Vichekesho Vya Msimu Huu
Cheki nilichomfanyia boss wangu
Bosi wangu karudi safari yake kutoka serengeti..! Si akanitumia picha, lakini ilikuwa network yenyewe tabu.. kwahio picha haikufunguka na kwa vile niliona itachelewa kufunguka na ataona sikumjibu basi nami..
Nikampelekea msg nikamuandikia umependeza saana bosi mashaallahโฆ!!
sasa baada tu ya kumfika msg.. na huku picha ikafunguka kumbe picha ya Sokwe..!!
Basi Kaniambia kesho niende ofsini kwake kuna barua yangu..
Nahisi hyo barua ina pesa, hapa cjalala, nmekosa usingizi kabisa,nawaza ninunulie nn hyo pesa.Na kesho asubuhi sa 12 asubuhi atanikuta ofisini kwake naisubiri barua, sipendagi ujinga mimi.
Hizi sifa zimezidi sasa
MADEM KWA SIFA..
kuumwa aumwe yeye lakn kujifanya anajali sana bas utamsikiaย BABY KARIBU TUMEZE DAWAย ๐๐๐
Hiki ndicho kifo mbele ya Mwanamke
Hiki ndiyo kifo.
KIFO NI NINI..
Kifo ni pale girlfriend wako anapofanya fujo Club akiwatukana MABAUSAย Huku akisema
“BABY WANGU HATA HAWAOGOPI”
๐๐๐๐
Huu mchezo hautaki makeup
Mama mwenye nyumba anajipodoa anashinda saloon kujipodoa lakini house girl hata mafuta usoni hapaki lakini akipita na khanga yake moja tuu nyumba inatetemeka๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐ huu mchezo hautaki mekapu
Angalia kilichojiri katika semina ya wanandoa kuhusu upendo
Kulikuwa na semina ya wanawake kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa.
Mwalimu aliwauliza ni wangapi wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha mikono kama ishara ya kuwa wanawapenda waume zao.
Mwalimu akauliza tena, โNi lini mara ya mwisho umemwambia mumeo โNakupenda Mpenziโ?
Majibu yalikuwa kama ifuatavyo:
Wengine wakisema Asubuhi ya leo,
Wengine jana,
Wengine wiki iliyopita
Wengine mwezi uliopita
Na wengine wakasema hawakumbuki!
Mwalimu aliwapa kazi kila mwanasemina achukue simu yake na kumtumia mume wake meseji yenye neno โNAKUPENDA MPENZIโ
Baada ya meseji kwenda aliwaamuru kubadilishana simu kila mtu na jirani yake.
Kila mwanasemina aliambiwa kusoma meseji za majibu kwenye simu aliyoshika
Simu ya 1 โ โSamahani, nani mwenzanguโ!
Simu ya 2 โ โSamahani, wrong numberโ!
Simu ya 3 โ โSi nimekuambia usinitumie messages kwenye namba hiiโ!
Simu ya 4 โ โMh! leo mvua itanyeshaโ!
Simu ya 5 โ โNikija tutaongea zaidiโ!
Simu ya 6 โ โโฆโฆImedhibitishwa umepokea Tsh300,000 kutoka kwa โฆโฆโ!
Simu ya 7 โ โMe tooโ!
Simu ya 6 โ โHuu ujumbe ndio ulikuwa unamtumia huyo hawara yako ee, leo utanikomaโ!
Madhara ya kubeba nauli kamili tuu. Cheki kilichonipata
Kubeba nauli kamili nayo ni shida
Yani nimepanda daladala
Kondakta mmoja akaingia kwenye Gari amevaa suti za blue za daladala na miwani Kisha akakusanya pesa Gari Zima alafu akakaa siti ya nyuma baade Kondakta mwingine akaanza kukusanya pesa watu wakalalamika na kusema tayari tumelipa na kumuonyesha tuliemlipa Kondakta akacheka na kusema huyo tuliemlipa ni kipofu na alikuwa anaomba msaada..!!
Mipango ya mke na mume ya pasaka
Mke: Unampango gani na pasaka hii mmewangu..
Mume: Nitafanya kama yesu..
Mke: Unamaanisha Nini?
Mume: Nitaondoka ijumaa na Kurudi j3..
Mke: Unanishangaza, kama utafanya hivi nami nitafanya kama Maria..
Mume: Unamaanisha Nini?
Mke: Nitapata mimba bila ya kuingingiliwa na wewe mume wangu..
Mume: ๐ณ๐ณ๐ณ
๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Je, hili nalo ulilipitia ulipokua Shuleni?
Hakuna Kitu Kilikua Kinaniumizaga Kipindi Nipo Shuleni.
Time Mmetoka Kwenye Mitihani Wa Mathematics Halafu Mpo Kikundi Fulani Either Mnarudi Nyumbani Au Mnapumzika Kwa Ajili Ya Next Exam.
Unasikia Jamaa Wanabishana Pale Jibu Lilikua 4 Mwingine Anasema 5, Na Wewe Ulijaza 80.
Huyu Jamaa kawaweza polisi kweli
Et jamaa kawekwa jela kwa kosa la kupoteza mamiilion.ya kampun akiwa gerezan babayake alituma barua
Ikisema yan.mwanangu tumapata shida maana shamba halijalimwa na jatujii litalimwaje na msimu ndio huo nataman.ungekuwepo ningepata msaada wa kulimiwa hili shamba
Yule kijana alijibu tafadhal baba usilime hilo shamba maana pesa zote nilizo ibwa nimeficha.huko
Kwakuwa barua zote laxima zipite kwa mkuu wa gereza ndio xiende kwa muhusika kesho yake mzee alikuwa shamba lote limelimwaa na polisi
Akatuma ujumbe tena yule kijana
Nashukulu umepata msaada sasa nazan unaweza ukaendelea kupanda mazao shamban.kwetu๐๐๐๐๐
Duh, Ukisikia ngoma droo ndio hii
Ni noma!
Baada ya Talaka mke kamtumia mume meseji:- “Nasikitika kukujulisha kuwa binti uliyemlea kwa miaka 20 sio mtoto wako” Mume akamjibu:- “Duh! Nashukuru Mungu kwani nilikuwa nikiumia rohoni kila siku kwamba nazini na binti yangu” ๐๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐๐










I’m so happy you’re here! ๐ฅณ



































































Recent Comments