Vihoja Vya Jumapili

Angalia ndoto nyingine zilivyo na Majanga

Ndoto zingine bwana usiombe zikupate

Mimi usiku wa kuamkia Leo nikiwa nimelala nimeota naendesha gari Yangu aina ya BMW mpya Mara gafla ikakwama kwenye tope .hivyo ikabidi nishuke ili kuisukuma loh! Yani kudadeki ile kuamka nikakuta nimesukuma kitanda hadi sebleni Daaa ilinisikitisha sana jiangalie sana sese hivi ndio narudisha kitanda chumbani .angalizo angalia ndoto unazo ota unaweza kuota upo baharini ukaamka unajikukuta unaogelea kwenye Jaba la Maji shauri yako.

Cheki jamaa alivyoumbuka baada ya kuhudhuria semina isiyomuhusu

Jamaa kavamia semina ya wasomi iliyokua inafanyika maeneo ya ubungo plaza bas wakaanza kujitambulisha
1. Naitwa Anna niko SUA mwaka3 nasoma agriculture
2. Naitwa Stella niko UDSM mwaka2 nasoma public relation

3. Naitwa Emmanuel niko UDOM mwaka3 nasoma computer science
bas jamaa nae akainuka kwa kusuasua huku akijishtukia akasema”Naitwa Elisha niko Tanesco mwaka wa 7 nasoma mita”

Faida 3 za uvutaji wa sigara

Ni hizi

1. Mvuta sigara hazeeki
2. Mvuta sigara haumwi na mbwa
3. Mvuta sigara nyumbani kwake haingii mwizi

UFAFANUZI

1. Hazeeki kwa sababu hufa mapema kwa kifua kikuu

2. Haumwi na mbwa kwa vile kifua na mapafu yanapooza na hulazimika kutembea na bakora

3. Nyumbani kwake haingii mwizi kwa kuwa inafika wakati ambapo halali:
atakohoa usiku kucha hivyo mwizi anajua yupo macho
kumbe kikohozi tu!

Cheki huyu mwanamke anavyomkomoa mme wake baada ya kumsaliti

MKE: Mbona unanukia pafyumu ya kike?
MUME: Yaa kuna mwanamke tulikuwa tumeminyana ndani ya daladala
MKE: Na lipstiki kwenye shati?
MUME: Tulikumbatiana na wageni toka Zambia walitembelea ofisi yetu
MKE: Na ile kondom iliyotumika kwenye mfuko wa suruali?
MUME: Bwana ee acha maswali ya kijinga mi nalala nina usingizi
MKE: Lazima niulize mie huwa nahakikisha nimeacha kila kitu hukohuko ndio narudi nyumbani
MUME: Umesema nini wewe?
MKE: Bwana ee acha maswali ya kijinga mi nalala nina usingizi. 😄😄

Cheki masifa yalivyomponza huyu, Sifa nyingine ni mbaya jamani

Mbongo, Mganda, na Mkenya walikamatwa na makosa Uchina.

Wakaambiwa adhabu ni ama kifo cha moja kwa moja au adhabu nyingine ambayo atakayeifaulu atakuwa huru, atakayeshindwa atauawa.

Basi wao wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu bahati yao.

Wakapelekwa msituni wakaambiwa kila mmoja aende kwa njia yake halafu arudi na matunda kumi ya kufanana.

Wakaingia msituni kila mtu njia yake.

… Mganda akarudi wa kwanza na machungwa kumi. Akaambiwa adhabu yake ni kumeza moja moja likiwa zima bila kufumba macho bila kulia wala kucheka wala kujitikisa mpaka yote kumi yaishe. Akameza la kwanza. Safi. Kumeza la pili, akashindwa kuvumilia akafumba macho. Akapigiwa risasi akafa.

Mkenya akaja. Ana vitunda vidogo vidogo kama pili vilaini. Akasomewa masharti. Akaanza kumeza bila kufumba macho wala kulia, wala nini… alipofika cha tisa akashindwa kuvumilia akaangua kicheko! Akapigwa risasi pia akafa.

Wakiwa kuzimu Mganda akamwuliza Mkenya, “Vipi, mbona ulishindwa kuvumilia wakati kilibaki kitunda kimoja tu?”

Mkenya akamjibu: “Mkuu, nilishindwa kuzuia kicheko maana nilimwona Mbongo anakuja na matikiti maji!”

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About