Vihoja Vya Januari
Huyu mchungaji ni noma, cheki alichomwambia pedeshe
Mchungaji kamfuata pedeshe moja maarufu kwa
kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki;
MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za
kujenga kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa
mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na Mungu
atakubariki zaidi
PEDESHE: Samahani Mchungaji haitakuwa vizuri
mimi kuchangia kanisa, fedha zangu ni haramu,
huwa nazipata kwa utapeli na kuuza madawa ya
kulevya.
MCHUNGAJI: Yote ni heri, pesa yako tutatumia
kwa kujenga eneo la choo we toa tu!!!
Dunia ina mambo, soma hii
Dunia ina mambo
Kuna mama mmoja kavamia bank uchi cha kushangaza hakuna anae kumbuka uso wake๐๐๐๐๐
Kilichotokea baada ya kichaa kumfumania mke wake na mwanamme mwingine
Jay akaruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospital ya Vichaa, akapakiwa ktk ambulance hadi karibu na nyumbani kwake, akaulizwa unapakumbuka? akajibu ndio nyumba yangu ileee, mara wakatoka watoto wawili wamevaa uniform akasema watoto wangu walee wanakwenda shule.. akatoka mwanamke akasema na mke wangu yulee, ghafla akatoka mwanaume Jay akasema na mimi yule naenda kazini. hivi Jay kweli kapona?
Kilichotokea nikiiwa namsaidia mtoto home work
Kusaidia Mtoto wa Nursery Homework ni Ngumu. Unamuuliza “Nina Pipi Tano, nikiwagawia Watoto Watatu, kila mmoja Pipi Mojamoja nabakiwa na ngapi? Anakwambia, “toa Kwanza nizione..”๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Hawa wanaume wanaopenda wanawake hovyo barabarani wamepatikana, hawatarudia ๐๐๐
Marafiki wawiliย (Jose na Ben)ย walikuwa wanatembea mtaani akatokea mwanamke akarusha busu kwa mmojawapo kupitia dirishani katika jengo la ghorofa tatu.
Wakaanza kujadiliana kama ifuatavyo:
Ben:ย Muone yule mrembo amenirushia busu
Jose:ย tafadhali achana na huyo mwanamke, usimjali..
(baadae yule mwanamke akamuashiria aende)
Ben:ย yule mwanamke ameniita!
Jose:ย Rafiki yangu, usiende. Nakutafadhalisha.
Ben:ย Kwa nini unaniambia nisiende Wakati mrembo kama yule ananiita? Huo ni wivu
Jose:ย Ben, Ninakutafadhalisha tena, usiende, tafadhali usiende kuleย (akihisi kutotiliwa maanani)
(Rafiki yake alimpuuza na alienda kwa yule mwanamke, mwanamke alishuka kukutana naye na wakapanda juu. Ghafla wakiwa wanataka kuanza taratibu za kula uroda, wakasikia mlio WA gari getini).. ๐๐
Lady:ย _(akiangalia kupitia dirishani)_
Oooh! Yule ni mume wangu!!
Ben:ย Mama yangu !
Nipo matatani, kweli ? ..!!
Lady:ย Usiwe na khofu, jifanye kuwa Dobi na anza kupiga pasi hizo nguo
(akimuonyesha lundo la nguo)
(Ben alitumia masaa matano kukamilisha kunyoosha zile nguo kwa sababu yule mume hakutoka tena siku ile)
(Siku iliyofuatia Ben alikwenda kwa Rafiki yake)
Ben:ย Kaka, unaweza kuamini Jana nimepiga pasi nguo kwa masaa matano???
Jose:ย Lakini nilikwambia usiende. Nguo zote hizo ulizonyoosha,ย Nilizifua Mimi Juzi!!
๐๐๐๐๐๐๐๐๐
When an experienced person speaks โฆ ๐you must listen..!
