akaendelea….
“Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali.”
MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??
JENNY: Nataka kuwa mke wa James.!!
Angalia nilivyoingizwa mjini na ujanja wangu wote
Ndio nilikuwa nimeshuka kwenye basi la SAI BABA pale Ubungo, nina Begi kubwa Mgongoni na begi Dogo la Lap Top mkononi, sura inatazama Mbele Very Serious kama nipo kwenye Gwaride la Uhuru!..Mabega juu yanafanya Cheers na Mawingu!, natembea kwa madoido…..leo nimetoka Likizo Moshi,
“Brother Simu ya ukweli hii..kitu cha Tecno C9 bei poa” hii ilikuwa sauti ya Teja mmoja hivi!
Yaani huyu Teja Bwege kweli,anataka kumuuzia nani sabuni? mimi sio wa kuja!…kamwe Siwezi kuibiwa hapa Town,hakuna wizi au utapeli nisioujua!, Mimi nimezaliwa Mwananyamala kwa Manjunju, nikalelewa Tandale kwa Mtogole, Shule ya msingi nimesoma Turiani Magomeni, Hivi Mbwa gani aniibie?…kwa Style ipi?
Sipendi kabisa Upuuzi!, Wajinga ndio wataibiwa, sio Mimi!…sasa Kwa mwendo wa haraka nikatoka nje kabisa ya Stendi ya Ubungo straight mpaka Stendi ya dala dala za Kariakoo, hapo ndipo nikakutana na Vijana wawili wadogo wakiwa na mzani wa kupimia uzito,…hakika napenda sana vijana wanaojituma kama hawa na sio ile Mijizi ya kule ndani Stendi!!,….hapa sasa nikapata wazo!
“Dogo mnapima uzito kwa shilingi ngapi?”
“Mia mbili tu Kaka!”
”Ok”
Kwa mwendo wa kikakamavu nikapanda juu ya mzani,lengo hapa ni kujua uzito wangu, Mtori niliokula mwezi mzima kule kwa Mshekuu sio mchezo, hapa nahisi nacheza kwenye kg za John Cena,
“Mama wee! Dogo mzani mzima huu kweli? Mbona nina kilo 134?” (Nilihamaki)
“Aaah! Brother huoni umepanda na Mabegi juu ya mzani?”’
Hahaha! kweli nimechanganyikiwa!…Sasa nikatoa mabegi yote mawili na kurudi juu ya Mzani, hapa ndipo Uzito ukashuka kutoka kg 134 mpaka kg 56!…My God kweli Body la “One Pack ” haliongopi! thats means mabegi yaliniongezea kg 78! duh hii ni hatari!
“Yaani we Dogo kitambi chote hiki kg 56? huu Mzani Mzima kweli?”
Kimya…
“Dogo huu Mzani vipi?”
Kimya…
Dogo ana dharau huyu!…Sasa ndio nikabandua macho yangu toka kwenye kioo cha mzani ili nimtazame huyu dogo asiyejibu!….ndipo macho yangu yakakutana na Kigoda tupu kilichochongwa Mvomero!…Dogo hakuwepo!….na Mabegi pia hayapo!…lap top haipo!….NIMEPIGWA!
Ni dhahiri watoto wa Mjini walikuwa wameniacha juu ya Mzani, wamechukua Lap top ya Milioni na wameniachia Mzani chakavu wa elfu 40, what a stress!….sasa nilirudisha macho kwenye kioo cha uzito na sasa kilisoma KG 38!…yaani dakika hii hii nimepungua kilo zingine 18, Hakiyamama nahisi hata utumbo wangu wamebeba!…niitieni Ambulance!
🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼
Cheki huyu dingi alivyo mnoko
Unamtumia baba ako meseji ukiwa shule “Baba naomba unitumie 100,000 ya pckt mny” anakuuliza “pckt mny” ndo nini? Unamjibu ni kifupi cha “pocket money” af ankutumia 10,000, unamuuliza hiyo hela ni ya nini? Anakwambia ni kifupi cha 100,000.
Hapo ndo unatamani kuchoma shule ufe.
Madogo wa sikuizi ni kiboko, cheki huyu alichokifanya akiwa darasani na mwalimu wake
Muda wa kwenda nyumbani ulikuwa umefika, mwalimu
akasema: yeyote atakaye jibu swali langu lolote kwa usahìhi ataondoka asiye jibu atabaki.
Dogo mmoja akatupa begi nje ya dirisha.
Mwalimu akauliza nani katupa ilo begi nje?
Dogo akajibu fasta mimi. Akafungua mlango akaenda kwao.
neno moja kwa dogo
Recent Comments