Vichekesho Vya Wazee

Kuwa na mahusiano na msichana kama huyu ni changamoto, Mabinti bwana!

Binti: Hallow mpenzi, Mambo

Jamaa: Poa baby

Binti:Uko wapi?

Jamaa: Niko town napata lunch

Binti: Wow unarudi saa ngap? Nina njaa dear naomba uniletee msosi

Jamaa: Narudi baada ya nusu saa nikuletee nini?

Binti: Niletee chipsi kuku, soseji, mayai manne ya kukaangwa pembeni, baga, piza, coke take away baridi, mkate wa moto kwenye ile bekari ya wapemba na maji ya kunywa ya kiimanjaro.

Jamaa:Umesahau viti, meza, masufuria, sahani na beseni na vijiko.

Binti: Kwanini dear?

Jamaa: Naona hutaki kula unataka kufungua hoteli!

Wanaume wote ni waaminifu

Hii ni kwa wanaume ila mwanamke anaweza kusoma na kujifunza kuwa wanaume wote ni waaminifu.

Mwanaume mmoja alienda kukata miti kwa ajili ya mkaa, bahati mbaya panga likadondokea mtoni, akaanza kulia sana. Malaika akatokea na kumuuliza kwanini analia. Jamaa akajibu; “Panga langu limedondokea mtoni na ndilo ninalotegemea kuendeshea maisha yangu”.

Malaika akazama mtoni na kuibika na panga la DHAHABU na kumuuliza, ndio hili?

Jamaa: Hapana.

Malaika akazama tena na kuibuka na panga la SHABA na kuuliza, ndio hili?

Jamaa: Hapana.

Malaika akazama tena mara hii akaibuka na panga la CHUMA na kuuliza ndio hili?

Jamaa: NDIYO.

Malaika akafurahishwa sana na uaminifu wake hivyo akampa mapanga yote matatu. Jamaa akafurahi sana.

Siku nyingine jamaa alikuwa anatembea na mkewe njiani ghafla mke akadondokea mtoni, jamaa akaanza kulia. Malaika akatokea na kumuuliza: Kwanini unalia?

Jamaa: Mke wangu kadondokea mtoni na nampenda sana.

Malaika akazama mtoni akaibuka na WEMA SEPETU na kuuliza; “huyu ndiye mkeo?”

Jamaa: NDIYO.

Malaika akakasirika sana na kumuuliza: kwa nini umenidanganya?

Jamaa: Nimesema ndiyo kwa sababu ningesema hapana ungezama tena na kuibuka na AUNT EZEKIEL na ningesema hapana tena ungezama na kuibuka na MKE wangu alafu ningesema ndiyo ungenipa wote watatu!

Sasa mimi maskini sina uwezo wa kuhudumia wote hao, ndio maana nikasema NDIYO kwa Wema Sepetu.

*FUNDISHO*
Wanaume huwa hatusemi uongo bila sababu na inakuwa sababu maalumu kwa faida ya wote.

WANAUME WOTE NI WAAMINIFU. Hii ndiyo kauli mbiu yetu.
😀😀😀😀

Huyu jamaa kawaweza wapenda vya bure

Jamaa kaingia mgahawani kwa fujo
JAMAA : Nipe soda moja na kila mtu mpe yake maana ninapokunywa soda napenda kila mtu anywe
WATU : Ha! Ha! Ha! Haaaa!
JAMAA : Nipe mchemsho na kila mtu mpe wa kwake maana ninapokula mchemsho napenda kila mtu ale wake
WATU: Watu weweeee! Tena safari hii Na makofi juu..
JAMAA : Mhudumu, nipe bili na kila mtu mpe yake maana ninapolipa bili napenda kuona kila mtu analipa yake
😂😂😂😂😂😂😂

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About