Nilichokifanya baada ya kualikwa na mchumba wangu kwao
Mchumba wangu amenialika kwao nikawaone wazazi wake lakini akaniambia nisiende mikono mitupuโฆ
Nikaamua kuvaa glovesโฆ
Sipendagi aibu ndogo ndogo ukweni.๐๐๐
Angalia nilivyookoa maisha ya mtu leo
Nmeokoa maisha ya mtu asubuhi ya leo huwezi amini.Nmekutana na ombaomba nikamuuliza atajisikiaje nikimpa sh.30,000/-
Akasema ATAKUFA kwa furaha.Nikaondoka bila kumpa ili ASIFE.๐๐๐๐
Kilichotokea baada ya kuzamia sherehe
Pale unapozamia kwenye Dinner Party ya Jumuiya Fulani, sasa Lengo la Jumuiya hiyo ni kupata Fedha za kutunisha Mfuko wa Jumuiyaโฆsasa unakakaa mbele kabisa ili Muda wa Msosi usichelewe na kukuta kwenye Buffee yamebaki maharage!
MC : “Papai zuri kabisa kutoka Newala, Papai Mwendokasi, hili ni Shilingi laki 1..jamani Papai,nipeni ofa!”
MOSHA : “Laki 3 hapaaa!”
“Jamani laki 3 pale kwa Mosha, Papai linaondoka jamani, papai hili ni self contained kabisaโฆ.papai jamani”
KIBOLIBO: “Milioni 1 hapaaa”
“Jamani Mambo yanazidi kunoga hapa!โฆBenedict Kibolibo anataka papai kwa milioni 1 jamani, linaondoka papai!”
RWEYEMAMU : “nitanunua Papai hilo kwa Milioni 5”
Haya sasa jamani Rweyemamu ametoa ofa ya Milioni 5 Jamani, nani mweingineee?”
Kimyaaaโฆ
Haya jamani Papai kama hakuna Ofa basi Papai linakwenda kwa Rweyemamu!โฆโฆ..haya sasa Kuna Kuku hapa Jogoo kabisa, bei yake ni laki 6 jamani Jogoo twitter huyu!”
WEWE “Milioni Mojaaa!”( hapa umejiwahi wa kwanza na wewe uonekane upo huku ukijua kabisa Wakina Mosha na Rweyemamu lazima watampandia Dau Jogoo, tena dau kubwa”
MC: ee sasa Kumekucha Jamani, Kabasele anamtaka Jogoo kwa Milioni 1 jamani!โฆ.ofa nyingineeee!”
Kimyaaaโฆ
Jamani Jogoo anakwenda kwa Kabasele jamani!โฆofa nyinginee!
Kimyaaaโฆ.
Kimyaaaโฆ.
๐๐๐โฆhapa sasa ndio mfukoni kuna Buku jero,..huko kwengineko NMB nill balanceโฆsasa unageuza mimacho kumtazama Mosha kama atapanda dau kwa jogoo๐(mama wee Mosha anachezea Simu!)โฆ..unamtazama Rweyemamu (teh anatafuna Kuku)โฆ..mama weee๐
MC: Haya jamani kama hakuna Mwingine basi zoezi letu liishie hapa na limekwenda kwa Mafanikio, Mpatieni Kabasele Jogoo wake!
Hapa sasa unapokea jogoo wako wa MILIONI kwa Tabasamu la Maitiโฆ.kule nyumbani Jogoo wako Mkubwa unauza elfu 20 lakini sasa haka kajogoo kapya Mkononi kanakuwa kazito utadhani umembeba John Cena๐โฆMama weee hapa sasa vidari ulivyotafuna unaviona kama vimerudi kwenye Ulimiโฆ.Chicken wings zinataka kutokea Masikioniโฆ..Uuuuwiiiii,๐๐๐
Na hapa sasa kabla Dinner haijaisha ndipo unapojikuta Umebuni Cocktail ya Sparetta na Tomato๐๐๐๐๐.
chiel wie okee









I’m so happy you’re here! ๐ฅณ




































































Recent Comments