Vihoja Vya Katikati Ya Juma
Misemo 17 ya kuchekesha
1) gari la kuvutwa halina overtake
2) kisigino hakikakai mbele
3) wimbo wa taifa haupgwi disko
4) feni haiwashwi beach
5) mshkaki hauchomwi kwa jiko la ges
6) mganga haagiz tembele
7) hata bibi alikuwa bint
8) mke wa mtu sumu,mume wamtu maziwa
9) kipara bila pesa ni kovu
10) mbwa hanenepi migiuu
11) picha ya rais haina bodyguard
12) mjini shule kijiji tuition
13) saa ya ukutani haivaliwi mkonon
14) heshima pesa shkamoo makelele
15) ulinz pesa bastora mzgo
16) kuku ni kuku jogoo mbwembwe
17) kusoma kuelewa kukesha mbwembwe
Sifa 10 za mwanaume ambaye kila binti anayetaka aolewe angependa aolewe naye!!
1. Awe na pesa nyingi
2.Siyo lazima awe mzuri wa sura
3. Ajenge ukweni
4.Awe mpole
5.Asimuonee wivu mke wake
6.Awe mwenye upendo wa dhati
7.Asishike simu ya mke wake.
8.Akimkuta na mwanaume apite tu, akitaka kujua ni nani asubiri nyumbani
9.Awe anamskiliza mke wake kwa kika kitu.
10.Asipende mwanamke mwingine zaid yake
UKIMPATA MWANAUME MWENYE SIFA HIZO KAPIME DNA LAZIMA ATAKUWA NI BABA AKO.
๐๐๐๐๐๐๐๐
Angalia jamaa alivyouweza huu mchepuko wake
Kuna mchepuko nilimtumia nauli jana ili aje,.kwang sasa leo kaniambia eti ” nimesahau ile line yenye M-pesa home plz nitumie tena kwa tigo mpenz””!! Me nikajifanya chizi nikatuma Kule kule kwenye voda (aliosema kaacha home) Nikatuma huko message ivi “nikuongezee Sh. Ngapi tena mpenz..!!” Akanjbu “elfu 20,000 tu mpenzi” Mtuhurumie jamani ๐๐๐
Angalia hawa machizi walichokisema baada ya kuona ndege angani
Machizi wamekaa sehemu mara ghafla ikapita ndege angani.
Chizi wa kwanza akasema:ndege ile itakua imembeba raisi.
Chizi mwenzie akajibu:hapana imebeba wazungu kama ingembeba raisi tungeona pikipiki zimetangulia mbeleโฆ
da!balaaa
Cheki hawa washikaji wanachokifanya baada ya kuvuta bangi, Bangi si mchezo
Kuna washikaji walikuwa wakivuta bangiโฆ kiberiti kikawaishiaโฆ wakamtuma mwenzao akatafute kingineโฆ bangi lilikuwa limemkoleaโฆ akazungukazunguka hatimaye akarudi palepale kijiweniโฆ
MSHIKAJI:ย oyaaa wanangu eeehโฆ niazimeni kiberiti mwanangu mwenyewe โฆ..
WENZAKE:ย baharia ee subiria kimtindo kuna mwana tumemtuma akatafute kiberiti.
Kama mpezi wako akikuita MAMITO Unatakiwa umjibu hivi
Akina dada mpenzi wako akikuita MAMITO usikubali
na yeye mwite MAFORONYA kama mbwai na iwe mbwai๐คช๐คช๐คช๐คช๐คช๐คช
Mambo ya kijijini haya!
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuniโฆunaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuniโฆ๐๐๐๐
Hii ndio ngoma droo kwa wanaume kati ya wanawake
{ NGOMA DROO}
Sikuizi utawasikia wadada wakisema kuachwa na mwanaume asie na pesa nisawa na kuluhusiwa hospital
{Sasa na sisi} wanaume tunasema
Kuachwa na demu mpenda pesa nisawa na kumaliza mkopo benk ๐๐๐๐๐๐
Wanaume atutakagi ujinga!!!! Wanaume heeeeee๐๐พโโ๐๐พโโ๐๐พโโ๐๐พโโ
Hakuna siku mbaya maishani kama hii
Hakuna siku mbaya maishan kuona mtu uliyesoma naye darasa moja, anakupita na private car,, afu we umeninginia kwenye daladala,,, tena ulikua unamzid akili ๐๐๐hapo Ndo utajua kwann gunia na dunia vinatofautiana neno moja
Huyu dogo nimsaidieje? Cheki alivyojichanganya
Nimekutana na dogo mmoja hivi hapa analia,namuliza analia nin??ananambia ”ALIPEWA MIA TANO ZIPO MBILI,MIA TANO MOJA YA NYANYA na MIA TANO NYINGINE YA VITUNGUU sasa KAKOSEA KAZICHANGANYA HAJUI TENA IPI NI YA NYANYA na IPI NI YA VITUNGUU!!!
.
.
Recent Comments