Vichekesho Vya Wakaka Na Wadada

Kilichotokea baada ya polisi wa kibongo kukutana na mwizi mzungu

POLISI KAKAMATA MZUNGU ‘yestaday I saw u at ze maize shop..(jana nilikuona dukani kwa muhindi) when u saw me u started 2 six six.(uliponiona ulianza ku-sitasita) u ran n decided 2 plant a car.(ulikimbia na ukaamua kupanda gari) zen u pot-cry me through ze window.(kisha ukanichungulia dirishani) now sleep down n snake well b4 I cut u a millet.(sasa lala chini kisha nyooka vizuri kabla sijakukata mtama) Chezea lugha wewe..!!!

Cheka kidogo, angalia anachosema huyu mchaga

Mchaga baada ya kufa akaulizwa na malaika anayetoa roho: Mangi hapa ni njiapanda kulia ni Mbinguni na kushoto ni Jehanamu, Je unachagua kwenda wapi?

MANGI: Bwashee, mi nabaki hapa hapa njiapanda aisee.
MALAIKA: Kwa nini?
MANGI: Aisee, nikifungua duka hapa si nitapata wateja wa Mbinguni na Jehanam. Yani patakuwa senta ya hatari, supu na nyama choma muda wote. Hata we utafaidi, unavyoenda kuchukua roho unaniletea stock nakupa hela yako cash mkononi. Na kila ukipita hapa unapiga mchemsho wako wa ulimi na bia mbili chap kabla ya kuingia mbinguni.
Kwanza nashangaa Shirima alipitaje hapa bila kushika ploti, au alikufa amelewa sana?

Madhara ya kubeba nauli kamili tuu. Cheki kilichonipata

Kubeba nauli kamili nayo ni shida
Yani nimepanda daladala
Kondakta mmoja akaingia kwenye Gari amevaa suti za blue za daladala na miwani Kisha akakusanya pesa Gari Zima alafu akakaa siti ya nyuma baade Kondakta mwingine akaanza kukusanya pesa watu wakalalamika na kusema tayari tumelipa na kumuonyesha tuliemlipa Kondakta akacheka na kusema huyo tuliemlipa ni kipofu na alikuwa anaomba msaada..!!

Madenge hakosi visa. Soma hii

MADENGE
HAKOSI
VISA

baada ya kumaliza form four baba akamwambia achague zawadi yoyote aipendayo
MADENGE: naomba pesa nikamuoe bibi maana siku nyingi amekuwa akiniita mchumba wake.
BABA: Shenzi, yule ni mama yangu mzazi huwezi kumuoa.
MADENGE: Mbona wewe umemuoa mama yangu mzazi sijasema kitu ww inakuuma? lazima nilipize kisasi ikikuuma muache mama yangu kila mtu akae na mamayake. 😂😂😂

Mke alichomfanyia mme wake kabla ya kwenda safari, Chezea mawaifu walokole wewe!

JAMAA alimuaga mke wake mlokole kuwa anaenda semina ya siku tatu, kumbe anakwenda kwa bi mdogo.

Mke akamwambia mumewe; “Tupige magoti tusali”,

Wakapiga magoti…:
MKE: Eee baba msaidie mume wangu afike salama safari yake.
MUME: Emen…

MKE: Mpe nguvu katika yote atakayoyafanya huko.
MUME: Emen…

MKE: Akitaka kufanya uasherati ashindwe.
MUME: Kimya…

MKE: Akifanya uasherati apatwe na janga baya kwa uwezo wako bwana.
MUME: …….!!

MKE: Yaani akifanya uasherati afie hukohuko kwa mateso makali.
MUME: Maombi gani sasa hayo!!?. Haya basi siendi semina ufurahi wewe.

Chezea mawaifu walokole wewe!

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About