Vichekesho Vya Kushangaza
Huu ndio uhondo na raha ya kupanda daladala wajameni
Wasiopanda dalaladala wanakosa uhondo wa kauli hizi
1. nitakupa
2. Atapewa mbele
3. Hujapewa mbele?
4. Utapewa nyuma
5. Nitakupa nikikaa vizuri
6. Ngoja isimame nikupe
7. subiri asimamishe nikupe
8. hivi nlivyo kaa ntakupaje?
9. Utapewa tulia
10. Nikupe mara ngapi?
Nilichokifanya wakati naangalia taarifa ya habari
Jana wakati naangalia taarifa ya habar mtangazaji akasema “mpenz mtazamaji nataka nikupeleke moja kwa moja had marekani” nikazima TV kwa haraka nikaenda kuvaa viatu. Hadi sahv bado nmekaa hapa seblen nahisi bado wanaihangaikia Visa yangu
๐๐๐๐๐๐
Kilichotokea wakati mchungaji akifungisha ndoa ya Mashoga
Mchungaji mmoja baada ya kuwafungisha ndoa “MASHOGA” wawili alipata wakati mgumu kutamka kuwa “sasa ninyi ni MKE na MUME”
atafanyaje wakati wote ni wanaume? mchungaji akapiga moyo konde na kusema “tangu sasa ninyi ni MAN UNITED”
Ungekua wewe ni mwalimu ungemshauri nini huyu mwanafunzi?
Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.
MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?
JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.
MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?
ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga.
MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.
MWAL: Na wewe James??
JAMES: mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiweโฆโฆ”
Akameza mate kisha akaendeleaโฆ.
“Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali.”
MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??
JENNY: Nataka kuwa mke wa James.!!
Simu ilivyozua utata
Mama alichukuwa simu akampa mwanawe. Mama..Mpigie babako mwambie chakula tayari. (Mtoto akachukuwa na kupiga) MtotoโฆMama simu ya baba imepokelewa na mwanamke. (Mama kwa hasira) Akirud atanitambua leo. (Baada ya muda kidogo baba akarud,kufika mlangon tu kapokewa na sufuria ya kichwa. Hajakaa vzur mwiko wa pua) Mama..Mwanangu ulipopiga simu ya babako mwanamke wake alisemaje?? Mtoto..Alisema mteja unaempigia hapatikan kwa sasaโฆ..
Angalia huyu mtoto anachomjibu baba yake baada ya kutoka kwenye mtihani
BABA: mwanangu kwenye huu mtihani uliofanya natumaini utafanya vizuri.
DOGO: ndio baba nitapata mia kwa mia.
BABA: kwanini unasema hivyo?.
DOGO: kwasababu jana kanisani tulifundishwa “Yesu ni jibu” kwahiyo kote nimejaza Yesu.
BABA: kwel kazi ipo
JE UNGEKUWA WEWE HUYO NDO MWANAO UNGEMFANYAJE?
Punguzeni pombe. Cheki kilichompata huyu
Jamani punguzeni pombe,kuna jirani yangu amerudi amelewa sasa nachungulia dirishani naona anagonga mlango wake takribani masaa mawili,wakati hapa anaishi peke yake, kwakuwa sipendagi ujinga nimetoka nikamwambia mwenyewe kasafiri.Nae kaondoka.
Muda ambao unaweza kumzoea dingi
Muda pekee ambao unaweza kumzoea DINGI ni pale unapomfundisha kutumia SMARTPHONEโฆ.
Wanakuwaga wapole sana aisee unaweza hata kumuagiza maji ya kunywa akakuleteaโฆ.
๐๐๐๐๐๐๐
Mambo ya mke na mume haya, chezea mchepuko!?
Mume akamwambia mke wake:
“Funga macho yako tufanye maombi”
Akaanza kwa Kimombo:-
“โฆ Lord I pray for Grace, I pray for Mercy, I pray 4 Joy, I pray 4 Love, I pray 4 Hope, I pray 4 GLORY, I pray 4 Faith, I pray 4โฆ.”
Mke akadakia, “Unadhani mimi sina ee” akaanza:-
I pray 4 Felix, I pray 4 Temu, I pray 4 Rweyemamu, I pray 4 Masawe, I pray 4 Benson, I pray 4 Onyango, I pray 4 Swai, I pray kwa wote niliowasahau!!
Chezea mchepukoโฆ!!
Angalia sababu ya mwanamme kubadili jina na Kuitwa jina la kike, hii dunia ina mambo kweli
Rashidi alimpa ujauzito mwanafunzi, akashtakiwa.
Kumbe Rashidi ana bibi yake mtaalamu wa yale mambo yao ya Sumbawanga, akampachika Rashidi i jinsia ya kike.
Alipofika mahakamani kuhojiwa Rashidi akasema sijampa ujauzito kwa sababu mimi pia nina jinsia ya kike.
Kwa kuthibitisha Rashid wakaenda kumkagua basi akashinda kesi, kufika nyumbani Rashid akawakuta watu wamejaa wanalia, akauliza kulikoni?
Akaambiwa bibi yako amefariki. ๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ๐ฐ๐ฐ๐ฐ๐๐๐๐๐๐
Kwa sasa Rashid anaitwa Leila๐๐๐
Recent Comments