Vichekesho Vya Kukupa Mudi Mpya
Kilichotokea Baada ya mlevi na mchungaji kukutana
MCHUNGAJI; “Unakunywa bia!?
MLEVI; “Ndio.
MCHUNGAJI; “Kwa siku unakunywa bia ngapi!?
MLEVI; “Nakunywa bia tano!
MCHUNGAJI; “Bia moja bei gani!?
MLEVU; “2500/
MCHUNGAJI; “Ulianza lini kunywa bia!?
MLEVI; “Miaka 18 iliyopita!
MCHUNGAJI; “Kwa hiyo kwa siku unatumia zaidi ya 10,000??
MLEVI; “Ndio!
MCHUNGAJI; “Kama u gekuwa unatunza hiyo pesa 10,000 kwa siku leo hii si ungekuwa na Range Rover!?
MLEVI; “Samahani, naweza kukuuliza swali!?
MCHUNGAJI; “Uliza!
MLEVI; “Unakunywa bia!?
MCHUNGAJI; “Hapana!
MLEVI; “Nionyeshe Range Rover yako!
MCHUNGAJI; “akasepa”
Ungekua wewe ndio boss wa huyu jamaa ungempa kazi? Ungemjibu nini?
*Boss*:-kijana unataka nini ndani ya ofisi zangu?
*Jamaa*:-Samahani naomba kazi ya ulinzi ndugu.
*Boss*:-umesoma mpaka wapi?
*Jamaa*:-mpaka form four.
*Boss*:-unajua kingereza?
*Jamaa*:-kwani hao wezi wanakuja na wazungu???.
😅😅😅😅😅😅
Angalia alichokifanya huyu mkaka alipoenda benki 🏦
At the bank..
Teller: Hii pesa ni fake
Mkaka: Shida iko wapi..pesa ni yangu..account pia ni yangu..weka tu!!!😂😂😂
🏃🏃🏃🏃
Cheki huyu dingi alivyo mnoko
Unamtumia baba ako meseji ukiwa shule “Baba naomba unitumie 100,000 ya pckt mny” anakuuliza “pckt mny” ndo nini? Unamjibu ni kifupi cha “pocket money” af ankutumia 10,000, unamuuliza hiyo hela ni ya nini? Anakwambia ni kifupi cha 100,000.
Hapo ndo unatamani kuchoma shule ufe.
Dunia ina mambo, soma hii
Dunia ina mambo
Kuna mama mmoja kavamia bank uchi cha kushangaza hakuna anae kumbuka uso wake😂😂😂😂😂
Kilichonitokea leo baada ya kuona nungunungu
Baada ya kukaa mda mlefu sijamuona nungu’nungu leo nikakuna nae nikajisikia furaha sana,
nikaona bora niende nikamkumbatie !! kutokana na kukaa cku nyingi sijamuona!
Dah! Alichonifanyia nung nung sitokisahau !!!
Misemo 10 bora ya kuchekesha itakayokuacha mdomo wazi
1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.
2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.
3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?
4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.
5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.
6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.
7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.
8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.
9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.
10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi
kufunika sufuria.
Angalia huyu mgeni anachokifanya, wageni wengine ni hatari
Hata kama ni Mgeni this is too much.
Mwenyeji: Karibu mgeni karibu ukae,utapenda chai au soda?
Mgeni: Nipe nianze na soda wakati chai inachemka.
Mwenyeji: Utakunywa fanta au sprite?
Mgeni: Nipe fanta wakati sprite inapoa.
Mwenyeji: Utakunywa na keki au mkate?
Mgeni: Nipe keki mkate nitanywea chai ikishachemka.
Mwenyeji: Utapendelea ndiz au machungwa,
Mgeni: Nipe machungwa ndizi ntakula na wali
mchana.
Chezea mgeni ww.!!!
Kwa nini watu hawapendi hesabu!! Sababu hii hapa!
Sababu ni hii
AL-SHABAB
AL-QAEDA
Kwenye MATHEMATICS pia kuna kundi linaitwa
“AL-GEBRA”
😂😂😂😂
🚶🏻🚶🏻🚶🏻🚶🏻🚶🏻🚶🏻
Kumbe ndo maana wengine hawapendi hesabu coz kuna element za ugaidi
Lugha za namba ni noma
Leo kuna mdogo wangu nimemtumia meseji nimemuomba aniazime chaja yake ya simu. Akanijibu 21002 Nikawa mkali nikamuambia kuchajia mara moja tu ndio HELA yote hio si bora nikanunue Chaja yangu mpya. Akaniambia nimesema TUMIA TU 😂😂mtatuua na lugha zenu😜
Huu ndio Umuhimu wa English katika mapenzi
HUU NDO UMUHIMU WA ENGLISH KATIKA MAPENZI
jaribu kumwita mpenzi wako “my sweet potato” atakuelewa ila mwite kwa kiswaili ” *kiazi wangu mbatata*”hiyo itakuwa vita ya tatu ya dunia😁😁
Kilichowakuta boss, mke wake na mfanyakazi wao
Bakari ni house boy mara nyingi huiba wine ya boss wake na kisha kuongeza maji kwenye chupa ili boss asigundue.
Mara kadhaa boss alihisi ladha tofauti anapokunywa wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu alihisi tu Bakari anahusika.
Ilikua ni bahati tu alimvizia na
kumbamba Bakari akichakachua wine, kwa kuwa mkewe alikua
anamtetea Bakari, ili kumthibitishia mkewe kuwa Bakari ndo culprit, boss alianza kwa kumuuliza Bakari maswali.
Siku hiyo Bakari alikua jikoni, boss na mkewe walikua sebuleni.
Boss: Bakariiii!
Bakari: Naam baba!
Boss: nani anakunywa wine yangu?
Bakari kimyaaaa hajibu kitu!
Boss: Bakariiiii !
Bakari: naam baba!
Boss: nauliza nani anakunywa wine yangu halafu anajazia majiii!
Bakari kimyaaaaa!
Boss akaamua amfuate hukohuko jikoni.
Boss: Kwanini nikikuita unaitikia, nikikuuliza unanyamaza?
Bakari: baba huku jikoni ndo kulivyo, unasikia jina tu likiitwa lakini maneno menginehusikii, na kama huamini baki jikoni mi niende sebuleni.
Bakari akaenda sebuleni akaanza kuita.
Bakari:Babaa!
Boss: naam Bakari!
Bakari: Saa sita usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl?
Boss kimyaaaa!
Bakari: Baba babaa!
Boss:ndio Bakari!
Bakari: Nauliza hivii, chumbani kwa house girl saa sita za usiku huwa wafuata nini?
Boss kimyaaaaaaa!
Boss akatoka nje: Bakari huku jikoni ni kweli husikii kitu zaidi ya jina!
Mke wa Boss akaingilia kati
Mama: nyie msinitanie kabisa mnasemaje?
Bakari: kweli mama ukiwa jikoni husikii kitu nenda uone
Mama akaenda na Bakari akaanza
Bakari: mamaaaa!
Mama: abeee!
Bakari: hebu niambie hiyo mimba ni ya baba au yangu?
Mama kimya
Bakari: mamaaaa!
Mama: abeeee!
Bakari: hebu niambie ukweli hiyo mimba ni ya baba au yangu??
Mama kimya
Mama akatoka nje: kweli humu jikoni kuna tatizo nilikuwa nasikia jina tu
Ukata wa January
Boss;- kwa nini umechelewa kazini
Juma;- kuna mtu njiani alidondosha elfu1
Boss;- ohhoh kwa hiyo ulikuwaunamsaidia kuitafuta
Juma;- hapana nilikuwa nimeikanyaga
😃😃😃😃😃😃😃😂😂😂😂😂😂😂
Jambo usilolijua kuhusu mwili wako
JE WAJUA!…..
Msuli mrefu kuliko yote kwenye mwili wa binadamu unaunganisha kope za macho na sehemu ya kutolea haja kubwa ndo mana kila ukijaribu kubana jicho moja sehemu ya haja kubwa hufunguka bila kutarajia?
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Nakuona unavojaribu kubana jicho …..
UTAKUJA KUNYA BUREEEE, hutaniwiii?!
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Angalia huyu msichana alichonifanyia
Kuna siku nilichalala kipesa nikaamua kuomba dem wangu aniazime 10,000/= akanipa.
Baada ya siku mbili nikapata pesa zaidi ya laki nne hivi, nikaamua kumpa 100,000/= mpenzi wangu bila yeye kuniomba.
Baada ya siku 3 akaja kuniambia:- “Bae, ile 10,000/- niliyokuazima mwenyewe amekuja kunidai, so kama unayo naomba unipe nimrudishie maana ananisumbua leo siku ya 3.”
SAA HIZI NIPO ZANGU SINGLE NATAFUTA DEM MWINGINE
Kilichotokea wakati mchungaji akifungisha ndoa ya Mashoga
Mchungaji mmoja baada ya kuwafungisha ndoa “MASHOGA” wawili alipata wakati mgumu kutamka kuwa “sasa ninyi ni MKE na MUME”
atafanyaje wakati wote ni wanaume? mchungaji akapiga moyo konde na kusema “tangu sasa ninyi ni MAN UNITED”
Duh! Hiki nacho chombo cha moto?
_Sheria inasema kila anaetembea na chombo cha moto barabarani sharti awe na leseni._
_Sasa hawa wauza kahawa mbona wanatembea na chombo cha moto lakini hawakamatwi 😡._
_Hizi sheria zinapendelea._
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Ulevi noma! Angalia huyu mlevi alichomfanyia huyu jamaa usiku! Ungekua wewe ungefanyaje?
Jamaa alikuwa amelaa na mkewe saa tisa ya usiku akastuka baada ya kusikia mtu anabisha hodi kwenda kufungua mlango
Akamkuta jamaa kalewa sana mlangoni kwao
JAMAA: Nini tena mheshimiwa kuamshana saa hizi?
MLEVI: Naomba uje unisukume.
Jamaa akiamini kuwa pengine kuna gari la huyu mlevi limezima jirani akamwambia subiri nikavae viatu. Baada ya kuvaa viatu akatoka na wakaanza kusindikizana na mlevi. Mlevi akaongoza njia
mpaka kwenye mabembea ya jirani akakaa kwenye bembea moja na kumgeukia jamaa na kumwambia.. Okay nisukume basi.
Recent Comments